Kutafakari kutoka Is 53,
10-11; Waeb 4, 14-16; Mk 10, 35-45
Maisha ya yule
ambaye anamtumikia Bwana yana maana kubwa. Yote ambayo anafanya yalenga kufunua
mapenzi ya Yule ambaye alimwalika kuwa mtumishi wake. Kwa sababu ya
kujisalimisha kwake kwa upendo watu wengi wataokolewa (andiko la kwanza). Huyo
ndiye Kuhani mkuu ambaye tunahitaji, yaani mtu kama sisi, ambaye anachukua hali
yetu ya udhaifu - ila dhambi – ili kutuonyesha njia kamili ya kushinda hali hii
na majaribu yote yanayotuzuia kuonja neema ya Mungu na kuishi kulingana na
mapenzi yake (andiko la pili).
Katika injili, ndugu
wawili, yaani Yakobo na Yohane walimwendea Yesu na kumwomba kitu. Walitaka
kuketi mmoja mkono wake wa kuume na mwingine mkono wake wa kushoto katika
utukufu wake. Ombi hili linadhihirisha kwamba wanafunzi wake walishindwa kufahamu
utambulisho na utume wa Mwalimu wao. Ni muhimu kukumbuka kwamba hali hii ilitokea
baada ya ufunuo wa Yesu kuhusu mambo yatakayomtokea yeye katika Yerusalemu, yaani
mateso, kifo na kisha kufufuka. Katika kipindi kingine, wakati Yesu alipoongea
kuhusu matukio muhimu hayo, wanafunzi walijadiliana kuhusu ni nani ndiye mkuu
kati yao, wakionyesha kwamba mawazo na matarajio yao yalikuwapo bado mbali sana
na pendekezo la Mwalimu Yesu. Hivyo, yeye alipaswa kuwa na uvumilivu sana mbele
ya ugumu wa wale aliowachagua kama washirika. Hata hivyo, aliweka halisi daima
masharti ya kumfuata.
Kwa wanafunzi wa
Yesu, sehemu muhimu ya tangazo lake ndio utukufu kwa sababu walitafuta kuwa
wahusika wakuu. Wengine kumi walikasirika kwa sababu walitafuta mambo sawa na
wote wawili nao hawakukubali kubaki nyuma. Kwa maneno mengine, wote walikuwa
wazi katika kutafuta kwao, yaani walitafuta msimamo, umaarufu na upendeleo,
lakini walichagua Mtu sio kamili wa kumfuata ili kutimiza lengo hili kwa sababu
mantiki ya Yesu ni tofauti. Mbele ya hali hii ya mgawanyiko kwa sababu ya
ghasia ya rejeo la maisha, Yesu aliwaalika tena kama mara ya kwanza na kusahihisha
matarajio yao potovu: “anaondosha fikra zao walizojijengea wenyewe.” Njia ya
maisha yake ina mwelekeo tofauti na wa dunia. “Katika ufalme wa Yesu, wale
walio viongozi hawapo ili kuwanyonya wengine au kutegemea heshima na utumishi
kutoka kwa watu wao, bali viongozi ndiyo huwa watumishi wa watu.”
Basi, mantiki
ya Yesu ndiyo mantiki ya utumishi unaokuta katika maisha yake rejeo lake:
“Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maisha yake kuwa fidia
ya watu wengi.” Hali hii ambayo ilishirikisha maisha yake wakati wote inakuwa ni
rejeo kwa maisha ya wale ambao wanatamani kumfuata kwa uaminifu: “Yeyote
anayetaka kuwa mkuu kati yenu sharti awe mtumishi wa wote; na anayetaka kuwa wa
kwanza kati yenu sharti awe mtumishi wenu.” Hakuna njia nyingine ili mtu aweze
kupata maana kamili ya maisha. Yeyote anayeamua kumfuata Yesu hawezi kuendelea kufikiri
na kutenda kama mtu wa zamani.
“Yesu anakumbana
na upinzani mkali huko Yerusalemu na kumfanya apoteze maisha yake. Lakini jambo
hilo Yesu anaona ni huduma ya upendo kwa watu wake (Mk 10:45).” Ndiyo kupitia
imani katika Kristo na msukumo kutoka Neno lake kwamba yeyote anaweza kukabiliana
na taabu, kukataa na mateso bila kukata tamaa. Hivyo, kuishi au kulima wito wa
mtumishi kwa uaminifu sio rahisi kwa sababu kuna vitu vingi dhidi ya uamuzi
wetu, yaani mawazo kandokando yetu kwa kawaida ni tofauti na pendekezo la
injili; upinzani kutoka kwa wengine hata familia; mwelekeo wa kibinadamu ambao
ndani yetu unatuimarisha kutafuta kutumikiwa badala ya kutumikia; kutokuwa na
imani yenye nguvu na kosa la uvumilivu katika matendo mazuri, n.k.
Vitu hivi vyote
ni sehemu ya safari yetu pamoja na hamu yetu ya kumfuata Yesu kwa uaminifu.
Lakini hatusahau kwamba hatutembei peke yetu. Yule aliyekubali “kujitoa kama
zawadi kwa watu wote” ndiye mfano wetu na kutuhakikishia msaada wake ili tudumu
katika utumishi kwa ajili ya wengine hata mbele ya kutokuelewana na taabu. Ikiwa
ndio upendo ambao unatoa maana ya maisha, hakuna njia nyingine ya kuishi kwa
maana ila kupitia utumishi kwa unyenyekevu na kwa ukarimu kwa wengine ulio
maonyesho halisi ya upendo na utambulisho na Yule ambaye “alikufa na kufufuka
kwa ajili yetu, inatoa mwenyewe kwa uhuru wetu na kuuimarisha kutafuta,
kugundua na kutangaza maana hii ya kweli na kamili.”
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário