Kutafakari kuhusu Mt 18: 21-35
Akiwaita wanafunzi ili wamfuate Yesu alikuwa
akianzisha jumuiya. Akijua moyo wa kibinadamu na kukiri kwamba kuna hali ambazo
zinaweza kuijenga ama kuharibu jumuiya, yeye alionyesha njia kamili ili
mahusiano kati ya wanafunzi wake yawe ya kweli na kuzaa matunda mazuri. Njia ambayo
Yesu alionyesha ilikuwa njia ya mazungumzo, ya msamaha na ya upatanisho. Kama hatua
ya kwanza ya marekebisho ya kidugu nilipaswa kumwita ndugu aliyekosa kwa mazungumzo
kati yake na mimi peke yetu. Ikiwa hatua hii haipati mafanikio inawezekana kuuomba
msaada wa jumuiya. Kwa Yesu, ndugu anayekosa anaendelea kuwa ni ndugu naye
anastahili kufikiriwa kama ndugu. Hali ya maisha ya ndugu fulani anayehudhuria
pamoja nasi katika maisha ya kijumuiya ni jukumu letu. Tunaalikwa kutumia
juhudi zote, pamoja na Yesu, ili ndugu huyo asipotee bali aokolewe.
Tukiendelea kwa ujumbe huu wa upatanisho,
tunataka kutafakari kwa kina juu ya thamani ya msamaha kwa maisha ya jumuiya
zetu. Petro alimjia Yesu na kumwuliza, akisema, Bwana, ndugu yangu anikose mara
ngapi nami nimsamehe? Yesu alimjibu, akisema “saba mara sabini.” Yesu alitumia
swali la Petro ili kuongea kuhusu mahitaji ya kusameheana bila kipimo wala
mpaka kama sharti kwa kuingia katika Ufalme na pia kama njia kamili ya uhusiano
mwema kati ya watu. Kama kawaida, Yesu anajulisha tabia ya Baba yake kama kipimo.
Katika mfano huu, bwana wa mtumishi mbaya sana ni kama Mungu Baba. Yeye
alimwonea huruma, akimsamehe lile deni na kumwacha aende. Bila shaka mtumishi
huyo hastahili, lakini huruma ya bwana huyo ni kubwa zaidi kuliko hali mbaya ya
mtumishi huyo wala haimtegemei. Na kama hitimisho, Yesu anawaalika wasikilizaji
wake wawe na huruma kama Baba Yake alivyo, yaani, wasamehe kwa mioyo yao yote.
Mungu anasamehe bila kipimo kwa sababu hii ni
tabia yake. Akitenda hivyo, anatarajia wanadamu wawe na uhusiano mwema naye na
tena kati yao. Kwa Yesu, rejeo la kutenda ni Baba daima kwa sababu angalia kwa
kina lile ambalo linatokea ndani ya binadamu. Yeyote ambaye anaweza kuona ndani
tena anaweza kuona vizuri. Ingawa binadamu ana udhaifu mwingi na kutenda mbaya,
mtazamo wa Mungu kwake ndio wa upendo, yaani ndio mtazamo ambao anatoa nafasi
ya kutenda tofauti na kuwa mwema. Kwa sababu ya mtazamo huu binadamu sio
mpotevu bali ndiye mtu wa tumaini. Kulingana na Mtakatifu Yohane Calabria, “tunapaswa
kuyachukia makosa bali kuwapenda waliokosa kwa maana ndio ndugu zetu.” Hata wakati
wanapotukosea mara nyingi, kulingana na swali la Petro, tunaalikwa kuwapenda.
Basi, andiko hili ni mwaliko wa kuifuata tabia ya Baba anayesamehe daima
bila kufikiria aina ama kiasi cha dhambi zetu. Msamaha ni maana ya sikukuu na
furaha kwa sababu unasababisha uzoefu wa ukombozi kwa mtu ambaye anamkosea
mwingine na kutubu, na pia kwa yule anapomsamehe. Mtu ambaye anasamehe ni
chombo cha huruma ya Mungu na mtoto wake wa kweli, kwa sababu, kulingana na
Baba Mt. Francisco, “Yesu
anasisitiza kwamba huruma si tendo la Baba peke yake, bali inakuwa kipimo cha
kuthibitisha nani kweli ni watoto wake. Kwa kifupi, tumeitwa kuonyesha huruma
kwa sababu huruma imeonyeshwa kwetu kwanza.”
Lakini tuwe macho kwa sababu hatuwezi kufikiri kwamba maneno ya Yesu ya “saba
mara sabini” ni mwaliko ili tuendeleze kukosa na kutarajia kwamba wengine wapatikane
kutusamehe daima. Huu ndio mwaliko ili tuache njia ya dhambi, kwa sababu matokeo
ya uzoefu wa kweli wa huruma ya Mungu, hasa kupitia Sakramenti ya Kitubio ndiyo
mabadiliko ya maisha. Kupitia sakramenti hii, anasema tena Baba Mt. Francisco, “Mungu
anakuja
kutusaidia katika udhaifu wetu... tukiguswa na huruma yake, tunaweza pia kuwa
na huruma kwa wengine”. Tunaalikwa kuishi kama tulioguswa na huruma, yaani
tuliosamehewa kwanza. Msamehe ni zawadi ya Mungu. Wakati tunaposamehe
tunaonekana na Mungu na kupata kufikia matarajio yake ya Baba Mwema.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário