Kutafakari kuhusu Lk 18, 1-8
Uwepo
wa Yesu ni mahali maalum pa mkutano kati ya Mungu na binadamu. Mara nyingi yeye
hukutana na Baba yake kwa mazungumzo ya ndani akiwapa watu mfano wa sala ya
kweli na yule ambaye anajua kila kitu na ndiye makini daima kwa maombi ya wanao.
Tunapoimba: Baba, sikia wanao, sikia sauti zao, sikia dunia nzima”, tunataka
kumaanisha kwamba Mungu ni Baba na kutarajia tuweze kumhutubia sala zetu kwa
imani kama wenye uhakika kwamba tumepokea sana. Basi, Yesu aliwafundisha
wafuasi wake wafanye kama Yeye alivyo, yaani, kusali daima bila kukata tamaa
kamwe. Ili wafuasi wake wafahamu vizuri mahitaji haya alisimulia mfano mmoja
kulingana na ufundishaji wake wa ajabu.
Hakimu
mmoja wakati wa muda mrefu alikataa kumsikiliza ombi la mama mjane dhidi ya
adui yake na hatimaye alimsikiliza kwa sababu ya kusisitiza kwake. Mfano wa
mama huyo ni lazima kuwa rejeo kwa maombi yetu. Mama huyo alikuwa na uhakika
kwamba yule hakimu akawa na uwezo wa kumtetea kwa hivyo alikuwa na uvumilivu
kuhusu ombi lake. Mama huyo anatujulisha kipimo ili kufikia mafanikio katika
mpango wowote hasa kuhusu uzoefu wa sala.
Kuna
hamu falani ndani yetu ambayo inatuvutia kwa Mungu. Kupitia hamu hii tunatambua
kwamba maana ya maisha ni kukutana naye, kulishwa na uhai wake na kuongozwa
naye kwa sababu bila yeye hatuwezi kufanya chochote. Ikiwa Mungu anachelewa
kuhusu dua zetu ni kwa sababu wakati wake ni tofauti na wetu. Kulingana na kifungu
cha nabii Isaya (55, 6.8), tunaalikwa kumtafuta Mungu daima kwa sababu
anapatikana naye yupo karibu. Changamoto kwetu ni kusali na kusubiri kulingana
na wakati na njia ya Mungu.
Basi,
kusali ni uzoefu wa ndani; ni kumhisi Mungu karibu sana nasi, kwa kuongea kwa
masikio yetu kila siku na siku zote. Kusali ni mazungumzo na Mungu, kwa kutumia
muda wa ubora kuliko wa kiasi. Tunaposali kwa kweli tunahisi kwamba vitu vingi
huanza kubadilisha ndani yetu nasi tunapata mtazamo tofauti kuhusu hali
kandokando yetu. Ingawa hali hii inaendelea kwa ugumu wake na changamoto zake,
mtazamo na tabia yetu itakuwa tofauti kwa sababu tunaimarishwa sio na udhaifu
wetu bali na nguvu ya yule ambaye ana mazoea ya kubadilisha hali mbaya ili iwe hali
mzuri na hali ya mauti ili iwe ya uzima.
Pamoja
na shauri kuhusu mahitaji ya kusali daima Yesu alitupa sala yake mwenyewe, sala
iliye na yaliyomo ya mazungumzo yake na Baba, yaani Baba Yetu. Sala hii tafsiri
hisia za wana ambao wanatambua ukuu na ukaribu wa Baba yao na kwa hivyo wana
uhusiano wa ndani naye. Kwao sala si sharti, bali mahitaji ambayo yanatokana na
ndani yao. Kwao sala ni uhusiano wa upendo kwa sababu wanapata kujiona wapendwa.
Wanapenda kufanya kama mwalimu wao ambaye alisali kutokana na moyo kwa moyo.
Labda
tunahitaji tabia hii kamili kwa sababu tunamwomba Baba mmoja aliye mwema na kujua
mahitaji yetu. Yeye ana macho na masikio yenye hisia kuhusu kile kinachotokea
nasi na yupo tayari daima ya kututendea mema kwa sababu pia hiyo ni njia yake.
Kwa upande wetu tuwe na imani zaidi na kujisalimisha kabisa mikononi mwake kama
Mwanawe wa pekee. Katika sala aliyotufundisha tunasali si kwa mahitaji yetu tu,
bali kwa mahitaji ya wote. Hivyo, ikiwa tunasema “Baba
Yetu” ni kwa sababu tunasadiki kwamba sisi ni ndugu wa wengine wengi.
Mungu hawabagui watu wala kusahau yeyote wa wana wake. Hapendezwi na sala
ambayo haifikirii ndugu wengine. Mungu hatupatii daima vitu ambavyo tunamwomba,
bali anatupatia daima vitu ambavyo tunahitaji. Ikiwa mara nyingi hatupokei vitu
ambavyo tunamwomba ni kwa sababu hatuombi ipasavyo. Labda tunashindwa kuwa na
tabia na nia kamili zilizodaiwa na Yesu wakati aliwafundisha wafuasi wake
kusali... Mfano wa mama mjane uwe utuimarishe kuanza tena kusali kwa njia
kamili.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário