Wakati wa safari ya
kwenda Yerusalemu, Yesu alitumia nafasi ya kuwafundisha wanafunzi wake hasa
kuhusu masharti ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwanza kabisa haitoshi kuwa
wanafunzi wake ili kupata wokovu. Hivyo, aliwapendekezea mlango mwembamba kama
changamoto. Ikiwa Yesu anajulisha mlango mwembamba ni kwa sababu pia kuna
mlango mpana.
Wakati Mt. Yohane Paulo wa II alipoongea na
vijana katika mwaka wa 1993, alitofautisha vizuri njia hizi mbili, akisema:
“kataeni barabara rahisi: barabara ya anasa, uhalifu, kudharau mazuri, na
kukwepa wajibu. Ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya na uasherati visiwe na
nafasi katika maisha yenu. Pitieni mlango mwembamba. Chagua barabara ielekeayo
kwenye uzima wa milele na furaha pamoja na Mungu.” Katika kifungu kingine Yesu
alisema kwamba mlango mwembamba ni njia ambayo inaongoza kwenye uzima na
wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo. “Huu ni mlango wa uvumilivu, busara,
kujitoa, ukarimu, wema, shukrani na kazi”. Kuhusu mlango mpana, hii ni njia
rahisi inayoongoza kwenye maangamizi na waendao njia hiyo ni wengi. Basi, ili
wanafunzi wa Yesu waweze kupata mafanikio katika safari yao wapaswa kupitia
mlango mwembamba.
Katika mazingira
yetu mlango mwembamba ni ishara ya juhudi yetu ya kushinda mwelekeo mbaya wa
maisha yetu na kuwatendea watu mema. Katika mwendo huu ndio sisi wa kwanza wa
kupata mafanikio ama bahati mbaya, kwa sababu lile tunalofanya kwa ajili ya
wengine linasababisha hali nzuri ama mbaya kwetu pia. Hadithi fulani
inatusaidia kuelewa vizuri hali hii. “Siku moja mwandishi wa habari alimhoji
mwenye shamba ambaye ameshinda mara ya tano mashindano kuhusu mahindi mazuri
zaidi katika eneo hilo. Mwandishi alimwuliza swali akisema, “unapataje kuzaa
mahindi bora kuliko wengine?” Mwenye shamba alijibu, mwendo huu ni rahisi sana;
nina mazoea ya kushiriki mbegu zangu nzuri na majirani wangu.” Mwandishi
aliendelea kwa swali akisema, “Kwa nini unashiriki mbegu zako nzuri na majirani
wako ikiwa hao wanashindana pia katika mashindano haya pamoja?” “kwa sababu ni
upepo ambao unasambaza poleni ya mahindi na tena ni upepo ambao unaweka poleni
mashambani na unafanya mbegu zikue. Ikiwa majirani wangu watakuwa na mahindi
mabaya, upepo utasambaza poleni mbaya shambani kwangu nayo mahindi yangu
yatakua mbaya. Basi ili mahindi yangu yawe mazuri ninapaswa kuwasaidia majirani
wangu wote ili wawe na mbegu nzuri.”
Basi, lile zuri ambalo
tunatarajia kwa maisha yetu tunapaswa kusaidia kwa ajili ya wengine. Katika
mwendo huu hatuwezi kuitafuta furaha kwa njia ya ubinafsi. Ikiwa tunataka kuwa
wenye furaha, tunapaswa kuisaidia hali hii nzuri kwa wale wanaoishi karibu nasi
nao wako na shida sawasawa nasi. Tunapaswa kushinda mwelekeo wa jamii wa
kufikiria wengine kama washindani nasi. Wengine sio washindani, bali ni ndugu.
Kujaribu kupata upendeleo tukiwavuruga wengine ni udhalimu na kutuacha mbali
sana na pendekezo la Yesu. Ikiwa tuko mbali na pendekezo la Yesu, matokeo yatakuwa
mbali sana na yale tuliyotarajia kwa maisha yetu. Tunaweza kuongea vizuri sana
kuhusu Yesu ili kuonyesha kwamba tunamjua Yeye na Biblia pia. Tunaweza hata
kufikiri kwamba kuongea bora kuliko wengine kunatuhakikishia faida ili tupokee
baadhi ya tuzo kutoka kwa Mungu. Lakini, kulingana na andiko hili, maneno
hayatoshi kuingia katika ufalme wa Mungu. Wokovu si astahili yetu, lakini hii
ni zawadi ya ukarimu wa Mungu.
Je, inawezekanaje
tuseme kwamba tunamjua Yesu naye aseme kwamba hatujui sisi?” Hii ni kwa sababu
katika biblia kitenzi kujua kinamaanisha uhusiano wa ndani, uzoefu wa kina
ambao ni muhimu sana katika safari yetu ya wanafunzi wa Yesu. Ikiwa yeye
anasema kwamba hatujui sisi ni kwa sababu sisi hatumjui yeye. Katika mwendo huu
hakuna makubaliano kati yetu na pendekezo lake, hakuna utambulisho. Hatuwezi
kuwa wanafunzi wa Yeu kupitia maneno peke yake. Ushuhuda wa maisha unathamini
zaidi kuliko maneno. Tukijifikiria bora kuliko wengine hatuuhakikishii wokovu.
Kila kitu tunachofanya kinasababisha matokeo makubwa kwetu na katika hali iliyo
kandokando yetu. Kwa maneno mengine, kufikia mafanikio ama bahati mbaya kwa
maisha yetu kunatutegemea sisi wenyewe; huu ni uamuzi wetu. Kwa upande wa Mungu
tunaumbwa ili kushiriki katika maisha yake, yaani ili kuokokewa. Neema ya Mungu
ituongoze ili tuweze kufanya mapenzi yake na kupata uhai.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário