Kutafakari kuhusu Lk
10, 25-37
Katika usomaji wake, mtaalamu fulani
wa Biblia alifanya uhusiano wa ajabu kati ya mikutano ya maskini na Yesu na ile
mikutano yake na matajiri. Kulingana na mtaalamu huyo, Maskini na wasio na
nguvu walipokutana na Yesu wanalenga msaada kutatua shida za kimwili kwa sababu
walijihisi kudharauliwa na kutengwa na wengine; hao wanataka kushiriki kamili
katika maisha ya kijamii pamoja na wenzao. Kuhusu mikutano ya Yesu na tajiri na
wenye nguvu, hali ni tofauti kabisa kwa sababu hao wanamiliki mali ya kutosha
duniani, wanajiona watawala wa dunia na kutaka kutawala katika uzima wa milele
pia. Mbele ya hayo Yesu anapendekeza kujinyima kama ilivyotokea kwa kijana
tajiri aliyependelea kuenda zake kwa huzuni kuliko kukubali pendekezo la Yesu
la kujinyima alicho nacho kwa ajili ya maskini – Mt 19: 16-22.
Katika injili ya siku ya leo
mwanasheria alimwendea Yesu na alimwuliza maswali mawili, yaani, la kwanza
“nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”; na la pili, “Jirani yangu ni
nani?” kuhusu swali la kwanza Yesu alimsaidia kugundua tena umuhimu wa sheria,
yaani, “kumpenda Mungu na kumpenda jirani”. Amri ya Kumpenda Mungu tunapata
katika kitabu cha Kumbukumbu la Sheria (6:5) na ya Kumpenda jirani kunapatikana
katika kitabu cha Walawi (19:18). Ikiwa Yesu alimwambia mwanasheria kwamba
yatosha kutenda hivyo ili apate uzima wa milele ni kwa sababu “Torati yaonyesha
njia ya uzima wa milele ikiwa mtu
anampenda Mungu na jirani yake.” Katika Agano la Kale Mungu alianzisha Agano na
Watu wa Israeli akiwafanya wana wake. Kama ishara halisi ya Agano hili tuko na
Amri kumi ambazo zinalenga ushusiano mwema na Mungu na jirani. Lakini,
kulingana na mawazo yao ya kiyahudi, jirani siyo yule ambaye anaishi karibu nao
bali yule ambaye ni karibu katika uhusiano wa damu. Basi, wageni hawawezi kuwa
jirani kwao. Hivi uelewa huu uliwazuia kuwa na uhusiano mwema hasa na Wasamaria
waliofahamiwa kama maadui wao.
Kupitia swali la pili, yaani “Jirani
yangu ni nani?” mwanasheria alitarajia Yesu akubaliane na mawazo haya ya kivuo.
Lakini Yesu alisimulia mfano wa Msamaria Mwema. Kulingana na mfano huu tuko na
kuhani, Mlawi moja, Msamaria na yule aliyekuwa ameshambuliwa na wanyang’anyi.
Wawili wa mwanzo, yaani kuhani na Mlawi, ni ishara ya wale ambao wanapaswa
kuitii sheria, na kulingana na sheria hii, hawawezi kugusa ama kuguswa na “kitu
kichafu”. Walitumia njia nyingine kwa sababu kuwa karibu na mtu yule aliye na
haja ya msaada kungewazuia kumsifu na kumtumikia Mungu kamili. Kwa kweli wawili
hawa wanapaswa kufahamu kwamba “ni
jambo baya kutofanya mazuri kwa kutumia jina la Mungu au la dini”. Msamaria peke yake aliyefahamiwa
kama adui wa yule aliyeanguka, alimwonea huruma, akasimama na kumsaidia. Kwa
sabau ya sheria ya utakaso wawili wa kwanza walidhararau yule aliye mwenzao hata
wakitotii sheria ya ujirani. Kupitia tabia yake ya huruma, “Msamaria alionyesha
ujirani mwema” kwa sabau hakuhitaji kuitii sheria ya utakaso. “Msamaria mwema
hakujifikiria mwenyewe, alimfikiria mwingine.” Kupitia mfano huu Yesu
anaonyesha kuwa swali la msingi sio “ni nani jirani yangu,” bali ninawezaje
kuwa jirani kwa mwenzangu?” Yesu anasahihisha mtazamo kuhusu jirani na
kuonyesha kuwa upendo wa kweli kwa Mungu unatokea pamoja na kushiriki katika maisha
ya wale anaowapenda.
Kwa Yesu, upendo
wa kweli unaonyeshwa kupitia ishara
za upole na huruma. Yesu mwenyewe
ni Msamaria Mwema kwa namna ya kipekee ambaye alichukua hali yetu na kuponya
majeraha yetu ya dhambi. Yeye anajitambulisha na wale ambao “wameanguka
kando ya njia za maisha”. Je, tunaweza
kutambua uwepo wake Kristo katika watu ambao kwa kawaida tunakutana na hao ambao wanaudai msaada wetu? Kumwabudu Mungu kwa kweli
kunatokea kupitia uhusiano mwema na ufanisi na wengine. Kusherehekea Ekaristi
ni alama ya undugu ikiwa undugu uko miongoni mwetu. Vinginevyo sio Mwili na Damu
ya Kristo tunayosherehekea. Haiwezekani kufanya uhusiano wa kweli na Mungu
wakati tunapowasahau wenzetu katika mahitaji yao. Hatuwezi kuishi kwa kutofautiana
kuhusu hali ya wengine kama ilivyotokea kwa Kaini, yaani “Je mimi ni
mlinzi wa ndugu yangu?” (Mwanzo 4:9). Hali hii ni kutofautiana iliyo
njia ya kukanusha utambulisho wetu wa wakristo. Sihitaji kujua ni nani
jirani yangu ili nimpende na kumsaidia. Kumpenda jirani ni kumsaidia kushinda
matokeo ya ukatili na udhalimu maishani mwake. Siku ya leo, kwa upande wetu
kama wakristo, jirani ni yule ambaye tunamgundua kama aliye na haja na kuamua
kuandamana naye kumhakikishia maisha kwa heshima hata wakati mwendo huu unapodai
kutumia muda wetu na rasilimali zetu. Ekaristi hii itusaidie kuwa “jirani
mwema”.
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah
Nenhum comentário:
Postar um comentário