Kutafakari kutoka 1 Waf 17,
10-16; Waeb 9, 24-28; Mk 12: 38-44
Kifungu cha
waraka wa Waebrania kinaongea kwamba Kristo alikatisha dhambi zake kwa
kujisalimisha mwenyewe msalabani. Hili ndilo fumbo ambalo ametuokoa nasi tunaguswa
kwa njia mpya daima katika kila Ekaristi ambayo tunasherehekea. Hili silo tukio
la kihistoria tu bali nafasi ya kushiriki katika maisha ya Kristo mwenyewe ambayo
inatuimarisha kuendelea kazi yake kwa kuyatoa maisha yetu kama yeye alivyo.
Sehemu ya kwanza
ya Injili inajulisha upinzani wa Yesu dhidi ya njia ya waalimu wa sheria ya
kuishi. Hao wanapenda sana kujiinua na kupendezwa. Wanasali kwa muda mrefu
lakini bila kusudi kamili. Wanajihisi bora kuliko wengine na kudhulumu wajane. Yesu
ana wasiwasi kuhusu njia hii ya unafiki kwa sababu inalipinga pendekezo lake
kwa wanafunzi wake.
Watu walijua
kwamba kuna tofauti hasa mfarakano kati ya mafundisho ya Yesu na ya waalimu wa
sheria. Yesu aliwafundisha watu kwa mamlaka aliyopokea kutoka kwa Baba. Kuhusu
mamlaka ya walimu wa sheria, yakosa ukweli. Baada ya uhuru kutoka utumwani
Babeli walimu walikuwa viongozi muhimu kwa ajili ya Wayahudi kwa sababu
waliandika Vitabu Vitano via mwanzo wa biblia vinavyojulikana kama Vitabu vya
Musa, yaani Toraa na hao peke yao waliweza kuhukumu na kujulisha sentensi
kulingana na sheria. Hao waliwasisitiza Wayahudi kuzingatia agano kwa kuzishika
sheria za Mungu kama msingi wa taifa lao jipya. Lakini ingawa waliwafundisha
watu waishi sheria, tabia yao ilikuwa mbali sana na mafundisho yao.
Utumiaji mbaya wa
mamlaka ni majaribu daima katika maisha ya walio na jukumu la kuwaongoza watu
katika jumuiya zetu za Kikristu na pia katika jamii. Lakini sio hao tu ambao
wanaguswa na majaribu haya. Hata sisi pia tuko na mwelekeo huu. Majaribu ya
kawaida ni yaani kujiona bora kuliko wengine, kutaka kutumikiwa badala ya
kutumikia, kuwanyonya wengine na kadhalika. Yeyote ambaye anataka kuwaongoza
wengine anapaswa kuiga mfano wa Yesu aliyekuwa na mawazo tofauti na kujua njia kamili
ya kushinda majaribio yote. Hatuwezi kumpendeza Mungu wala kuwa wenye furaha
ikiwa hatuishi majukumu yetu kama utumishi.
Lakini katika
sehemu ya pili ya injili hii tuko na njia kamili ya kuwa mwanafunzi wa Yesu, yaani
mfano wa mama mmoja mjane maskini aliyeenda hekaluni kutoa sadaka yake. Yesu
alikuwa ameketi karibu na sanduku la hazina pamoja na wanafunzi wake. Alitazama
jinsi watu walivyoweka pesa sandukuni. Yeye aliweza kuona moyo na kusudi kwa
kila mmoja alipotoa sadaka. Alipotazama mjane akiweka fedha sandukuni yeye
alitambua kwamba mama huyo alitoa zaidi kuliko wengine kwa sababu sadaka zao
zilikuwa ziada ya matajiri bila kusudi kamili kwa moyo. Sadaka ya mjane
ilimpendeza Mungu kwa sababu alitoa kila alicho nacho cha kuishi, yaani alitoa maisha
yake kama zawadi, kama sadaka.
Mama mjane
maskini hakumjua Yesu, lakini alimpendeza kwa sababu alitenda kulingana na
pendekezo la binadamu mpya. Mtu anakuta
maana ya kweli ya maisha wakati anapoweza kutenda kama Mungu katika ukarimu
wake, yaani zaidi kuliko kutoa kitu, mtu anaweza kujitoa mwenyewe kama sadaka
yote kwa kuonyesha kwamba maisha yake ya kila siku yanamtegemea Mungu. Tuko na
tabia ambayo inadhihirisha ukuu wa moyo wa mtu fulani.
Tunaalikwa kwa
macho kwa ishara halisi ndogo zinazotoka kwa watu unyenyekevu tunaowakutana kwa
kawaida na kujifunza kutoka kwao tabia kamili mbele ya Mungu. Yeye hupendezwa
sio na wingi wa vitu ambavyo tunatoa bali na ukarimu wa moyo wetu. Thamani ya sadaka
yetu hupimwa kulingana na ukarimu wetu. Ukuu wa mtu hautokana na kipimo cha
zawadi ambayo anatoa bali na uzuri wa ishara yake na upendo wake. Kweli, ndizo
ishara ndogo zinazofanya tofauti. Msaada mkubwa ambao ninaweza kumpa wengine
ndimi ninayealikwa nilivyo. Zaidi ya hilo ndio unafiki ambao unanizuia kuwa na
uhusiano mwema na wengine. Tunaweza kushinda hali mbaya hii kwa msaada wa watu
wanyenyekevu ambao wanajenga undugu kandokando yetu na kuwa maonyesho ya
ukarimu wa Mungu.
Fr Nega
Nenhum comentário:
Postar um comentário