Kutafakari kuhusu Lk 17, 5-10
“Mwenye
haki ataishi kwa imani yake.” Tafakari yetu inalenga imani kama zawadi
muhimu sana iliyo njia maalum ya kuishi nayo inatoa maana kwa maisha. Imani ni
msaada kubwa katika majibu yetu kwa upendo wa Mungu. Hii ni zawadi inayochochea
karama ya Mungu iliyo ndani yetu kupitia Roho Mtakatifu. Wakati wanafunzi wa
Yesu walipomwomba wakisema, “Ongeza Imani yetu”, walionyesha tabia ya
unyenyekevu wakitambua udhaifu wao mbele ya changamoto za kazi. Kwa dua hii walitaka
kumaanisha kwamba walikuwako tayari kwa kila kitu kwa ajili ya Yesu, lakini
walihitaji msaada wake.
Kwa maneno mengine, ilikuwa tangazo la imani
kuutambua uwezo wa Yesu kwa ajili ya imani yao haba. Jibu la Yesu linadhihirisha
kwamba wanafunzi hawakuwa na imani jinsi walivyodhani walicho nacho. Jibu la
Yesu linawasaidia kufahamu umuhimu wa Imani na lengo lake la kweli. Kulingana
na Yesu imani inauhusu utumishi na kuthibitisha utambulisho wa wafuasi na
mwalimu wao. Yesu hakujibu moja kwa moja, bali alipendelea kuonyesha kwamba imani
sio jambo lolote. Haitoshi kusema “Nasadiki” ama “nakusadiki”. Ni kama
ilivyotokea katika hadithi fulani:
“Kuna mtu ambaye alikuwa anatembea kwenye njia
nyembamba bila kuwa makini kutazama alipokuwa anaelekea. Ghafla aliteleza
kandokando ya mtelemko wa ghafla. Alishikilia tawi la mti kwenye mtelemko.
Akigundua kuwa hawezi kushikilia kwa muda mrefu aliomba msaada. Aliita: “Kama
kuna mtu huko juu anisaidie?” Sauti ilimjibu: “Nipo hapa.” Aliuliza: “Wewe ni
nani?” Sauti ilimjibu: “Ni mimi Bwana Yesu Kristo.” Mtu huyo alisema: “Nisaidie
Bwana.” Bwana Yesu: “Unaniamini?” Mtu huyo alijibu: “Nakuamini kabisa.” Bwana
Yesu akasema: “Achia tawi la mti.” Mtu huyo alishangaa: “Nini?” Bwana Yesu:
“Achia tawi la mti.” Baada ya kimya cha muda mrefu mtu huyo alisema: “Hakuna
mtu mwingine huko juu?”
Bila shaka tabia ya mtu huyo siyo imani kwa
sababu inakosa muhimu sana iliyo kuacha kitu ambacho kinaonekana kuwa usalama
na kujiruhusu kuongozwa na Yule anayejua analofanya. Imani ya kweli inadai
tabia ya kujisalimisha, kulingana na hadithi nyingine: “Siku moja ajali
ilitokea katika nyumba ya ghorofa kubwa nayo nyumba hii ilianza kuwaka moto.
Watu wote walipaswa kutoka nje. Familia moja ilipata kutoka, lakini mtoto mdogo
wake alibaki nyuma. Wazazi hawakuweza kurudi tena ili wachukue mtoto kwa sababu
moto ilikuwa kali sana. Mtoto alikaribia dirisha moja katika sehemu ya juu ya
nyumba akilia sana. Yeye hakuweza kumwona yeyote nje ya nyumba kwa sababu ya
moshi nyingi. Lakini, kutoka nje baba ya mtoto huyo aliyepata kumwona mtoto,
alimwambia, ‘mwanangu, ukatupe chini kutoka huko kwa maana mimi nitakuchukua
mikononi mwangu.’ Ingawa mtoto hakupata kumwona babaye, akaisikiliza sauti yake
na kuamua kujitupa. Kisha, mara babaye alipata kumchukua mwanae mikononi mwake,
akimwokoa.”
Katika hadithi hii, kwanza kabisa kuna uhusiano wa
kifamilia, yaani, baba na mtoto. Baba anatumia nafasi ya kusema kitu, yaani, ‘mwanangu,
utupe chini kutoka huko kwa maana mimi nitakuchukua mikononi mwangu.’ Anasema hayo kwa sababu anajua mwanae na
tena anajua kwamba huyo mwanae anahitaji msaada wake. Anaposema hayo,
anahakikisha uwepo na utunzaji wake. Basi, hali ya imani inafanana na hivi. Hii
ni zawadi iliyotoka kwa Mungu na inatenda ndani yetu ili lile ambalo
lisilowezekana libadilishwe kuwa linalowezekana. Imani hii hata ndogo inaweza
kushinda vikwazo vikubwa. Tukumbuke yale ambayo Yesu aliwaambia wanafunzi wake
waliochanganyikiwa, yaani, “Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya
haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii”.
Imani hii tulipokea katika ubatizo kama
mbegu ambayo inahitaji kuchipua, kukua na kuboresha. Tunahitaji kuiimarisha
zawadi hii kwa sababu ni maonyesho ya utambulisho wetu na, kupitia ushuhuda wa
imani halisi tunaweza kuwaimarisha wengine katika safari yao. Mt. Yohana
Calabria asema: imani yetu iwe halisi na ya kweli; haiwezekani kuwa na tofauti kati
ya imani tunayoamini na tabia tunayoishi.” Si lazima imani kubwa; kweli imani
yetu inapaswa kuwa hai na ufanisi. Kuhusu hayo, mtume Yakobo asema, “mwonyeshe
imani yenu bila matendo nami nitaionyesha imani yangu kwa matendo yangu. Imani
bila matendo imekufa.” Katika sehemu
nyingi za injili tunakuta mifano ya Imani hai na ufanisi, yaani, wakati Yesu
alipokutana na mtu aliye na aina hii ya imani na mtu huyo alimwomba ili amponye,
Yesu asema, “imani yako imekuokoa”.
Kulingana na hadithi, ingawa mtoto hakupata kumwona babaye, lakini akaisikiliza sauti yake na kuamua
kujitupa, vivyo hivyo sisi tunaalikwa kuchukua uamuzi wa kujisalimisha. Hii
ndiyo imani. Mungu ambaye tunasadiki yu kama vile yule baba ambaye alipata
kumchukua mwanae mikononi mwake, akimwokoa.” Tumeipewa imani na kupitia
zawadi hii tunaweza kujibu kwa mwaliko wa Mungu. Bila shaka jibu ambalo yeye anatarajia
ni kwamba tuweze kujikabidhi mikononi mwake kama ilivyotokea kwa Ibrahimu na
kwa wenye haki wengine wa Biblia. Mfano, kulingana na uzoefu wa Ibrahimu,
haitoshi kusema “nakuamini”; ni lazima kutii, kuruhusu kuongozwa na Mungu hadi
palipompendeza. Kuhusu uzoefu huu wa Ibrahimu, waraka wa Waebrania unatuletea
ushuhuda mzuri sana, yaani, “Kwa njia ya imani Ibrahimu alitii alipoitwa ahamie
nchi ambayo angepewa kuwa mali yake. Alihama bila kujua anakokwenda” (Waeb
11:8).
Kumwachia Mungu ni kuwa na imani ya Ibrahimu.
Ni imani ya kumwacha Mungu aitwe Mungu
aliye Baba na Mtoaji. “Matatizo yote yapaswa kufikiriwa na kusomeka kwa
maelewano na ubaba wake” (Mt. Yohane Calabria). Huyo, yaani, Mt. Yohane
Calabria, anafahamiwa kama Mtakatifu wa Riziki kwa maana ya tabia ya imani ya
kweli na kujisalimisha kwake katika Riziki ya Mungu. Kulingana naye, Riziki ya
Mungu ni kama Mama ambaye anatenda mambo yote kwa wema wetu. Tunapaswa kujiona
kubebwa mikononi mwake wa mama.” Kuhusu hayo, anaendelea kwa kusema, “Kama sisi
tuko mikononi mwa Mungu, tuko mikononi pazuri.” Je, tabia yetu ni kama ile ya
mtoto mdogo ambaye anaruhusu kuongozwa kwa sababu ana uhakika kuamba mama au
baba yake anajua lile analofanya? Yeyote ambaye anaamini anaweza kujisalimisha
mikononi mwa Mungu Baba kama Mt. Calabria alivyo.
Ikiwa
tunajiita Wakristo, ni kwa sababu tunajua kwamba sisi ni washiriki wa imani ya
kanisa lilipo kwa karne nyingi. Wakati tunapotumia imani yetu kama jibu kwa mwaliko
wa Mungu, hatuyategemei mawazo yetu peke yake, bali tunaitegemea imani ya watu
wote wa Mungu, yaani, imani ambayo inawahusu Ibrahimu, Musa, manabii wa
Israeli, mitume na wanafunzi wengine wengi wa Yesu Kristo, Mt. Yohana Calabria
na kadhalika. Imani yangu ya kibinafsi ni urithi wa imani ya jumuiya ya kanisa.
Kutokuwepo kwangu katika jumuiya ama kikundi kunasababisha shida kwangu na kwa
kikundi. Basi imani inadhihirisha utambulisho wetu; hii ni njia yetu wenyewe ya
kuishi na kutumikia. Imani
yetu inauhusu utumishi ambao tunaweza kufanya. Kwa kutumikia kwa kweli tunataka
kumwomba Bwana Yesu kwa unyenyekevu “Bwana Mkubwa, ingawa imani yetu ni haba
ukatufanye wanafunzi wako waaminifu!”
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário