Kutafakari kuhusu Lk 18, 1-8
Uwepo wa Yesu ni
mahali maalum pa mkutano kati ya Mungu na binadamu. Mara nyingi yeye hukutana
na Baba yake kwa mazungumzo ya ndani akiwapa watu mfano wa sala ya kweli na yule
ambaye anajua kila kitu na ndiye makini daima kwa maombi ya wanao. Tunapoimba:
Baba, sikia wanao, sikia sauti zao, sikia dunia nzima”, tunataka kumaanisha
kwamba Mungu ni Baba na kutarajia tuweze kumhutubia sala zetu kwa imani kama wenye
uhakika kwamba tumepokea sana. Basi, Yesu aliwafundisha wafuasi wake wafanye
kama Yeye alivyo, yaani, kusali daima bila kukata tamaa kamwe. Ili wafuasi wake
wafahamu vizuri mahitaji haya alisimulia mfano mmoja kulingana na ufundishaji
wake wa ajabu.
Hakimu mmoja
wakati wa muda mrefu alikataa kumsikiliza ombi la mama mjane dhidi ya adui yake
na hatimaye alimsikiliza kwa sababu ya kusisitiza kwake. Mfano wa mama huyo ni lazima
kuwa rejeo kwa maombi yetu. Mama huyo alikuwa na hakika kwamba yule hakimu
akawa na uwezo wa kumtetea kwa hivyo alikuwa na uvumilivu kuhusu ombi lake. Mama
huyo anatujulisha kipimo ili kufikia mafanikio katika mpango wowote hasa kuhusu
uzoefu wa sala.
Kuna hamu falani
ndani yetu ambayo inatuvutia kwa Mungu. Kupitia hamu hii tunatambua kwamba
maana ya maisha ni kukutana naye, kulishwa na uhai wake na kuongozwa naye kwa
sababu bila yeye hatuwezi kufanya chochote. Ikiwa Mungu anachelewa kuhusu dua
zetu ni kwa sababu wakati wake ni tofauti na wetu. Kulingana na kifungu cha
nabii Isaya (55, 6.8), tunaalikwa kumtafuta Mungu daima kwa sababu anapatikana
naye yupo karibu. Changamoto kwetu ni kusali na kusubiri kulingana na wakati na
njia za Mungu.
Basi, kusali ni uzoefu
wa ndani; ni kumhisi Mungu karibu sana nasi, kwa kuongea kwa masikio yetu kila
siku na siku zote. Kusali ni mazungumzo na Mungu, kwa kutumia muda wa ubora
kuliko wa kiasi. Tunaposali kwa kweli tunahisi kwamba vitu vingi huanza
kubadilisha ndani yetu na tunapata mtazamo tofauti kuhusu hali kandokando yetu.
Ingawa hali hii inaendelea kwa ugumu wake na changamoto zake, mtazamo na tabia
yetu itakuwa tofauti kwa sababu tunaimarishwa sio na udhaifu wetu bali na nguvu
ya yule ambaye ana mazoea ya kubadilisha hali mbaya ili iwe hali mzuri na hali
ya mauti ili iwe ya uzima.
Pamoja na shauri
kuhusu mahitaji ya kusali daima Yesu alitupa sala yake mwenyewe, sala iliye na
yaliyomo ya mazungumzo yake na Baba, yaani Baba Yetu. Sala hii tafsiri hisia za
wana ambao wanatambua ukuu na ukaribu wa Baba yao na kwa hivyo wana uhusiano wa
ndani naye. Kwao sala si sharti, bali mahitaji ambayo yanatokana na ndani yao.
Kwao sala ni uhusiano wa upendo kwa sababu wanapata kujiona wapendwa. Wanapenda
kufanya kama mwalimu wao ambaye alisali kutokana na moyo kwa moyo.
Labda tunahitaji
tabia hii kamili kwa sababu tunamwomba Baba mmoja aliye mwema na kujua mahitaji
yetu. Ana macho na masikio yenye hisia kuhusu kile kinachotokea nasi na yupo
tayari daima ya kututendea mema kwa sababu pia hiyo ni njia yake. Kwa upande
wetu tuwe na imani zaidi na kujisalimisha kabisa mikononi mwake kama Mwanao wa
pekee. Katika sala aliyotufundisha tunasali si kwa mahitaji yetu tu, bali kwa
mahitaji ya wote. Hivyo, ikiwa tunasema “Baba Yetu” ni kwa
sababu tunasadiki kwamba sisi ni ndugu wa wengine wengi.
Mungu hawabagui watu wala kusahau yeyote wa wana wake. Hapendezwi na sala
ambayo haifikirii ndugu wengine. Mungu hatupatii daima vitu ambavyo tunamwomba,
bali anatupatia daima vitu ambavyo tunahitaji. Ikiwa mara nyingi hatupokei vitu
ambavyo tunamwomba ni kwa sababu hatuombi ipasavyo. Labda tunashindwa kuwa na
tabia na nia kamili zilizodaiwa na Yesu wakati aliwafundisha wafuasi wake
kusali... Mfano wa mama mjane uwe utuimarishe kuanza tena kusali kwa njia
kamili.
Fr Ndega