quarta-feira, 7 de outubro de 2015

MUNGU BABA YETU KATIKA BIBLIA NA KATIKA MAWAZO WA Mt. YOHANE CALABRIA

katika siku hii ya maadhimisho ya sikukuu ya Mtakatifu Yohana Calabria nataka kupendekeza kutafakari kuhusu UBABA WA MUNGU. Tunamshukuru Mungu Baba ambaye ametupa Yohane kama nyota mbinguni na nuru karibu nasi. 
YOHANA WA MASKINI (M: Jorge Trevisol – Translation to Kiswahili: Fr Ndega)
- Imba viumbe vyote! Hii ni siku kwa wote/ Mungu alitupa Yohana, nyota mbinguni, nuru karibu nasi/ imba viumbe na watu!/ imbeni kwa furaha kubwa!/ uhai unapendeza Mungu/ ana upendo wa Baba kwa maskini wake/ Ref: /: Imba Yohana wa maskini, kwamba dunia itakusikiliza/ Mungu aliyefanya mvua, jua, bahari na ni Baba yetu pia.:/ 2. Ninahisi upo karibu/ naimba na unaimba nami/ unasema kwa nyuso za wengi kwa uhai dhaifu ndani yangu unakutafuta/ ufukuze hofu yetu/ kila wakati una nguvu/ Kuishi sasa kwa muda ni kuhisi kwamba wewe ni yote milele/ 3. kwa sababu uliishi hayo/ kwa sababu ulituambia/ vivyo hivyo tutaishi/ pamoja na wewe/ kamwe bila na wewe/
MPANGO WANGU WA KUTAFAKARI
Utangulizi
1 Ubaba wa Mungu katika Biblia
            1.1 neno Baba kwa uhusiano na Mungu katika Agano la Kale
            1.2 neno Baba katika Injili
            1.3 maneno Mungu Baba ni yenyewe ya Waraka wa Mitume
            1.4 Yesu anamdhihirisha Mungu kama Baba
            1.5 “Sala Baba yetu ni awali ya Injili” (Mt. Yohane Calabria)  
2 Uzoefu wa Ubaba wa Mungu kwa Mtakatifu Yohana Calabria na Familia yake ya Kiroho
Hitimisho

Utangulizi
Msomo wa kutafakari kwetu ni kuhusu Mungu Baba au ubaba wa Mungu. Bila shaka kwamba baada ya tutafute maana ya maneno haya katika Biblia, rejeo kwa kutafakari kwetu itakuwa maandiko, mawazo na mtazamo wa Mtakatifu Yohana Calabria. Msomo huu kuhusu ubaba wa Mungu ni jambo la msingi la kiroho ya Calabria. Ni vizuri sana kujua kwamba Yohana Calabria aliwekwa mtakatifu katika mwaka wa Mungu Baba ambao ulikuwa sehemu ya mwisho katika maandalizi kwa sherehe ya yubilei ya Miaka elfu mbili ya kuzaliwa kwake Bwana Yesu Kristu.
Mwanaume huyo mkuu anayeitwa Yohana Calabria alizaliwa terehe nane mwezi wa kumi mwaka wa elfu moja mia nane sabini na tatu. Alikuwa maskini sana kwa mtazamo wa kibinadamu na tajiri sana kwa upande wa Mungu. Kulingana na uzoefu wake tunajifunza kwamba hatuweze kuongea kuhusu Mungu ikiwa hatupitii hayo. Na huu ulikuwa uzoefu wake, yani, Mungu ni Baba na Mtoaji. Ingawa hali mbili inatokea pamoja katika Mungu, tutatafakari kuhusu ubaba peke yake.

1 Ubaba wa Mungu katika Biblia

1.1 neno Baba kwa uhusiano na Mungu katika Agano la Kale
Maneno Baba yetu si maneno ya Yesu tu, kwa sababu kabla yeye yalitumika katika maandiko ya manabii ya Agano la Kale. Bila shaka Yesu hakuyatumia maneno haya tu, bali alianzisha uhusiano mpya na Mungu, akileta maana mpya kabisa kwa maneno Baba yetu. Neno Baba kwa uhusiano na Mungu, tunaweza kukuta katika: Isaya 9:6 (Baba milele); Is 63:16 (wewe ni Baba yetu - mara mbili); Is 64:8 (wewe ni Baba yetu); Yeremia 3:4.19 (Baba yangu – mara mbili); Malaki 2:10 (Tuna Baba mmoja)

1.2 neno Baba katika Injili
Kuhusu injili hali ni tofauti sana kwa sababu neno hili lilikuwapo midomoni mwa Yesu daima, yaani, Baba, Baba yangu, Baba yenu, Baba yake, Baba Yako, Baba yao, Baba yetu,etc. Katika Mathayo - mara 42; Marko – mara 5; Luka - mara 16; Yohane – mara 114. Tunaweza kusema kwamba Yohane ni “Injili ya Baba” kwa sababu inaongea sana kuhusu uhusiano wa Yesu na Baba yake. Tena tunatambua kwamba katika toleo hili peke yake tunaweza kufanya maneno kama Baba mtakatifu, Baba mwenye haki, Baba yangu na yenu pamoja, etc. Katika matoleo ya Mathayo, Marko na Luka tunakuta uzoefu wa ubaba kwa uhusiano na huruma na kujua, kwa nfano, Baba atawasamehe, Baba yenu anajua,etc.  Lakini sala ya Bwana inayojulikana kama Baba yetu, tunaweza kukuta katika Mathayo na Luka peke yao.

1.3 maneno Mungu Baba ni yenyewe ya Waraka wa Mitume
Maneno mawili pamoja, yaani, Mungu Baba, tunakuta katika Agano Jipya peke yake na hasa katika Waraka: Wagalatia 1,1; Waefeso 6,23; Wafilipi 2,11; Wakolosai 3,17; 1Wathesalonike 1,1; 2Wathesalonike 1,2; 1Timotheo 1,4; 2Timotheo 1,4; Tito 1,4; 1Petro 1,2; 2Petro 1,17; 2Yohane 1,3; Yuda 1,1. Mara nyingi maneno haya Mungu Baba yanatumika kuonyesha shukrani au utambulisho kuhusu zawadi za Mungu katika jumuyia. Yanaonyesha pia matakwa ya mtume mwandishi kuhusu safari ya imani ya jumuiya fulani.

1.4 Yesu anamdhihirisha Mungu kama Baba
Yesu anapoongea na Mungu na kuhusu Mungu, anatumia neno Baba. Hali hii inatafisiri uzoefu wa ndani, ushirika wa upendo na uhai kati ya Mwana na Baba yake. Maisha yake na uzoefu wake na Baba ni mwaliko kwa wasikilizaji washiriki katika ushirika sawa, wakiishi kwa uzoefu wa ndani na Mungu. Yesu anatuletea ufunuo wa uso kweli wa Mungu: wa kwanza - Mungu aliye na wasiwasi kwa utunzaji wa upendo kwa kila kitu, “hata nywele moja ya kichwa chetu” (Lk 21,18); wa pili - Mungu Baba, ambaye ana watoto tofauti na anashiriki zawadi zake na wote kwa njia sawa. Anawapenda wote na anataka kwamba watu wote wajihisi kuishi katika familia, washiriki furaha yake kama Baba. Katika familia hii anautoa utunzaji na ulinzi ambao ni maonyesho ya upendo wake wa Baba. Tuko katika ushirika wa ndani naye ikiwa tunashiriki hisia zake kuhusu wengine. Kwa hivyo Yesu alitufundisha kusali, akishiriki nasi njia yake yenyewe ya kusali. Alitujulisha kujua huyo ambaye ni Baba yake na Baba yetu pia.

1.5 “Sala Baba yetu ni awali ya Injili” (Mt. Yohane Calabria)

Mantra: Baba sikia wanao, sikia sauti zao, sikia dunia nzima...
Yesu anapowafundisha wanafunzi wake kusali, aliwakumbusha kuhusu mahitaji ya tabia ya mwana anayemwomba Baba kwa imani. Kama yeye alivyoishi, tabia kamili ya wanafunzi lazima kuwa kujisalimisha mikononi mwa Huyo anayejua mahitaji ya wana kabla ya wamwulize kitu. Sala ya kweli ni kitendo cha kujisalimisha. Sehemu ya kwanza ya sala ambayo Yesu anawafundisha wanafunzi wake ni utambulisho wa ubaba wa Mungu, ambaye ni mwema na mtoaji. Katika sala hii, kila kitu ambacho kinaja baada ya Baba kinategemea kwa neno hili/mwelekeo/hali. Ni lazima kufanya mapenzi ya Mungu ili Ufalme wake utokee duniani kama mbinguni. Mapenzi ya Baba huyu lazima kuwa chakula cha watoto wake kama kilichotokea na uzoefu wa Yesu miongoni mwa wanadamu.  
Kwa Baba huyu sisi lazima kuhutubia kwa imani, wenye uhakika kwamba tumepokea sana. Tunaomba kwa mkate, msamaha na upatanisho. Kulingana na Maandiko matakatifu, “kutokana na wema wake tumepokea neema juu ya neema”. Sala hii inathibitisha utunzaji wa upendo wa Mungu anayeshiriki zawadi zake na wana wake, akitarajia kwamba tufanye vivyo hivyo na wengine ili udugu uwe maonyesho ya kweli ya ubaba wake na chombo cha huruma yake. Maombi Baba yetu yanatufundisha kufikiri kuhusu mahitaji ya wengine na si kwa mahitaji ya kibinafsi tu. Kupitia sala hii tunaomba muhimu zaidi, yaani, “mkate wa kila siku” kwa sababu sisi lazima kupinga dhidi ya aina yote ya ukusanyaji na ubadhirifu ambao unaharibu udugu, kufanya maskini na wenye njaa wateseke. Kuhusu mambo haya Baba Mtakatifu Francisco asema: “Ulaji umetuongoza kutumia chepesi pamoja na ubadhirifu wa chakula cha kila siku... sisi lazima kukumbuka kwamba chakula ambacho sisi hutupa takatakani ni kama ikiwa tulikuwa tumeiba kutoka meza ya walio maskini na wenye njaa.”
Kwa Mt. Yohana Calabria, “sala Baba Yetu ni awali ya Injili. Matatizo lazima kufikiriwa na kusomwa kwa uhusiano na maelewano kwa ubaba wa Mungu.” Ikiwa tunasema “Baba Yetu” ni kwa sababu tunasadiki kwamba sisi ni ndugu wa wengine wengi. Mungu hawabagui watu na hamsahau yeyote wa wana wake. Hapendezwi na sala ambayo haifikirii ndugu wengine. Mungu si daima anatupa vitu ambavyo tunamwomba, bali anatupa daima vitu tunavyohitaji kwa sababu anajua kila kitu. Ikiwa mara nyingi hatupokei vitu ambavyo tunamwomba ni kwa sababu hatuombi ipasavyo. Labda kutokuwa na tabia na nia kamili iliyodaiwa na Yesu wakati aliwafundisha wafuasi wake kusali. Tunaalikwa kuishi kwa udugu kutokana na ubaba wa Mungu na kuwa na mioyo ya wana, kwa sababu mtu asiyeishi kama mwana hajifunzi kuwa ndugu.

2 Uzoefu wa Ubaba wa Mungu kwa Mt. Yohana Calabria na kwa Familia yake ya Kiroho
Mantra: Baba yetu sisi ni wanawe, Baba yetu sisi ni ndugu...
Mt. Yohane Calabria alikuwa mwenye unyeti daima kwa ishara za utunzaji wa Mungu ulimwenguni. Lakini usiku mmoja wakati yeye hakupata kulala usingizi, alichukua injili na aliufanya ugunduzi mkubwa. Aligundua jinsi ya kuishi kwa uhalisi ubaba wa Mungu. Kifungu ambacho kiliichukua uangalifu wake zaidi kilikuwa Mt 6,24-34. Kutokana na kifungu hiki alichukua ahadi kwake na kwa familia yake ya kiroho, yaani, “Mtafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake; na hayo yote mtapewa kwa ziada.” Kulingana naye kwa kushuhudia duniani kwamba Mungu ni Baba, Mama, Kila Kitu, tunahitaji kwanza kufanya sisi wenyewe uzoefu wa ubaba wa Mungu na kulima hisia ya miliki ya Baba huyu. Kama hivyo alimwambia mama fulani: “Sisi ni wa Mungu, Mungu ni Baba, Mama Kila kitu chetu. Upende Bwana na atakuwa heri (mwenye furaha)” (24-1-1930).
Kwa yeye, “Mungu ni Baba na Baba mwema. Hakuna mama ambaye anawapenda sana watoto wake kama Mungu anawapenda watu wote na kila mmoja wetu”. Calabria anaongea pia kuhusu Mungu kama Riziki, kwa sababu kulingana naye, haiwezekani kutenga Ubaba wa Mungu na Riziki yake. Kwa hivyo, asema, “Riziki ni Mama mpole ambaye hupatia kila kitu kwa wema wetu, hata kwa wema wetu mkubwa. Tunapaswa kuhisi tumebebwa kwa mikono yake ya mama”. Yohana Calabria aliamini katika ukweli huo na aliyapanga maisha na kazi zake zote kulingana na hali hii. Katika mwanzo mwa kazi yake, alipoonekana mtoto wa kwanza, Yohana alifahamu kwamba Mungu akatarajia kutoka kwake imani maalum ambayo huonyeshwa kupitia matendo mema kwa masikini wapendelewa na Mungu. Baada ya mtoto wa kwanza, wengine wengi walikuja nyumbani. Nyumba hiyo iliitwa “Nyumba ya wavulana wema”. Kama hii, ishara ya mapenzi ya Mungu ilikuwa wazi sana kwa Yohana Calabria.
Kupitia uzoefu ambao Mt. Calabria aliishi kuhusu ubaba wa Mungu, akawa mshahidi na mhubiri wa ubaba huu. Kama hivyo asema, “Injili anatuongelea, kwa mfano, Mungu ni Baba, anatujali zaidi kuliko ndege wa angani na maua ya mashamba hata atatujalia kile ambacho tunahitaji kwa chakula na kwa mavazi, lakini tunapaswa kuutafuta kwanza Ufalme wake na haki yake. Basi, je, imani yetu katika ubaba wa Mungu ni nzuri? Je, tena ni nzuri imani yetu katika Riziki yake takatifu na wema?” 
Imani kweli na asili inafikiria Mungu si kama Muumba na Bwana tu, bali kwanza kama Baba”. Mungu ni Baba, hutujali na wote ambao tunawapenda; macho yake ni makini sana kwa kila kitu; hakuwezi tokea chochote kisichotarajiwa kama mshangao (bila maana); kila kitu kinapangwa na kuongozwa na hekima, nguvu na wema wake pasipo mwisho. Juu ya yote tunaweza kusema kwamba ni kwa wema wake.

Hitimisho
Uzoefu wa ubaba wa Mungu ulimhamasisha Yohane Calabria kuanza Kazi kubwa. Katika mwanzo, padre Yohane alisaidiwa na mama yake. Lakini, baada ya wakati mchache, walikuja Mabruda, Mapadre, Masister, makundi mengi ya watu wasio watawa. Pamoja na padre Yohana, sisi ni Familia ya Kiroho ya Calabria inayoitwa “Poor Servants of Divine Providence” na kazi yetu ni kutafuta Ufalme wa Mungu. Hali hii inatokea katika ahadi ya kuifufua imani duniani kwa Mungu Baba wa wanadamu wote, kupitia kujisalimisha kabisa kwa Riziki yake. Kiroho yetu ni Injili. Kulingana na Mtakatifu Yohana Calabria, tunahitaji kurudi kwa Injili daima ili maisha yetu yabadilike na hali kandokando yetu pia.
Maandiko ya Mt. Yohana Calabria yanadhihirisha jinsi alivyokuwa na ubinadamu mno, akifahamu ugumu wa wengine, lakini kwa wakati sawa, alijua kuonyesha njia kamili kwa ufumbuzi wa matatizo yao. Kutokana na uzoefu wa Mt. Calabria tunajifunza kwamba Mungu ni Baba mwema na mtoaji bila mwisho, na sisi sote ni ndugu katika Kristo. Tunaalikwa kuishi kama ndugu kutokana na ubaba wa Mungu na kuwatendea mema wengine vivyo hivyo tungependa wao watutendee. Kulingana naye, “Tunapaswa kuwa na kujihisi watumishi, bali kwa utumishi wa Mwenyeji fulani ambaye ni pia, na kwanza kabisa, Baba. Basi utumishi wetu ni wa wana, utumishi wa huria na upendo... kama alivyotumika Bwana wetu Yesu Kristo, mtumishi wa Baba kwa namna ya ajabu, ambaye wakati wa maisha yake ya kibinadamu alifanya tu kutimiza amri zako: “Ninafanya kama Baba alivyoniamuru kufanya.”

Tumsifu na tumshukuru Mungu Baba kwa kielelezo cha imani ambacho ni Yohane Calabria na mtume wake duniani kupitia Familia yake ya Kiroho. 

Fr Ndega
Mapitio: Sara  

domingo, 4 de outubro de 2015

IN THE BEGINNING GOD CREATED WOMAN AND MAN


Reflection from Mk 10:2-16

    In the beginning of today’s gospel Jesus was teaching the people as he always did. Suddenly some Pharisees came to him, trying to trap him. The matter was about divorce. Jesus perceived their bad intention, but even so welcomed them well, listening to them with patience and valuing their effort in questioning him. In the dialogue with Jesus, their unique problem was the deficient vision about matrimony and family. Jesus corrects this mentality, reminding them about the original plan of God concerning man and woman. He speaks also about adultery as result of the divorce and shows special relationship with the children who merit to be respected and valued so that they can grow in security and joy.

      Some Pharisees use the Law of Moses to trap Jesus. According to their mentality, this Law allows divorce, but Jesus doesn’t agree with them. Why does Jesus have a different position in relating to this matter of the Law? According to the Book of Deuteronomy 24, the man can write a letter of divorce if he finds something in his wife which he doesn’t like. The woman had very few opportunities to present letter of divorce to his husband, for example, if the husband was infected with leprosy. In this context the situation of the woman was very difficult because she was bullied and depended of the good will of the man. But Jesus helps them to think better because the Law was made for the good of the people and not the people for the good of law.

    The position of Jesus is very clear. He came to reveal the original plan of God and according to this plan, both man and woman have been created liked and resembled God and God shared with them his love which makes them to desire one another and at last to leave their parents, to unite themselves and be one body. This reality shows that the man doesn’t have right to do what he wants with his wife, for example, to abandon the wife in any moment he wants. So, their union means that they cannot abandon each other or to be separated. The main objective of Jesus is to recover the dignity of the woman removed by the Law. According to Jesus woman has right of being respected in the matrimonial life and not being mistreated or dominated like possession. The intention of God is that husband and wife continue growing in love and lastly get eternal life. And we can share this plan of God of living unity of life in our families or communities.   

       Human desire to love and to be loved is the reason of the existence of the marriage and the family. The family is the base of human experience and anything which goes against this principio is prohibited in the Bible. For that “don’t commit adultery” is included among the Ten Commandments. Why does adultery threaten the family? Adultery can destroy a family because it can result in pregnancy and the birth of a child. That child will start out life with no family. If adultery doesn’t destroy a family, it almost always causes terrible harm to a marriage, such as sense of betrayal and loss of trust which means that adultery causes a fraudulent life. It is necessary to be careful with some kinds of friendship. When the husband or wife has some friendship with relationship stronger than which he/she has with the spouse it is more difficult to resist to the adultery. When a husband or wife is having sex with someone other than their spouse, the thought cannot release about another person and how to deceive the spouse. Adultery doesn’t protect the family and doesn’t protect the spouses from emotional pain.  


     Protecting the family is the reason for the commandment. Why the family is so important? Because without it the social stability is impossible. Because without it the passing on of society’s values from generation to generation is impossible. Because the relationship between parents and children make them more responsible and mature. Because more than anything else the family satisfies emotional and material needs, giving to the children secure and stable childhood.

Fr Ndega
Review: Sara

MWANZO MUNGU ALIWAUMBA MWANAMKE NA MWANAMUME


Kutafakari kutoka Marko 10:2-16

     Mwanzoni mwa injili ya leo Yesu alikuwa akiwafundisha watu kama ilivyokuwa desturi yake. Ghafla baadhi ya Mafarisayo walimwendea wakimjaribu. Jambo lilikuwa kuhusu talaka. Yesu aliitambua nia yao mbaya, lakini aliwatendea mema, akiwasikiliza kwa utulivu na kuthamini juhudi zao za kumwuliza maswali. Katika mazungumzo na Yesu shida yao ya pekee ilikuwa mtazamo pungufu kuhusu ndoa na familia. Yesu alisahihisha mtazamo huo, akiwakumbusha mpango asili wa Mungu kwa mwanamume na mwanamke. Aliongea pia kuhusu uzinzi kama matokeo ya talaka na kuonyesha uhusiano maalum na watoto wadogo ambao wanastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa ili wakue kwa usalama na furaha.

      Baadhi ya Mafarisayo wanatumia sheria ya Musa kumjaribu Yesu. Kulingana na mawazo yao, Sheria hiyo inaruhusu talaka, lakini Yesu anayakataa hayo. Kwa nini Yesu ana msimamo tofauti kwa uhusiano na jambo hili la Sheria? Kulingana na Kitabu cha Kumbukumbu la Sheria, sura 24, mwanamume aliweza kumpatia mkewe talaka ikiwa hakupendezwa naye kwa sababu ameona kwake kitu kisichofaa. Mwanamke alikuwa na nafasi chache za kutoa talaka kwa mmewe, mfano mwanaume akiugua ukoma. Katika mazingira haya hali ya mwanamke ilikuwa ngumu sana kwa sababu daima alionewa na daima alitegemea huruma tu ya mwanamume. Lakini Yesu aliwasaidia kufikiri vizuri kwa sababu Sheria zimewekwa kwa manufaa ya watu na si watu kwa ajili ya sheria.

      Msimamo wa Yesu ni wazi sana. Yeye alikuja kudhihirisha mpango asili wa Mungu na kulingana na mpango huu, wote mme na mke wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na Mungu ameweka upendo asili unaowafanya watamaniane na hatimaye kuwaacha wazazi wao, kuungana na kuwa mwili mmoja. Jambo hili linaonyesha kuwa mwanaume hana haki ya kuamua atakavyo kwa mkewe, mfano kumwacha mke wake kwa muda wowote anaotaka. Hivyo kuungana kwao kunamaanisha kuwa hawawezi kuachana au kutenganishwa. Lengo kuu la Yesu, ni kukarabati nafasi na utu wa mwanamke ulioharibiwa na sheria. Kulingana na Yesu Mwanamke ana haki ya kuheshimiwa katika maisha ya ndoa na si kutendewa na kumilikiwa kama chombo tu. Nia ya Mungu ni kuwa mume na mke waendelee kukua katika pendo na kupata uzima wa milele. Nasi tunaweza kuushiriki mpango huu wa kuishi maisha ya umoja katika familia na jumuiya zetu.

     Thamani ya kibinadamu ya kupenda na kupendwa ni maana ya uzoefu wa ndoa na familia. Familia ni msingi wa uzoefu wa kibinadamu na yoyote ambayo ni dhidi ya kanuni hii ni marufuku katika biblia. Kwa hiyo “Usizini” ni moja miongoni mwa Amri Kumi. Kwa nini uzinzi hutishia familia? Uzinzi unaweza kuharibu familia kwa sababu unaweza kusababisha ujauzito na kuzaliwa kwa mtoto. Mtoto huyo ataanza safari ya maisha pasipo familia. Ikiwa uzinzi hauharibu familia, mara nyingi unasababisha madhara ya kutisha ndoa, kama hisia ya usaliti na upotevu wa itibari ambayo inamaanisha kwamba uzinzi unasababisha maisha ya ulaghai. Ni lazima kuwa macho kwa baadhi ya aina za urafiki. Wakati mume au mke ana urafiki fulani ambao anaanzisha uhusiano wa nguvu zaidi kuliko ule anaoishi na mke au mume, ni ngumu sana kuuepuka uzinzi. Wakati mume au mke ana ngono na mwingine kuliko mkewe/mumewe, mawazo kuhusu yule mtu ni daima na mawazo kuhusu jinsi ya kumdanganya mume au mke ni daima pia. Uzinzi haulindi familia na tena hauwalindi wanandoa dhidi ya maumivu ya hisia. 

        Maana ya Amri “Usizini” ni ulinzi kwa familia. Kwa nini familia ni muhimu sana? Kwa sababu pasipo familia uimara wa jamii hauwezekani. Kwa sababu bila familia mawasiliano ya thamani ya jamii kizazi kwa kizazi hayawezekani. Kwa maana uhusiano kati ya wazazi na watoto unawafanya kuwajibika na kukomaa zaidi. Kwa sababu bora kuliko chochote, familia inayaridhisha mahitaji ya hisia na fizikia/mwili, kuwapa watoto utoto salama na imara.

Fr Ndega

Mapitio: Sara 

domingo, 27 de setembro de 2015

KUTENDA MEMA KWA JINA LA YESU


Kutafakari kutoka Hes 11:25-29; Mk 9:38-43, 45, 47-48

Mungu hawabagui watu kwa maana anapenda na katika upendo hakuna ubaguzi. Maatarajio yake ni kwamba watu wake wote wangekuwa manabii, wanasikiliza neno lake na kuongea katika jina lake. Kupitia Roho wake Mtakatifu, anawahamasisha watu ili watende mema kulingana na mapenzi yake, akidhibitisha kwamba tendo lake halina mpaka. Mbele ya Mungu hakuna mtu wa heshima zaidi kuliko mwingine. Yeye hakubali umaarufu au ubaguzi, bali anatarajia ahadi kwa njia yake ya kufikiri na kutenda. Maana kwa njia hii ni upendo wake wa bure kwa wote.

Wanafunzi wa kwanza walijaribu kumkataza mtu fulani kufanya mwujiza kwa jina la Yesu kwa sababu hakuwa mmoja wao. Wlifanya hivyo kwa mamlaka gani? Yesu hakubaliani na tabia hii na akawaambia kwamba mtu ambaye anatenda mema kwa jina lake (Yesu) hawezi kumnenea mabaya. Kisha akiendelea kwa mafundisho yake, alisema kwamba watu wanaosaidia wafuasi wake watapokea tuzo kwa sababu ya utambulisho wake na wale waliotumiwa katika jina lake. Yesu anawakumbusha pia kwamba juhudi yote ya wale wanaomfuata lazima kuwa hamasa kwa wale ambao wanaanza kumwamini Kristo au wana ugumu kumwamini. Kashfa ni jambo mahututi sana na ni lazima kuepukwa kwa sababu huivuruga imani.

Tumetafakari kuhusu ugumu wa wanafunzi wa Yesu kuelewa na kuyapokea mafundisho yake. Wanaelewa nusunusu, hasa ile sehemu rahisi, wanaipokea na kuacha yaliyo magumu. Ni hatari mno kuelewa nusu ya ukweli kwa sababu kama hii tunaweza kuleta uzushi. Kujaribu kumkataza mtu fulani ambaye alifanya mema kwa jina la Yesu ni ishara ya ugumu ya kumfahamu Yesu na mapendekezo yake. Maana ya kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu si maneno tu, bali ni matendo mema hata kama mtu huyu hayumo kwenye kundi. Badala ya kuwakataa wengine ambao wanatenda mema kwa jina la Yesu, wanafunzi wake wanapaswa kujikataa wenyewe. Kuwa mwanafunzi wa Yesu inamaanisha imani iliyoonyeshwa kwa matendo. Kwani wao wanaokiri na kutenda kama kadiri ya neno” ndiyo mama na ndugu zake na wanafunzi wake. Ikiwa huyo mtu alitenda mema kwa jina la Yesu, tayari alikuwa mwanafunzi wake. Mtazamo wa wanafunzi una upungufu na ubaguzi, lakini mtazamo wa Yesu ni mpana na ni kwa wote wenye mapenzi mema.

Kitu muhimu katika dini au imani ni matendo na siyo maneno. Matendo husema zaidi ya maneno. Mifano halisi ni wakristo wa kwanza, waliweza kuwavuta wengine si kwa maneno, bali njia yao ya maisha. Kuhusu wao watu walisema: “Mwone kama wanavyopendana”! hali hii iliwezekana kwa sababu ya upendo wao ulionyeshwa kupitia ridhaa wao kwa wao, kushiriki pamoja, uvumilivu katika maombi pamoja na unyenyekevu wa moyo. Kuhusu hayo Sinodi ya Afrika imesema: “Sharti muhimu la kuhubiri ni ushuhuda wa maisha”. Mwanafunzi wa kweli wa Yesu hawezi kuwa na ubaguzi na kuamini kuwa watu wa kundi lake pekee, au chama chake cha utume, au kanisa lake ndiyo wanafunzi pekee wa Yesu na wameokolewa. Hatuwezi kufikiri kwamba Yesu ni mali yetu. Ikiwa tunahisi karibu na Yesu, hatuwezi kuishi mbali sana na ndugu zetu, kufungwa kabisa kwa hali kandokando yetu na hata kufikiri kwamba tunakuwa na mamlaka ya kuwazuia wengine watende kwa jina la Yesu. Tuko mbele ya kosa kubwa. Sisi lazima kuwa makini sana kuhusu baadhi ya uzoefu ambao unatufungua kwa Mungu lakini unatufunga kwa wengine. Ikiwa imani yetu haituongozi kukutana na wengine na kutambua mema ambayo wanaweza kufanya imani yetu ni utenganisha. Basi, ili Mungu atufundishe kutambua mwendelezo wa kazi zake mbele ya matendo mema ya wakristo na kusaidiana kwa wema wa wote.

Fr Ndega

Mapitio: Sara

domingo, 20 de setembro de 2015

UFUNDISHAJI NA TABIA YA AJABU


Wis 2:12.17; Jas 3: 16-4:3; Mk 9,30-37


       Kifungu hiki kutokana na kitabu cha Hekima ya Sulemani kinaongea kuhusu ushuhuda muhimu wa mtu mwenye haki na upinzani wa wale ambao hawaukubali ushuhuda wake na wanamtendea vibaya, kupanga mauti yake. Hali hii inatokea kwa sababu ya njia ya maisha yake kulingana na mapenzi ya Mungu. Njia hii inawasikitisha wale wanaopendelea kuishi vibaya, mbali na Mungu. Hata hivyo, mtu huyo mwenye haki ni mwana wa Mungu, na Mungu mwenyewe atamtegemeza na kumwokoa mikononi mwa adui zake. Hii ni ishara ya Kristo, aliye Mwana wa Mungu kwa namna ya pekee kabisa. Yeye, katika uaminifu wake kwa mpango wa Mungu, alipata wokovu hata kwa wale waliwakandamiza wengine. Somo la pili linasema kuwa hekima ambayo inasababisha kujua kamili inatoka kwa juu kwa sababu ni Mungu mwenyewe chanzo cha hekima ya kweli. Mtu anayeongozwa na hekima hii anaweza kuwa mwenye moyo safi, tena ni mtu wa amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu na kutenda mema kwa ajili yao.

         Injili ni mwendelezo wa tangazo la Petro kuhusu utambulisho wa Yesu na mwaliko wa Yesu mwenyewe kwa wafuasi wake wamfuate katika kujisalimisha kwake ili wapate uzima. Yesu alitambua kwamba wakahitaji kujua zaidi kuhusu maana ya umasiha wake na kuyafahamu vizuri mapendekezo yake. Kwa hivyo alitumia kipindi maalum kuwafundisha peke yao kuhusu maana kamili ya umasiha aliochagua na uanafunzi. Hakutaka watu wafahamu alipo. Yesu alijaribu tena kuongea na wanafunzi kuhusu mateso, kifo na ufufuko wake, lakini walionekana mbali sana na mwalimu. Hawakuelewa tena kwa sababu walishughulika sana kwa mawazo na nia tofauti. Hata hivyo Yesu anatumia mifano ili waweze kufahamu ufunuo wake. Vipengele vya msingi vya ufunuo huu ni, maana ya kuwa wa kwanza katika ufalme wa Mungu, jinsi ya kumpokea na hatimaye kuwa watumishi katika ufalme wake.
  
         Yesu anadhihirisha utambulisho wake kama Mwana wa Adamu (mtu). Katika Agano la Kale tunakuta maneno haya katika kitabu cha nabii Danieli na Ezekieli. Kulingana na Daniel Mwana huyu ni hali ya utukufu wa yule ambaye atakuja siku ya mwisho (Dan 7:13). Kulingana na toleo la Ezekieli maneno Mwana wa Mtu yanatumika kueleza ubinadamu na kifu chake (Ezk 2:1,3:1, 25, 17:2). Hii ni maana iliyotumiwa na Yesu ili kuongea kuhusu utambulisho wake kwa uhusiano na hali ya binadamu na fumbo la mateso, kifo na ufufuko wake kwa ajili ya wenye dhambi. Kulingana na injili ya Marko Yesu ni mwenye unyeti mbele ya hali ya ujinga na udhaifu wa wanafunzi wa kwanza; aliwafundisha polepole na kwa uvumilivu, akitumia mifano kadiri ya mazingira na akili zao na kufungua ufahamu wao ili waelewe mpango wa Mungu. Mtoto alijulishwa na Yesu ni tena sehemu ya ufundishaji na tabia yake ya ajabu.

         Watoto wadogo wana mahali maalum moyoni mwa Yesu. Alisema kwamba Ufalme wa Mungu ni wa watoto na mtu ambaye anataka kuingia katika Ufalme huu anapaswa kuwa kama wao. Siku hizi Yesu anatuongelea kwamba ni lazima mabadiliko ya mawazo na tabia ili tuweze kumfuata kwa kweli. Tena rejea kwa njia hii ni watoto wadogo ambao wana tabia kamili katika uhusiano wao na Mungu na wengine. Wanatusaidia kutafuta muhimu zaidi ya maisha yaani ukweli, unyenyekevu wa moyo, ufukara na imani kama mtoto mchanga kwa uhusiano na wazazi wake. Kama wanafunzi wa kwanza sisi pia hatupati kufahamu kila kitu kumhusu Yesu na mapendekezo yake, lakini ikiwa turuhusu, yeye anaweza kufungua akili zetu na kubadilisha mioyo yetu ilingane na matarajio yake. Ili mfano wa watoto wadogo utusaidie kufahamu nia za Yesu kuhusu maisha yetu na kukubali mapendekezo yake ili tupate uzima.

Fr Ndega

Mapitio: Sara

quinta-feira, 17 de setembro de 2015

KUJIKANA KUUCHUKUA MSALABA NA KUMFUATA YESU


Kutafakari kutoka Is 50:5-9; Mk 8:27-35

      Yesu alikuwa anatembea pamoja na wanafunzi wake na karibu na Kaisarea Filipi anawauliza maswali kuhusu utambulisho wake kulingana na mtazamo wa watu. Majibu yalikuwa ishara ya kwamba wazo kuhusu Yesu halikuwa wazi sana kwa upande wa watu. Ingawa halikuwa wazi kwa watu, kwa wafuasi wa Yesu lazima kuwe tofauti, kwa sababu kwa Yesu si muhimu sana yale ambayo watu wanafikiri, bali kukiri kwa wafuasi wake. Petro anadhihirisha yale ambayo wanafunzi wengine kumi na mmoja wanajua pia: Yesu ni masiya wa Mungu. Lakini hawawezi kutangaza habari hii kwa sababu ya kutokuwa na maana kamili. Yesu alitambua kwamba wafuasi wake walihitaji ufunuo zaidi na kujifunza vizuri maana ya umasiha wake na masharti kwa uanafunzi wa kweli.

         Mawazo ya wafuasi wa Yesu kuhusu masiya yalifuata matarajio ya wayahudi wengine, yaani, masiya wa kisiasa atakayetumia nguvu zake za kimungu ili kuwakomboa Wayahudi toka ukoloni wa Warumi. Bila shaka kwamba yesu anayakanusha mawazo hayo kwa kuonyesha njia tofauti ya kutimiza ujumbe wake wa masiya, ni kwamba, kupitia mateso, kifo na kufufuka. Umasiha ulichaguliwa na Yesu ni umasiha wa mtumishi mwema kulingana na Somo la kwanza. Utambulisho wa Mtumishi huyo ni kuwa makini kwa sauti ya Mungu ili aweze kufanya mapenzi yake kutumikia kabisa. Kwa kufanya mapenzi ya Mungu mtumishi huyo anapaswa kuteseka na kufa, lakini alisimama upande wa Mungu ambaye alimsaidia akimfanya mshindi. Pamoja na wazo wa wongo kuhusu umasiha wa Kristo, itikio la Petro lilidhihirisha pia baadhi ya upinzani dhidi ya njia ya maisha ambayo Yesu alichagua ili atimize mapenzi ya Mungu. Uamuzi wa Yesu ulikuwa katika ushirika na Baba yake na upinzani dhidi ya njia hii ni upinzani dhidi ya mapenzi ya Mungu.

    Wanafunzi wa kwanza walihitaji mwendo mrefu ili kujifunza kumhusu Yesu na kuyafahamu mapendekezo yake sawasawa. Wakati Yesu alimkemea Petro na kumwalika afuate mtazamo wa Mungu, alihitajika rejea za nguvu kwa uanafunzi wa kweli. Kidogo kidogo walitambua kwamba kwa kujitoa kama Yesu alivyo, walipaswa kuzifuata hatua tatu, yaani, kujikana wenyewe, kuichukwa misalaba yao na kumfuata Yesu. Kwa maneno mengine, walipaswa kuyabadilisha maisha yao kwa jumla. Kama hii ni lazima kuwa kwa sisi sote. Wale ambao hukutana na Yesu hawakubaki walivyo na hawawezi kumdai Yesu atende kulingana na mapendekezo yao. Mwendo lazima kuwa tofauti. Kwa kumfuata Yesu kweli tunapaswa kupatikana kwa kila kitu na kuweka ndani ya maisha yetu mapendekezo ya Yesu. Tunapaswa kufanya maisha yetu kulingana na njia ya Yesu ya kuishi  na kuchukua msalaba kama yeye alivyo.


      Injili ya Marko katika kifungu hiki inatusaidia kutafakari kuhusu njia ambayo tumechagua ili kumfuata Yesu. Je, hii ni njia ya kweli? Tunatambua kwamba Kumfuata Yesu hakuuleti upendeleo au hadhi, bali mateso na kujisalimisha kwa ajili ya injili. Basi, yeyote ambaye anataka kuishi shwari na bila ahadi hawezi kumfuata Yesu. Yeyote ambaye anatamani kumfuata Kristu bila msalaba hatamfuata Kristo kweli kamwe. Kupitia mambo hayo tunaweza kujiuliza maswali: Je, Kristu gani tumemfuata? Mawazo au kitu gani tunahitaji kujinyima bado ili tuweze kumfuata Yesu kikamilifu? Maisha yetu ya kawaida ni ishara ya kwamba tumekuta hazina yetu ya kweli? Ili Ekaristi hii takatifu itusaidie kuishi wito wetu wa wanafunzi wa Yesu kwa shauku na furaha. Ili ujumbe wa liturujia ya siku ya leo uiimarishe imani yetu na kutuhamasishe kumfuata Yesu kwa uaminifu na tayari kwa kila kitu kwa ajili ya injili, kwa ajili ya ufalme wa Mungu.

Fr Ndega
Mapitio: Sarah

domingo, 6 de setembro de 2015

HE HAS DONE WELL EVERYTHING


Reflection from Isaiah 35:4-7; Jas 2:1-5; Mk 7: 31-37

     According to the First reading, the People of Israel were exiled in Babylon and the prophet Isaiah announced new time, a time of liberation and joy.  According to the prophet that People was like blind person whom lived in the darkness of Babylon and didn’t get to see the way to go back home; they were like paralysed person whom is not able to use the own legs to leave the place where he didn’t feel well; and they were like deaf and dumb person because closed the ear to the Word of God. However God will come to save them because these people belong to God and he loves them. This marvellous action which God will perform to the people of Israel will be assumed later by Jesus for all humanity because he is the salvation of God for all. In the Second reading James invites the Christians to overcome the tendency of discrimination in the community and to value the presence of each one more than his/her economic condition or capacities. The person values for what he/she is.
      
       In the Gospel the good actions of Jesus are recognized by the people, whom exclaimed with enthusiasm, “He has done well everything!” he even causes the deaf to hear and the dumb to speak!” The presence of Jesus brings new time to the world. In him the Kingdom of God became a concrete reality, inviting all to participate. When he announced his mission in the synagogue of Nazareth, place where he was brought up, he was rejected. But he was most welcomed in the side of Galilee, place called Ten Towns. According to Mathew’s version, Galilee is considered Land of Gentiles (non-Jews). The presence of Jesus made the people, whom were in the “darkness”, to see a great light. Although these people had different tongue and customs in relating to Jews of the Judea, they also expected the Messiah anxiously. We get to understand this reality because the Gospel of Mark was written for the Christians of Roma and the objective of this gospel is to answer to the question “Who is Jesus?”. The answer to this question we find in the last moment of the human life of Jesus on the cross from the mouth of the roman army officer: “This man was really the Son of God!” 
       
      As Son of God, the objective of Jesus is to announce the salvation of God not only for some people, but for all. Jesus was a Jews, but not property of the Jews. The signs used by Jesus revealed that the salvation of God is not a plan for the future time only, but it starts in the history and exists for all. When we speak about the “chosen people” we want to mean the plan of wisdom of God whom uses some people in order to reach others more easily. Like this, from the people of Israel, Jesus and his collaborators reached also the ones whom aren’t Jews, proclaiming the good news of the Gospel. That man brought to Jesus had two problems: he was deaf and dumb. He suffered a lot and many times lived isolated because wasn’t able to communicate himself with his neighbours what he thought and desired, and others couldn’t dialogue with him. He desired to meet Jesus and to experience new life in order to perform good relationship with others. Before performing the miracle, Jesus looks at heaven because it is God only whom makes possible to heal the deaf-mute person. 
       

      As followers of Jesus, we are motivated by his decision and gestures. Our mission is continuity of his mission and like him, we are invited to do well everything. The deaf and dumb person is sign of our difficulty to listen to the Word of God and to proclaim it with fidelity. But through us, even with our weaknesses, Jesus continues doing wonders in the life of many people. The gospel doesn’t have borders; in the same way must be the good actions of the Christians. We are invited to overcome obstacles which prevent us to welcome others and to be sensible to their needs. After the people sow the miracle of Jesus and proclaimed it without ceasing, in the same way we must proclaim the wonders of God in order the people experience new life.

Fr Ndega