Kutafakari kuhusu Dan 12:
1-3; Waeb 10: 11-14; Mk 13: 24-32
Tuanze tafakari hii tukijiuliza swali moja: “Je, Wakristo wanapaswa kuwa na
tabia gani wakati wa mazingira magumu na mbele ya kosa la uhakika lililo tabia
ya wakati huu? Sisi tu watu wa tumaini kwa sababu maisha ya mtu anayemfuata Yesu
yamejaa maana. Basi, ujumbe wa liturgia hii ni msukumo kwetu tulioalikwa kutoa
maana za tumaini letu kupitia imani yetu katika Kristo. Uhakika wa ukaribu wake
ndio nguvu yetu. Tukikumbuka kwamba leo ndiyo Siku ya Kidunia ya Maskini,
tunataka kuwa manabii wa tumaini dhidi ya utabiri wa kukata tamaa ambao
unatuzuia kupanga wakati mwema kwa maskini wa jamii yetu. Jambo hili lina
uhusiano gani nasi? Baba Mtakatifu Francisco anatuambia kwamba: “Manabii wako upande
wa maskini kwa sababu wanajua ndipo katika upande huu kwamba Mungu ako”.
Somo la kwanza linalotokana na kitabu cha nabii Danieli ni ufunuo kuhusu
hukumu na ufufuko. Hilo ndilo mojawapo kati ya maandiko ya Agano la Kale yanayoongelea
imani katika ufufuko (angalia pia 2 Mac 7, 9). Watu wa Israeli walitumwa na Wagiriki
na kuteseka sana. Wengi miongoni mwao waliacha kumwamini Mungu, lakini wengine
ambao waliendelea kumwamini walihitaji ujumbe wa tumaini na kutia moyo ili
kuendelea safari yao kwa uvumilivu. Mungu ndipo daima kati ya watu wake na
kuwasaidia mbele ya mazingira magumu ambayo wanakabiliana. Tendo lake kupitia malaika
yake linahakikishia ukombozi na tena uzima kwa wale ambao walikufa kwa sababu
ya kumwamini Bwana na kutenda mema hadi upeo.
Kulingana na somo la pili toleo la Kristo lilishinda dhabihu zote za
makuhani wa Agano la Kale. Dhabihu zao zilitendeka mara nyingi wala hazikuwa na
nguvu ya kuondoa dhambi za watu, yaani zilikosa ufanisi. Kwa upande wa Kristo, hali
ni tofauti. Toleo lake lilitendeka mara moja tu nayo ilitosha kwa kuwatakasa
watu wengi katika nyakati zote kwa sababu alijitolea mwenyewe. Katika kila misa
takatifu tunasherehekea fumbo la toleo hii. Ndiye Kristo mwenyewe ambaye
anatuhusisha katika mwendo huu kwa ajili ya wokovu wetu na wa wengine.
Mwanzoni mwa sura
ya kumi na tatu ya injili hii ya Marko Yesu aliongea kuhusu uharibifu wa
Yerusalemu. Ufunuo huu uliwaimarisha baadhi ya wanafunzi wake wamwulize kuhusu
ishara gani na siku gani na saa gani ya uharibifu huu. Kisha, Yesu alitumia
nafasi hii ili kuongelea mambo mengi yatakayotokea na haja ya ushuhuda ili kukutana
naye tena na kushiriki katika furaha yake. Aliporudi tena atawakusanya wateule
wake kutoka dunia nzima. Alitabiri kwamba “nguvu za mbingu zitatikiswa”
akimaanisha kwamba miungu ya uongo, yaani jua, mwezi, itapoteza mwanga wao.
Hata wale waliojiona watu wa kimungu (nyota za angani) ambao wanawatesesha watu
wa mataifa hasa walio maskini, hao (miungo ya uongo) wataanguka na mtazamo wa
wote utamwelekezea Mwana wa Mtu akija amejaa nguvu na utukufu kama mshindi. Hakuna
mtu anayejua wakati kamili ambao mambo yote yatatokea ila Baba peke yake. Kwa hivyo
ni lazima kumwamini yeye.
Ingawa uharibifu
wa mji wa Yerusalemu ulitokea katika mwaka wa 70 B.K., nia ya Yesu haikuwa
kuwajulisha kuhusu tukio hili, bali kuhusu matokeo ya tukio hili maishani mwa
wafuasi wake. Ni lazima kutafakari injili hii kulingana na mazingira ambayo
jumuiya ya Marko ilikuwa inaishi, yaani wanafunzi wa Yesu waliishi kipindi cha
machafuko na kujaribiwa kukata tamaa kuhusu utambulisho wao wa wafuasi kwa maana
ya majaribio na mateso mengi. Hao walijiuliza: “hayo yatokeayo yamaanisha
nini?”. Mbele ya hali hii mwinjilisti aliwakumbusha mafundisho ya Yesu yasemayo
kwamba baada ya mambo yote wanafunzi watakuwa washindi kama mwalimu kwa sababu
ya uvumilivu wao mpaka upeo. Bwana wa Mtu ndiye msingi na lengo la historia. Kwa
hivyo historia haiendi kwa mwisho bali kwa lengo kamili: Yesu Kristo mwenyewe.
Andiko hili
linatuambia kwamba Kristo ni mshindi na atafanya kuwa washindi wale ambao
wanamfuata. Ujio wake mara ya pili utaanzisha historia mpya na ubinadamu mpya. Yeye
anataka kushiriki na wanafunzi wote watakaobaki wamesimama kupitia imani na
ushuhuda kwa uaminifu. Maneno yake yatuambia kuwa mazingira magumu ni sehemu ya
safari ya wale ambao wanamfuata katika nyakati zote, lakini tena yatuhakikishia
kwamba ikiwa tunabaki tumesimama kwa uvumilivu mpaka upeo tutaokolewa. Kuhusu
wakati huu, hakuna mtu anayejua. Hii ni sehemu ya mpango wa
hekima na wema wa Baba. Kwa hivyo ni lazima kumwamini yeye ambaye anaiongoza
historia ya kibinadamu kwa lengo kamili. Tuko mikononi mwake; kwa hivyo tuko
katika mikono mizuri”. Ujumbe huu unatoa tumaini kwa maisha yetu. Sisi tulioalikwa
kuendelea utume wa Mwana wake Yesu, tunapaswa kuwa macho kwa ishara za uwepo
wake ambazo zimetokea kati yetu. Ili hali mpya ikatokee maishani mwetu, miungu mingi
ya uongo yapaswa kuanguka na kupoteza thamani yao. Kwa maneno mengine,
tunapaswa kuacha picha za uongo za Mungu, mawazo na tabia ambayo inayapinga
mafundisho ya injili. Tuishi wito wetu kwa shauku na furaha kwa sababu kuna
tumaini kwa wakati ujao wetu.
Fr Ndega