Kutafakari kutoka Yer 31,1-7; Wab 5,1-6; Mk 10, 46-52
Kifungu cha
Yeremia ni mwaliko wa furaha kwa sababu Bwana anapanga kutenda mambo ya ajabu
katika maisha ya watu wake: hakika, kazi hii imekwisha anza. Yeye ndiye Baba
amejaa upendo kwa ajili ya watu wake, hasa kwa ajili ya wadogo na wasio na
nguvu miongoni mwetu. Yeye huvutia kwake kila anayeishi ili kufanya uzoefu wa
wokovu wake kwa sababu “upole wake unafikia kila kiumbe.” Anatuambia leo: “Wewe
ambaye husikiliza, wewe unayeteseka, wewe unayependa nawe unayesali, wewe ni
mwanangu mpendwa, binti yangu mpendwa!” Mbele ya Mungu ambaye anatenda hivyo kwa
ajili yetu, tabia yetu lazima kuwa ya amini kabisa, tukiacha nafasi kwa tendo la
neema yake katika maisha yetu, yaani, kuruhusu Mungu awe Mungu ndani yetu.
Kifungu cha waraka kwa Wayahudi kinaleta
mfano wa kuhani ambaye amechaguliwa miongoni mwa watu na kufanya wakfu kwa manufaa
yao. Yeye amevaa udhaifu na kwa hivyo anaweza kuhisi huruma kamili kwa ajili ya
wanaokosa. Ukweli huu inamzungumzia Yesu Kristo, Kuhani wa kweli, ambaye “anakusanya
katika nafsi yake udhaifu wa mtu na nguvu ya kufanya upya wa Aliye juu.” Yeye
hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu” bali ndiye Baba aliyemtukuza.
Sisi pia tangu ubatizo wetu katika Kristo, tuko na heshima ya kikuhani iliyo
huduma ya wokovu. Kwanza ya yote hii ni zawadi ya Mungu nasi mbele ya hali hii tunapaswa
kujibu kwa uaminifu na furaha. Tunasaidiwa na neema yake na jumuiya ya imani ili
tuweze kuishi wito wetu kama zawadi kwa ajili ya wengine.
Kifungu cha injili anaongelea kuponywa
kwa Bartimayo na, basi, ufunuo wa Yesu kama mwanga ambaye anatupa mtazamo mpya.
Muujiza huu ulitokea wakati Yesu alikuwa anaondoka mji wa Yeriko, yaani, katika
pembezoni. Yeriko ni mmoja miongoni mwa miji ya zamani ulimwenguni. Mji huu ni
eneo la baadhi ya matukio makuu ya biblia; hata katika muda wa Musa iliongelewa
kuhusu mji huu. Tukumbuke “kuzingirwa na kuchukuliwa kwa Yeriko” na Waisraeli
katika wakati wa Yoshua (Yoshua 6, 1-27). Tukumbuke pia Zakayo; mabadiliko ya
maisha yake yalitokea katika Yeriko. Mji huu ni karibu na mto Yordano na Yesu
alipita mahali huko mara nyingi. Andiko la siku ya leo linaongea kuhusu mkutano
wa Yesu na kipofu Bartimayo, aliyeketi kando ya barabara ya mji. Hakika alikwisha
amesikia kuhusu Yesu na alitaka sana nafasi ya kukutana naye. Lakini hakujua
kwamba Yesu pia alitaka kukutana naye ili kumwongozea njia mpya ya kuishi.
Kisha, nafasi imefika! Shauku ya kipofu ilikuwa kubwa sana hata hakuna mtu aweze kumnyamazisha.
Kilio cha kipofu ni kilio cha kila
binadamu ambaye anajua udhaifu wake mwenyewe na kuhusu mahitaji ya huruma ya
Mungu. Kipofu ni ishara ya kivuo dhahiri cha ndugu zetu wengi walio waathirika
wa udhalimu na kosa la usawa wa kijamii. Ni nafasi ya kutambua kwamba watu
wengi wanaanguka au wameachwa barabarani ama katika mahusiano yetu. Wanapaza
sauti kwa huruma na kwa nafasi kwa sababu wanaamini kwamba wale ambao wanajiona
kuwa wafuasi wa Yesu wanaweza kusikiliza sauti yao na kuwatendea mema. Yesu
alisikia si kilio cha kipofu tu, bali pia kilio cha wale ambao walimwambia
kipofu “anyamaze”!, wakionyesha kutojali. Yesu analaumu kutojali kwa sababu
kunaharibu undugu na kukana utambulisho wa mwanafunzi wa kweli.
Hakika jibu la Yesu linaonyesha
mchanganyiko wa huruma na hasira, kwa sababu alikuwa akishughulika kwa upofu wa
aina mbili tofauti, yaani, upofu wa Bartimayo na upofu wa umati wa watu ambao
walikuwa wakimfuata Yesu bila ushirika na hisia zake. Je, ni nani ana upofu
zaidi, yule aliye kipofu asili au wale ambao hawapati kuona walio na mahitaji
kandokando yao? Hata hivyo kuna tumaini, kwa sababu miongoni mwa wale ambao walimwambia
kipofu “nyamaze!” walikuwapo wengine ambao walimwambia “jipe moyo, anakuita!
Yeye hajakusahau wala hawaachi wale ambao wanamwamini”. Sauti hizi ni za watu
ambao wanachukua ujumbe wa kinabii na kupata kuwahamasisha waliokata tamaa. Ni
ishara pia ya walio vyombo vya Mungu katika maisha ya yeyote anayetaka kugundua
wito wake ili aweze kumjibu Mungu kulingana na matarajio yake.
Yesu ambaye
tunamfuata ni mwenye hisia sana. Ana macho na masikio yalio makini sana kwa
hali halisi ya watu. Anatualika kuwa na hisia sawa naye. Mara nyingi sisi tu
kama kipofu huyo, yaani, tunahitaji na kutarajia mkutano wa mabadiliko ya
maisha ili kuona vizuri kile kinachotokea kandokando yetu na kumfuata Yesu
ambaye analeta maana mpya kwa maisha yetu. Tena mara nyingi sisi ni kama
wengine karibu na Yesu, lakini mbali sana na ndugu, waliofungwa kwa hali iliyo kandokando
yetu na hata tunafikiri kwamba tuna mamlaka ya kuwaambia wengine: “mnyamaze”. Hapo
tuko na kosa kubwa. Tunapaswa kuwa macho kwa baadhi ya uzoefu wa sala ambao
unatufungua kwa Mungu lakini unatufunga kwa wengine. Ikiwa imani yetu haituongozi
kukutana na wengine wala haitufanyi wenye huruma, mbele ya mateso na mahitaji
yao, imani ni kipofu, ni udanganyifu na kuhitaji kupona. Mungu atupatie neema
ya imani ya kweli na halisi.
Fr Ndega