Kutafakari kuhusu Is 52, 7-10; Hb 1, 1-6; Yoh 1, 1-18
Sisi tunaishi wakati wa furaha na shukrani,
yaani wakati wa Krisimasi. Kila kitu kinaonekana kuwa na rangi zaidi, mwanga zaidi
na maana zaidi. Haya ndiyo matokeo ya uwepo wa Mungu miongoni mwetu; yeye aliyachukua
mazingira yetu na kutualika kujifunza kutoka kwake ili tuweze kuishi vizuri.
Tumshukuru Mungu kwa kuendelea kutupa sisi nafasi ya kuwa watu wapya. Ujumbe wa kuzaliwa kwa Yesu ni ujumbe
wa furaha kubwa kwa wote, kwa sababu Mwokozi alizaliwa
kwa wote. Tufurahi kwa sababu Mungu aliamua kuyajenga makao yake kati yetu
na kutuletea wokovu. Wokovu ni kazi ya Mungu, lakini unatendeka duniani kwa ushiriki wa binadamu. Tuchukue Mariamu na Yusufu kama mifano. Hivyo, katika udogo wa tukio hilo na unyenyekevu
wa watu waliohusika, tunaweza kutambua ukuu wa Mungu wetu. Hali halisi hii inathibitisha methali ya Kiafrika inayosema, “Watu wanyenyekevu, wakifanya vitu
rahisi katika mahali padogo wanaweza kubadilisha ulimwengu.” Mabadiliko makubwa ambayo jamii yetu inahitaji yanapaswa kutokea ndani ya binadamu. Jamii
mpya itatokea wakati kila mtu
atambue haja ya kujibadilisha
mwenyewe kuliko kujaribu kubadilisha wengine.
Kulingana na somo la kwanza, baada ya uzoefu
wa utumwa Watu wa Israeli wanaishi hali mpya na kugundua tena wito wao kama
watu wa Mungu. Wito huu sio kutumia kisasi dhidi ya maadui yao, bali kutangaza
habari njema ndiyo habari ya amani. Habari hii ni ujumbe wa faraja unaotoka kwa
Mungu na kuwaongoza watu kuchukua ahadi ya kujenga uhusiano mpya na Mungu na
miongoni mwao pia. Huu ndio ujumbe wa furaha ambao unapaswa kutangazika kwa wote
kwa sababu wokovu wa Mungu ni kwa wote. Kama watu wapya wa Mungu, sisi ni
warithi wa ujumbe huu yaani tunatangaza wokovu wa Mungu ndiye Yesu Kristo.
Miguu yetu ni ishara ya upatikanaji wetu, hamu yetu kwa ajili ya mpango wa
Mungu. Yote ambayo Mungu amefanya maishani mwetu ni lazima kutangazika. Furaha
iliyo matokeo ya tendo hili haitakuwa kamili maishani mwetu ikiwa hatuwezi kutangaza
kwa wengine. Mwendo huu unaanza katika Mungu mwenyewe aliye Mungu wa neno. Aliviumba
vyote kwa nguvu ya neno lake. Hivyo, somo la pili linashuhudia kwamba Yeye
aliongea zamani kwa mababu yetu, anaongea leo na kuendelea kuongea kwa sababu huyo
Neno alikuwako kwake milele, Neno hili ni Mwanawe Yesu Kristo aliye mpatanishi wa
Agano Jipya.
Neno la Mungu ambaye alikuwako milele ni Mwana
wa Mungu. Huyo ni maana ya vyote vilivyofanyika. Huyo Neno alifanyika mwili
tumboni mwa Bikira Maria akija ulimwenguni amejaa neema na ukweli akifunua sura
ya Mungu kama Baba aliyejaa huruma. Mwana Yesu alitufanya watoto wa Mungu na
kutuangaza kwa mwanga wake ili tuwe mashahidi wa nuru na kweli kama vile Yohana
Mbatizaji. Mambo yote ambayo Mungu anafanya ni mazuri na kamili kwa sababu hii
ni njia yake ya kutenda. “Neno alifanyika mwili na akakaa kwetu”. Katika Yesu, Mungu ni mmoja wetu. Yeye ni
huruma ambaye alijiruhusu kukuta na kuguswa akituletea pendekezo mpya la maisha.
Kwa hivyo, haitoshi kuitambua huruma ya Mungu katika Yesu; ni muhimu pia tujiruhusu kuguswa
na huruma hii na tena kuongozwa na ujumbe
wake wa amani na upendo. Kuzaliwa
kwake Yesu kuliwafanya wanadamu
wote wawe familia moja ya kipekee.
Kweli, Mungu alijidhihirisha kama
jirani, maskini na
aliyekataliwa, akiwaalika wote watambue thamani ya ishara ndogo na miradi midogo. Bila shaka chaguo hili la
Mungu linatuaibisha, kutualika kufikiri
na kutenda kwa njia tofauti.
Mungu Mwenyezi anakubali hali ya mtoto mdogo, kwa
utegemezi kabisa wa utunzaji na
upendo wa binadamu. Ndiyo imani inayotuongoza kutambua mtoto huyu mdogo wa Bethlehemu katika
kila mtoto ambaye sisi hukutana katika safari yetu ya kawaida. Kila mtoto anaomba upendo wetu. Tufikiri
kuhusu watoto ambao hawana uzoefu wa upendo
wa wazazi wao; pia kuhusu watoto wa mitaa/barabara ambao hawana mahali pa kuishi; tena kuhusu watoto wanaotumika kama askari, wakibadilishwa kuwa
vyombo vya ukatili, badala ya kuwa vyombo vya
amani; pia kuhusu watoto ambao ni
waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia, na kuhusu watoto waliolazimishwa kuacha ndoto zao kwa sababu ya hali ya kiuchumi siyo nzuri. Mtoto ndogo ya Bethlehemu
ni mwaliko ili tuweze kusaidia kwa hali tofauti maishani mwa watoto
hawa.
Ingawa tunaishi katika jamii ya ulaji,
inayotuzuia kulenga muhimu katika maisha yetu, tunapaswa kuwa macho. Krismasi ni zaidi ya ulaji. Ni
sikukuu ya ufunuo wa fumbo la upendo wa Mungu unaobadilisha moyo wa binadamu kuwa makao ya thamani za kweli. Mungu anatupenda kwa
hiari na ukarimu, bila astahili kwa upande wetu. Uzoefu huu unatuongoza kutenda vivyo hivyo ili
Krismasi iwe zaidi ya wakati mmoja
tu kwa mwaka. Itakuwa Krismasi daima ikiwa tuweze kujifunza jinsi ya kupenda kwa kweli na kuweka juhudi kwa kujenga jamii ya
undugu na ya haki
kwa wema wa wote.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário