Kutafakari kutoka Mk 1, 40-45
Injili hii
inatusaidia kutafakari kuhusu ugonjwa katika mazingira ya Yesu. Sio baadhi ya
watu tu walikuwa wagonjwa, bali jamii nzima kwa sababu ilikuwa na mazoea ya
kuwatendea mbaya walio na mahitaji ya utunzaji maalum. Hasa waliokuwa na ukoma
walipaswa kujitenga na wengine na kukabili hali yao. Hao waliwekwa katika kundi
maalum la wenye dhambi kwa sababu walichukuliwa kama waliolaaniwa na Mungu. Mtu
aliyejichanganya nao alipata dhambi yao pia. Hata wana wa familia hawakuweza kuwa kuwakaribia
kwa sababu ya hatari ya kuambukizwa. Ubaguzi wa jamii kwao ulikuwa mbaya zaidi
kuliko hatari yoyote ya kuambukiza. Yesu ndiye mwangalifu kwa hali hii kwa
sababu ni dhidi ya mpango wa Mungu ambaye anataka maisha mengi kwa watu wake
hasa wagonjwa. Hivyo, Yesu mwenyewe hakuwa na hofu ya kuwa mchafu kwa maana ya hali
ya wagonjwa. Yeye aliwakaribia wagonjwa wengi na kuwagusa akivuka mipaka
iliyowekwa na jamii.
Hata
akijua kwamba sheria ilikataza mgonjwa wa ukoma awakaribia watu, wakati mtu
huyo alipomwona Yesu, alimwendea na kutambua kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa kumtakasa.
Alionyesha imani yake katika Yesu na mara Yesu alimwonea huruma. Tunaweza
kutambua uhusiano maalum kati ya tabia hizi mbili, yaani, imani ya mgonjwa na
huruma ya Yesu. Yesu alifunua uso wa Mungu ulio uso wa huruma. Kupitia maneno
na matendo, kila kitu katika Yesu kinadhihirisha tabia hii. Ndiyo huruma ambayo
inamwimarisha Yesu atende. Yeye alimponya mgonjwa kwa sababu alitaka, lakini tena
alitambua na kuthamini sana tabia ya imani ya mgonjwa. Pamoja na kuponya
mgonjwa, tena Yesu alisahihisha mawazo ya uongo kumhusu Mungu katika jamii
ambayo yaliisaidia hali hii mbaya.
Mtu huyo
mgonjwa ni mfano wa hali yetu ya kibinadamu yenye haja ya utakaso na kuponywa
na Mungu. Kwanza kabisa tunapaswa kutambua kwamba sisi tu wagonjwa. Hatuwezi
kumkaribia Mungu ikiwa hatukubali mapenzi yake kwetu. Yeye ndiye wa kwanza
ambaye anataka kuondoa hali mbaya ya maisha yetu, lakini hawezi kutenda
maishani mwetu ikiwa hatumruhusu. Uumbaji mpya ambao Yesu alitenda katika
maisha ya mgonjwa wa ukoma unatendeka katika maisha yetu wakati mapenzi yetu ndiyo
kulingana na mapenzi yake. Tunaalikwa kuamini kwamba Yesu ana hisia sana mbele
ya hali ya wagonjwa kwa sababu hakuja kwa walio na afya nzuri bali kwa
wagonjwa. Kama mtu yule mwenye ukoma, sisi pia tunahitaji
mkutano na Yesu ambao ubadilishe maisha yetu kabisa. Kutokana na hisia yake
tunaalikwa kushinda mawazo ya kijamii ambayo yaendelea kuwalaani ndugu wengi
waishi kutengwa na kubaguliwa. kwa kumfuata Yesu kwa kweli tunapaswa kushiriki katika
hisia zake kuhusu hali ya mateso ya ndugu hawa.
Kuhusu hayo, majira ya kihistoria
yamejaa mifano ya watu ambao walikuwa na uwezo na ujasiri wa kutenda dhidi ya
mawazo wa kijamii kuhusu wagonjwa na walio na mahitaji mengi. Mfano moja kati
yao ndiye Mtakatifu Yohane Calabria. Mtu huyo anaweza kutusaidia kwa maisha
yake mwenyewe. Kama mfano wa utunzaji wa Mungu, yeye alikuwa na hisia sana kwa hali
ya wagonjwa. Alimwona Kristo mwenyewe katika walio wagonjwa. Alikuwa na mazoea
ya kuwaimarisha kwa maneno ya kutia moyo na kutenda kwa ufanisi kwa ajili ya
mwili wao. Alifikiria mateso ya wagonjwa kama msaada mkubwa kwa ajili ya mtume wa Kanisa. Aliwaimarisha na
kuwashauri wagonjwa kuukaribisha ugonjwa na mateso kwa uvumilivu na sala. Kristo
mwenyewe aliwapenda wagonjwa na wakati wa maisha yake alikwenda mara nyingi
kuwatembelea na kuwaponya. Tunaalikwa kumkaribia Yesu na kuruhusu atuponye
kutoka ugonjwa wetu wa kiroho ili tuwe mwenye hisia kuhusu hali ya walio
wagonjwa wa kimwili.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário