Kutafakari kuhusu Lk 15, 1-3.11-32
Sura ya kumi na tano ya toleo la Luka ni maarufu miongoni mwa mifano ya
Yesu. Inaitwa sura ya Mifano ya huruma. Tuna mifano mitatu (Kondoo aliyepotea:
4-7; Sarafu iliyopotea: 8-10; Mwana mpotevu: 11-32). Katika nafasi hii
tunaalikwa kutafakari kuhusu mfano mmoja peke yake, yaani mwana mpotevu ama
baba mwenye huruma. Mfano huu ndio maonyesho ya tabia ya huruma ya Mungu kwa
ajili ya wenye dhambi kwa sababu ya upendo wake mkubwa.
Kwa kufahamu nia ya Yesu wakati aliposimulia mfano huu tunahitaji
kutafakari kwanza kuhusu mazingira ambayo Yesu aliishi. Yeye
ndiye sura ya huruma ya Mungu naye alifunua huruma hii siyo kwa maneno tu bali pia
kwa matendo. Kwa hivyo, kulingana na andiko hili watozaushuru na wenye dhambi
walimkaribia Yesu ili kumsikiliza. Wasingalifanya hili ikiwa wasingekuwa na
uhakika wa kukaribishwa vizuri na Yesu. kwa upande mwingine, tuko na kikundi
cha pili, kilichojumuisha Mafarisayo na Waandishi wa sheria ambao walichagua
kimanung’uniko, kukosoa na kupinga ishara za Yesu kwa ajili ya kikundi cha
kwanza.
Chote vikundi viwili ingawa
vilikuwa na uzoefu tofauti ya Mungu na tabia tofauti kumhusu Yeye, watu hawa ni
wanawe na hao ndio wapendwa naye. Hakuna hata kimoja kijuacho sura ya kweli ya
Mungu kwa sababu watu wa kikundi kimoja fulani walijiona kama wenye haki na
kuwalaumu watu wa kikundi kingine ambao walijikiri kama wenye dhambi, yaani
bila nafasi ya kuondolewa dhambi yao. Katika mkutano na Yesu walivutiwa na
huruma na, kwa hivyo, nafasi mpya kwa maisha yao. Hayo ndiyo mazingira ambayo
Yesu alitumia ili kuumba hadithi hii ya Baba mwenye huruma. Tunataka kujifunza
mengi kutoka kwa Baba huyo.
Ingawa
yako matukio mengi katika Agano la Kale ambayo yanaonyesha njia maalum ya Mungu
ya kutenda, ni “katika Yesu Kristo kwamba huruma ya Mungu imepata kuwa hai na
yenye kuonekana, na hata ilifikia kilele chake katika Yeye... Yesu ni uso wa
huruma ya Baba. Kila kitu ndani yake
kinaongelea huruma. Hakuna chochote kwake kinachopungukiwa na huruma (Baba Mt
Francisco).”
Katika mfano wa mwana mpotevu,
ingawa tuko na vitendo vya kijana mdogo na kijana mkubwa, macho yetu yamlenga
baba wa vijana hawa wawili ndiye aliye mhusika mkuu wakati wote. Muhimu ya
tukio hili ni uhusiano wake wa upendo kwa ajili ya vijana wake ambao wote ni
wapotevu kwa njia tofauti. Kulingana na Yesu, Mungu ni kama baba mmoja aliye na
watoto tofauti na kushiriki nao zawadi zake kwa njia sawa. Yeye anawapenda wote
na kutaka wajione wakiwa katika familia, kushiriki katika furaha yake ya baba.
Katika familia hii anautoa utunzaji na ulinzi ili wawe na maana nzuri ya kukaa katika
ushirika naye daima. Wakati yeyote anapoamua kujitenga naye na kuenda mbali kutoka
kwake sio kwa sababu anashindwa kupendwa, bali ni kwa sababu anajiona mwenye
uhuru. Baba huyo anaheshimu uhuru wa watoto wake na kuwahakikishia makaribisho
wakati wanapoamua kurudi nyumbani.
Basi, mara nyingi uzoefu wetu ni
kama vile hali hii. Tunajiona mbali na Mungu wakati sisi hutenda dhidi yake,
yaani tunapomkosea. Yeye anajihisi ameachwa na kusalitiwa, lakini hashindwi kutupenda.
Kama yule baba, Mungu anashughulika sana na maisha yetu kwa kutupatia ulinzi na
utunzaji wake. Kwa hivyo tunahisi majuto na kuvutiwa ili kuishi tena uzoefu wa
ushirika ambao tumepoteza. Ingawa mara nyingi hatuishi kama wanawe, kwa sababu
ya dhambi zetu, Mungu anabaki mwaminifu daima kama Baba mwema. Huruma yake ina
nguvu kuliko makosa yetu.
Katika mfano huu yuko pia mwana
mkubwa ambaye hajihisi mwana, kwa sababu anajiona kama mfanyakazi, wala
hajihisi ndugu, kwa sababu anamkataa ndugu yake mdogo. Tabia ya huyo mwana mkubwa
inaizuia furaha na sikukuu kwa kikamilifu. Kumrudia Mungu ni maana ya furaha
kubwa kwake. Lakini furaha yake haiwezekani kuwa kabisa ikiwa hatushiriki
katika hisia zake kuhusu wengine. Yeye anataka kwamba tutende kama yeye alivyo.
Kwa hivyo Yesu alisema, “Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo.” Upatanisho na
wengine ni kipimo ili uhusiano wetu na Mungu uwe kweli. Hii ni njia ya kweli ya
toba iliyo mwendo wa muda mrefu
na huanza mioyoni mwetu. Turuhusu kuguswa na huruma ya Mungu ili
tuweze kuwa vyombo vya huruma hii kwa wale wanaohitaji msamaha wetu.
Nenhum comentário:
Postar um comentário