sexta-feira, 2 de novembro de 2018

MPENDENI MUNGU NA JIRANI KAMA NILIVYOWAPENDA NINYI


Kutafakari kutoka Kum 6:2-6; Waeb 7:23-28; Marko 12,28-34


      Kulingana na Maandiko Matakatifu Mungu ana uhusiano maalum na Watu wa Israeli. Alianzisha agano na watu hawa, akiwapa baadhi ya mwongozo ili watembee salama na kuwa maisha mengi. Katika mazingira haya tunaweza kukiri kuzaliwa kwa Amri kumi. Kuishi Amri kulikuwa muhimu kwa Waisraeli ambao wanafikiria Neno la Mungu kuwa ni Sheria na Sheria kuwa ni Neno la Mungu. Wanaposema kwamba “Sheria ya Bwana ni kamili, faraja ya roho”, wanaongea kuhusu Neno la Mungu. Kuna uhusiano wa ndani kati ya Sheria na Neno, kwa sababu Amri za Sheria zinaonyesha utunzaji wa upendo wa Mungu ambaye anapoongea anaongoza njia kamili ya ukombozi na uzima. Kutii kwa Amri ni chanzo cha baraka maana huongoza kwa uzima, wakati kutotii kwa Amri kunaongoza kwa mauti.

      Basi, chanzo cha Amri ndio upendo wa Mungu. Yeye ni upendo na kupenda kwa hiari. Anafikia wote kwa uhusiano huu. Yeye anatarajia tuweze kumpenda pia kwa sababu aliweka moyoni mwa kila mtu uwezo huu tangu mwanzo mwa uumbaji. Upendo ni sheria yake ya kipekee. Sheria hii hailazimishi bali ndiyo zawadi na kuonyesha njia ya uhuru wa kweli. Hii ndiyo maana ya hotuba ya Musa kwa Watu wa Israeli katika somo la kwanza. Kupitia Musa, Mungu anaongea na Watu kutoka moyo kwa moyo, sababu Mungu anataka kuandika sheria yake mioyoni mwa wote. Yeyote anaishi sheria ya Mungu kwa kweli ikiwa anaweza kupenda. Kumpenda Mungu kunamaanisha kuishi kulingana na mapenzi yake. Katika somo la pili Kristo ni kuhani mkubwa kuliko makuhani wa Agano la Kale kwa maana alijitoa nafsi yake kwa upendo kwa ajili ya wenye dhambi wote, akitufundisha njia halisi ya kumpenda Mungu kwa kweli.

     Kando ya sheria kuu Wayahudi waliweka sheria nyingi ambazo polepole zilibadilisha makini kutoka muhimu sana. Jibu la Yesu ni kugundua tena jambo hili yaani, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote... Mpende jirani yako kama nafsi yako”. Kumpenda Mungu ni kwanza wa Amri zote, lakini Yesu aliiunganisha na upendo kwa jirani, akionyesha kwamba haiwezekani kumpenda Mungu kwa kweli bila kumpenda jirani. Kutokana na Amri ya kumpenda Mungu inaububujika upendo kwa jirani kama matokeo. Chanzo ni Mungu daima, kwa sababu alitupenda kwanza na kwa hiari. Ndio kutokana na njia ya Mungu ya kutupenda kwamba tunapaswa kuwapenda wengine. Hii ni changamoto kwa tamaduni yote hasa mahali ambapo uaminifu kwa familia na desturi kwa kawaida umekuwa kama amri ya kwanza.


     Hivyo, baadaye Yesu alitaka kufanya rahisi zaidi akijionyesha kama mfano. Kwa hivyo alibadilisha Amri mbili hizi ziwe moja peke yake, yaani tupendane kama yeye alivyotupenda. Kama Mungu alivyotupenda katika Kristo tunaalikwa kupendana kutoka kwa Kristo. Mtu ambaye anapenda kulingana na njia hii alifahamu umuhimu wa sheria naye sio mbali na Ufalme wa Mungu. Kwa kweli, mtu ambaye anamfuata Yesu hafuati sheria au mafundisho bali anamfuata Mtu aliyetupenda mpaka upeo. Tunajua kwamba katika jamii kuna sheria nyingi. Watu wenye hekima na upevu wanatii sheria lakini hawakuwa watumwa kwa sababu wanafahamu kwamba muhimu siyo sheria yenyewe bali ndiyo roho inayosukuma sheria na tabia mtu anayochukua mbele ya sheria. Lengo la sheria yote ni kuwafanya watu waishi vizuri, yaani kwa maelewano. Sheria inakuwa bila maana ikiwa lengo lake ni kuonea ama kusaidia marupurupu kwa baadhi ya watu kwa kubagua wengine. Hali hii ni pendekezo sio kwa jamii tu, bali pia kwa Kanisa, kwa jumuiya na kwa familia zetu. Changamoto kwetu leo ni kuweka juhudi ili sheria yote iwe chombo cha ndugu kama maonyesho ya upendo kwa Mungu na kwa jirani.    

Fr Ndega

Nenhum comentário: