Tafakari kutoka Is 22, 19-23;
Rom 11,33-36; Mt 16, 13-20
Kama Wakristo,
tumejengwa juu ya msingi wa mitume, yaani imani yetu ilianza kwa kukiri kwa
imani ya mitume. Ingawa sisi tu tofauti, utambulisho wetu ni kuwa wamoja. Ndio ubatizo
wetu umetuunganisha na Kristo kwa ajili ya kujenga mwili mmoja na kuishi kwa
uaminifu Agano ambalo Mungu alifanya nasi tulio watu wake.
Katika somo la
kwanza, kwa sababu ya kosa la uaminifu wa Shebna, Mungu atamchagua Eliakimu na
kumpa mamlaka ya kuwatawala watu wake. Kulingana na mpango wa Mungu kwa watu
wake, kiongozi huyo atakuwa kama baba
aliye na ufunguo wa mti kwa ajili ya kuwatunza watu na kuzaa hali ya utulivu na
kuamini. Kupitia watumishi wema na wanyenyekevu Mungu anaendelea kuwaongoza na
kuwatunza watu wake. Kulingana na somo la pili, Mungu anafanya mema yale
anayofanya kwa sababu anatenda kwa hekima na upendo. Kwa upande wetu, ni lazima
kufungua moyo kwa kupokea msukumo wake ili tutende kama yeye alivyo.
Yesu alikuwa
anatembea pamoja na wanafunzi wake na walipofika eneo la Kaisarea Filipi yeye aliwauliza
maswali kuhusu utambulisho wake kulingana na mtazamo wa watu. Hii ilikuwa nafasi
nzuri ya kuwafundisha vizuri kuhusu utambulisho wake wa Masiha wa Mungu. Jibu
la kwanza linadhihirisha kwamba watu hawakuwa na wazo kamili kuhusu Yesu na walifikiri
kwamba ilitosha kumlinganisha na manabii wa zamani. Kwa maneno mengine
walikuwako mbali na matarajio ya Yesu. “Kumwita Yesu nabii ni nusu tu ya ukweli
wote. Manabii huandaa njia kwa ajili ya mtu mwingine. Lakini Yesu pekee ndiye
ambaye njia yake iliandaliwa na manabii wengine wote.” Ingawa kwa watu mawazo
kuhusu Yesu hayakuwa wazi, kwa mitume yapaswa kuwa tofauti, maana kwa Yesu si
muhimu yale ambayo watu wanafikiri, bali kukiri kwa wafuasi wake.
Kwa hivyo, Yeye
aliwauliza akisema, “Na ninyi, Je, mnasema mimi ni nani?” Jibu la Petro alidhihirisha
yale ambayo wanafunzi wengine kumi na mmoja walijua pia: Yesu ni Masiya wa
Mungu. Lakini hawawezi kutangaza habari hii kwa sababu ya kutokuwa na maana
kamili. Mawazo yao kuhusu Masiya yalifuata matarajio ya Wayahudi wengine,
yaani, Masiya wa kisiasa atakayetumia nguvu zake za kimungu ili kuwakomboa
Wayahudi toka ukoloni wa Warumi. Bila shaka kwamba Yesu aliyakanusha mawazo
hayo akionyesha njia tofauti ya kutimiza ujumbe wake wa Masiya. Masihi ambayo
Yesu alichagua ni ile ya mtumishi wa Bwana aliye makini kwa sauti ya Mungu na
kufanya mapenzi yake kwa njia ya mateso, kufa na kufufuka.
Ingawa jibu la
Petro lilikosa maana kamili, Yesu aliutambua ufunguzi wa Petro kwa msukumo wa
Mungu. Msukumo huu ulimsaidia Yesu ili kumpa Petro nafasi ya uongozi kati ya
mitume. “Yeye ni sawa na wenzake lakini ana tofauti fulani. Kukutana na Kristo
kumbadilisha Petro sana mpaka anapewa kazi hii maalumu. Hasemi kwamba yeye ni
tofauti na wenzake. Tena atamkana Yesu (Mt 26:33) lakini anatubu (Mt 26:69-75)
na anarudishwa tena kwa kazi yake hiyo (Yoh 21:1-19).” Hivyo, Petro alipokea
kazi hii sio kwa sababu alistahili, bali kwa imani yake thabiti na imara ndiyo
mwamba. Imani ya Petro na ya mitume wengine ni maonyesho ya uamuzi wa kuyatoa
maisha yao kwa ajili ya Kristo. Imani hii ndiyo msingi wa imani yetu kama
Wakristo.
Jukumu la Petro
na mitume wengine limerithiwa na Baba Mtakatifu Francisco na maaskofu wote. Kama
Yesu alitambua mkono wa Baba na tendo la Roho Mtakatifu katika Petro, tena
anatambua tendo hili katika waandamizi wao wote na kuandamana nao ili kazi yao
ionyeshe utunzaji na upendo wa Mungu kwa watu wake. Ingawa wana jukumu la
kuliongoza kundi la Yesu, wanashiriki pamoja nasi katika kundi moja. Imani yao
thabiti na imara inathibitisha imani yetu na kutuhakikishia umoja yetu katika
Kristo. Kwa upande wetu ni lazima usikivu na ushirika na wachungaji wetu kwa
ajili ya manufaa ya Kanisa zima. Utume wa upendo na wa unyenyekevu wa
wachungaji pamoja na utiifu wa wana kondoo uwe daima maonyesho ya Kanisa la
kweli la Kristo.
Fr Ndega
Fr Ndega