domingo, 26 de junho de 2016

KUJIKANA NA KUJINYIMA KAMA MASHARTI KUMFUATA YESU NA KUPATA UZIMA


Kutafakari kutoka Lk 9, 51-62


     Baada ya Petro kumkiri Yesu kama Kristu, aliye Masiya wa Mungu, Yesu aliwalika Thenashara wote wamfuate katika kujisalimisha kwake ili wapate uzima. Yesu alitambua kwamba walihitaji kujua zaidi kuhusu maana ya umasiha wake na kuyafahamu vizuri mapendekezo yake. Kwa hivyo, alitumia wakati wa safari hadi Yerusalemu kuwafundisha kamili. Mambo mengi yanatokea wakati wa safari hii na hayo yote yalikuwa nafasi ya mafundisho, hasa kuhusu njia kamili ya kutenda mbele ya kukataliwa. Safari kwenda Yerusalemu siyo safari ya kimwili tu bali ni hasa ya kiroho. Mwanzoni mwa injili inasemekana kwamba “wakati siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia...” Basi, hii ni safari kuelekea mbinguni. Mti wa Yerusalemu unafahamiwa kama “Mti wa Mungu” ulio makao ya dini ya kiyahudi. Ingawa Yesu anajua kwamba mti huu ni mahali pa kuwaua manabii, kama ishara ya upinzani kwa mavutio ya Mungu, hata hivyo anataka kwenda huko ili mapenzi ya Mungu ya kuwaokoa watu wake yatimie.

      Kwa kufika mahali huko Yerusalemu ilikuwa lazima kupitia katika eneo la Samaria. Basi, Yesu aliwatumia baadhi ya wanafunzi wamtangulie katika Samaria wamtengenezea mahali pa kupumzika kidogo kwa sababu ya safari ya muda mrefu. Wanafunzi wa Yesu walikuwa na mazoea ya kushughulika kwa mawazo na tabia tofauti na mwalimu wao. Hii ndiyo maana ya kupatwa na hasira sana walipokataliwa wakipita katika Samaria, na kutaka Mungu aliteketeze eneo hilo. Katika safari hii kwenye Yerusalemu Yesu alikuwa akiwaongoza wanafunzi wake katika njia ya upatanisho na amani. Kwa hivyo hakubali pendekezo lao na kuwapendekezea kwenda kijiji kingine, yaani, njia nyingine. Kumfuata Yesu si rahisi sana. Wakati uliopita tulitafakari kuhusu masharti matatu ya kumfuata kwa uaminifu, yaani, “kujikana mwenyewe, kuuchukua msalaba wa kila siku na kumfuata Yesu.” Siku ya leo masharti yanaendelea kuwa matatu, lakini hapo ni kama onyo, shauri. Yesu hataki kuwadanganya wafuasi wake kupitia ahadi pasipo maana. Katika mapendekezo yake, Yesu ni wazi sana. Yeye anauheshimu uhuru wa watu, lakini anayajulisha masharti kwa wale ambao wanataka kumfuata. Vingenevyo hawatapata kumfuata kwa uaminifu.

      Wanafunzi wa Yesu walitaka kutenda kwa njia ya kibinafsi, yaani bila utambuzi na kutafakari (ishara ya kutokwepo kwa Kristo moyoni mwao). Walikuwa waaminifu kwa mwelekeo wa kibinadamu wa kisasi kuliko njia aliyopendezwa Yesu. Mwaliko waa Yesu wa kuenda mahali pengine ni uthibitisho kwamba ni lazima kuheshimu uhuru wa watu. Kumfuata Yesu ni kuchagua kuishi na kutenda tofauti. Mtu hawezi kutazama nyuma ili aongozwe kulingana na hali ya zamani kukanusha utambulisho mpya ulio matokeo ya mkutano na Kristo. Katika mwendo wa kumfuata Yesu mtu anakuwa mtumishi wa ufalme wa Mungu. Katika mwendo huu masharti hayatoki kwa mtu bali yatoka kwa Yesu. Kutazama nyuma kunaweza kuwa hatari kwa safari kwa sababu katika safari hii muhimu sana sio tulichoacha nyuma bali tutakachopokea mbele kwa sababu ya uamuzi wa kumfuata Yesu. Bila kujikana na kujinyima mtu hawezi kumfuata Yesu na kupata uzima. 


Yesu halazimishi uhuru wa wanafunzi wake, lakini anaanzisha masharti ili waweze kumfuata kweli. “Kama wafuasi, wakristo tunaweza kukosa uvumilivu na kuwadharau watu wa makanisa, dini na imani nyingine. Kama Wayahudi na Wasamaria, Wakristo wa Afrika kutoka makabila mbalimbali wanaweza kuwa na chuki kubwa kati yao, kiasi cha kushiriki katika mapigano ya kikabila. Huu siyo mwelekeo wa Yesu.”  Kutokana na mfano wa Kristo, anayeitwa pia mtu asiye na ukatili, njia ya kipekee ya kuushinda ukatili ni kujibu kwa ishara za amani. Yesu anataka kwamba tabia zetu zishinde mwelekeo wa jamii kwenye kisasi, ukatili na ukabila. Ukabila unauharibu undugu, kukanusha utambulisho wetu wa wakristo. Yesu anatualika kufahamu kuwa uovu hauwezi kuondoa uovu, bali ni wema tu unaoweza kufanya hivi. Ekaristi hii takatifu itusaidie kupenda kama Yesu alivyo na, kupitia upendo huu, tuweze kuijenga jamii inayotarajiwa na Mungu.

Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah

SELF RENOUNCE AND DETACHMENT AS CONDITIONS TO FOLLOW JESUS


Reflection from Lk 9, 51-62


      After Peter recognising Jesus as Christ, that is Messiah of God, Jesus invited all twelve ones to follow him in his surrender so that they can get eternal life. Jesus realised that they needed to know more about the meaning of his messianic activity and to understand well his proposals. For that he used the moment of travelling to Jerusalem to teach them rightly. Many things happened during this travel and everything was opportunity for teaching especially about the right way of acting when the person is rejected. The travel to Jerusalem is not a physical travel only, but it is especially spiritual. In the beginning of the gospel it is said that “when the days drew near for Jesus to be received up...” So, this is travel to heaven (event of ascension). The city of Jerusalem is known as “City of God”, the city of Jewish’s religion. Although Jesus knows that this city is place of killing prophets, as sign of resistance to the appeals of God, however he wants to go there in order the will of God should be fulfilled.      

      In order to reach the city of Jerusalem it was necessary to pass through the region of Samaria. So, Jesus sent some disciples whom would advance him in Samaria in order to prepare for him a place to rest because the long travel. The disciples had the habit of thinking and acting differently of their master Jesus. That is the reason of their bad reaction when were prevented to pass through that place and desired God would destroy that region completely. In that travel to Jerusalem Jesus was leading his disciples in the way of reconciliation and peace. For that didn’t agree with their proposal and proposed to go another village, that is, another way. To follow Jesus is not very easy. In the passage before this text, we reflect about three main requirements to follow Jesus faithfully, such as, “To renounce oneself, to carry the daily cross and to follow Jesus.” In the text of today the requirements continue in the same direction, but now they are as advice. Jesus doesn’t want to cheat or deceive the disciples with promises without meaning or foundation. Jesus is very clear in his proposals. He respects the freedom of the people, however presents conditions for the ones who want to follow him. Otherwise they will not get following him with faithfulness.
  
      The disciples wanted to act in individual way, that is, without discernment and reflection (sign of the absence of Christ in their hearts). They were faithful more to the human tendency to vengeance/revenge than to the way which is pleasing to Christ. The invitation of Jesus to go to another place is confirmation that it is necessary to respect the freedom of the people. To follow Jesus is to live and to act in different way. The person cannot look back in order to be guided according to the passed reality, denying the new identity which is result of the meeting with Christ. In the process of following Christ the person becomes servant of the Kingdom of God. In this process, the requirements don’t come from the person, but they come from Jesus. To look back might be dangerous to the journey because in this journey the more important is not what we leave behind but what we’ll receive ahead because the decision of following Jesus. Without self renounce and detachment the person cannot follow Jesus and getting eternal life.
    
      Jesus doesn’t force the freedom on his disciples, but establishes conditions in order they can follow him truly. “As disciples, we Christians can be lacking in patience and despise the people of other Churches, religions and faith. Like the Jews and Samaritans, the Christians of Africa from different tribes can have great hate or resentment among them, amount of participation in tribe fights. But this is not the direction of Jesus.” From the example of Jesus, whom is called also the one who has no violence, the unique way to overcome the violence is to answer with gestures of peace. Jesus wants that our attitudes may overcome the tendency of the society to vengeance, violence and tribalism. Tribalism destroys the brotherhood, denying our identity of Christians. Jesus invites us to understand that evil cannot remove the evil but only kindness can do that. May this Eucharistic celebration help us to love like Jesus and through this love we may build the society which is expected by God.   

Fr Ndega
Review: Sarah

sexta-feira, 24 de junho de 2016

EXPERIENCIA DE DIOS EN EL ROSTRO DEL OTRO: UN MISTERIO QUE ME ULTRAPASA.


Introducción: razón de esta reflexión.

Los invito a reflexionar sobre dos temas interrrelacionados, los cuales son pasión por Dios y por el ser humano, teniendo como iconos a la Samaritana y el Buen Samaritano. Tengo muy en cuenta la necesidad de rever las imágenes de Dios y percibir la riqueza y, al mismo tiempo, la apertura del esquema: paternidad, filiación y fraternidad. Cuando hablo de apertura (esquema citado), tengo presente, una vez m{as que Dios como Padre nos remite a los demás, el encuentro-confronte con los demás, principalmente con los más necesitados, a su vez, me interpela para reconocer el cuidado y la paternidad de Dios (los necesitados tienen dificultades de reconocer la paternidad de Dios cuando son abandonados y olvidados por los que dicen ser sus hermanos). Con esto, quiero decir que la fraternidad bien cultivada, en último análisis, me reporta a la paternidad de Dios.

Quien quiera trabajar este proceso, podrá relacionar Mt. 6, 24-34 con Mt. 25, 31-46. Hay una sintonía muy agudizada entre los dos textos, que no puede ser dejada de lado. Así, se puede hablar de pasión por Dios y pasión por el ser humano como algo inseparable. Quien no tiene pasión por Dios (búsqueda y cultivo de su presencia), jamás desenvolverá pasió por el ser humano (en la óptica de Jesús de Nazareth). De otra manera, quien no tiene pasión por el ser humano, vive la ilusión de quien encuentra a Dios. No se trata de idolatrar al ser humano, como si él fuese un dios, sino reconocerlo como un lugar teológico, esto es, un espacio en el cual Dios se manifiesta. Según lo que Jesús hizo y enseñó, no se hace una verdadera experiencia de Dios sin fraternidad: la condición es: “se se aman… en esto el Padre es glorificado”. Dejémonos tocar por Dios. Supliquemos la ayuda del Espíritu Santo, pidiendo la gracia que sigue:

Gracia a pedir
Que el Espíritu de Dios haga arder en nuestro corazón la llama del verdadero amor, llevándonos a encuentros significativos con las personas, especialmente las más necesitadas, a través de las cuales podamos hacer experiencia del verdadero Dios que nos llama a una total donación por su Reino.

Pasión por Dios: la Samaritana y nuestra experiencia de Dios.

Si tenemos en manos el texto de Juan 4, 1-42 y leemos atentamente, veremos que el gran momento de aquella mujer samaritana, no está en el texto. Su gran momento fue la decisión de ir a buscar agua aquel día, en aquel horario y en aquel pozo. Alguien estaría esperándola y esto ella no lo sabía. De hecho, no fue su decisión (“No fuiste tu que me elegiste…”). Como ella lo hizo tantas veces, se sumergió en una verdadera aventura, pero diferente de las otras veces, esta aventura le trajo verdadero sentido. Ella realizó una experiencia de plenitud, de vida eterna.

Experiencia tiene que ver con desinstalación, con disposición. Si quiero experimentar algo, tengo que estar dispuesto. “No existe experiencia desinteresada. Sólo puede experimentar alguna cosa quien desea experimentar” (Scholl). Toda experiencia exige una apertura interior, un abrirse para dejar que lo nuevo entre dentro de nosotros y disposición para dejarnos alcanzar y tocar por aquello que bien a nuestro encuentro.

Experimentar muchas veces, tiene que ver con sufrir. Quien quiere preservarse de todos los peligros tendrá que quedarse en casa. Ponerse en camino puede ser peligroso. Quien quiera experimentar alguna cosa tiene que arriesgarse. Aquel que sale de viaje está corriendo un riesgo. Sin correr riesgos, nadie puede experimentar cosas nuevas.

A partir del Cantar de los Cantares, sabemos que la razón de buscar a Dios es que Dios nos buscó y nos tocó con su amor. Nuestra búsqueda de Dios es, por lo tanto una historia de amor. Nuestro anhelo por el amor de Dios sólo ha de cerrarse con la muerte, cuando nos encontremos con Dios definitivamente. El día que desistamos de buscar a Dios, pasaremos a contentarnos con cosas sin valor, como el hijo pródigo de la parábola (Lc. 15, 11-32). Ese día buscaremos saciar nuestra hambre con las bellotas destinadas a los cerdos. Sólo mientras buscamos a Dios es que nuestra alma permanece viva.

A través de esta situación (encuentro con la Samaritana), Jesús nos garantiza que nuestra vida es el verdadero lugar del encuentro y de la experiencia de Dios. Si no conseguimos sentir a Dios es porque no tenemos coraje de sentirnos nosotros mismos. Falta coraje para admitir nuestras limitaciones reales. Lo que escondo de mí mismo, esconde de mi el rostro de Dios. Siendo así, continuaré con sed, vacío. Percibimos entonces, que Jesús sólo se reveló cuando la mujer se desarmó.

Dios mismo colocó en nuestro corazón el deseo de la eterna comunión con él. Queramos o no, en todo cuanto buscamos apasionadamente, en último análisis, estamos en búsqueda de Dios. Esta mujer trilló por tantos caminos y… nada. Jesús la ayudó a descubrir que su sed era sed de sentido, sed de Dios.

Todos nosotros conocemos las célebres palabras de San Agustín: “Inquieto está nuestro corazón mientras no descanse en Ti, o mi Dios”. Y todavía: “No creo que pueda encontrar algún cosa que desee tanto como Dios”. Nuestra vocación es mantener vivos los deseos del corazón, para que así permanezca abierto para Dios, y para que este corazón se abra también para las otras personas. Cuando me interrogo por mi deseo más profundo, descubro cómo desearía responder al deseo que Dios tiene por mí, al amor de Dios. Mi deseo más profundo consiste en hacer enteramente transparente para el amor y la bondad de Dios, para la misericordia y la dulzura de Dios, sin falsificación alguna por mi egoísmo, sin ningún oscurecimiento por medio de mi propia necesidad de reconocimiento y de éxito. Así estaré siempre más abierto a las necesidades ajenas como el buen samaritano.

Para preguntarse: ¿ en qué sentido me identifico con la samaritana en mi pasión por Dios?

Pasión por el ser humano: ser Buen Samaritano para encontrar a Dios

Los discípulos vieron a Dios en el rostro de Jesucristo. En el encuentro con el ser humano Jesús, Dios se manifestó a ellos. En la forma como Jesús hablaba, en su forma de mirar, de tocar, de dirigirse a los otros, ellos experimentaron a Dios. “Quien me ve, ve al Padre” (Jn 14, 9).

No es sólo en Jesús que podemos tener la experiencia de Dios, sino también en cada ser humano. En el monaquismo primitivo, tenía mucho vigor estar palabra: “Quien ve al hermano, ve a Dios”. El mismo Jesús, en el discurso del juicio final en Mt. 25, 31-46, se identificó con los pobres, los enfermos, los sin ropa y sin techo.

En verdad, para con estos caídos al borde del camino, debo tener las mismas actitudes de Cristo. Este es mi lugar de encuentro con el verdadero Dios. Tomando el texto de Lc. 10, 25-37, vemos que Jesús es el Buen Samaritano, por excelencis, pues se inclinó hasta nuestra miseria, nos levantó y nos curó. Nos invita a tener las mismas actitudes y sentimientos. Quien reconoce al propio Cristo en el rostro de quien sufre necesidad, hay que ir a su encuentro de una forma diferente y tratarlo de manera diferente. No podemos ver a Dios directamente en el ser humano. Es necesario tener ojos de fe para en esta persona concreta ver más allá de lo que ven los ojos. Tengo que meditar profundamente en el misterio del ser humano. No puedo restringir al otro aquello que en él percibo. En cada uno está presente un misterio que lo ultrapasa, un nucleo divino, y más, Dios mismo vive en cada ser humano. Si realmente medito sobre el otro, he de reconocer cuan poco se sobre él, y como en el me deparo con algo que no soy capaz de describir. Es Dios, en último análisis, quien brilla para mi en mi hermano y en mi hermana. Para que el otro sea mi prójimo, necesito hacerme prójimo de él.

De muchos santos se cuenta que Dios vino a su encuentro justamente en el rostro del pobre y del enfermo. Cuando San Martin compartió su manto con el pobre, Cristo se le apareció en sueños y le reveló que aquel pobre era él mismo. Cuando San Francisco besó al leproso, en él reconoció a Cristo. Precisamente en la persona que no tiene nada atrayente para presentar a los otros puede brillar para nosotros el misterio de Dios. Esta realidad tampoco fue difícil para Calabria que, a partir de su descubrimiento sobre la paternidad de Dios, no consideraba como extrañas a las personas que venían a su encuentro, sino hermanos y hermanas para ser amados y recibidos, principalmente si pasan necesidad. Podemos ejercitarnos para considerar al otro con los ojos de la fe. Pero para que en el otro podamos experimentar al mismo Dios, es necesaria su gracia. Siempre es apenas por un momento que Dios brilla para nosotros en el otro. Después ya no lo vemos más. Pasa con nosotros lo mismo que le pasó a los discípulos de Emaús. En el momento de partir el pan “se le abrieron los ojos y lo reconocieron, pero él desapareció” (Lc 24,31).

La experiencia de Dios en el rostro del hermano o de la hermana, exige de nosotros una total sensibilidad y atención. Se trata de una manera diferente de relacionarse. No podemos permitir que nuestros encuentros con las personas sean tan vacios al punto de impedirnos hacer la experiencia del eterno, del Dios amor. Con seguridad, cada encuentro es un compartir que se hace y nunca salimos más pobres. Dios nos ayude a no perdernos un solo instante de los que se nos da para experimentarlo y que estos encuentros sean verdaderamente llenos de sentido.

Para preguntarse: en mi historia personal, ¿ cómo he vivido la pasión por el ser humano para llegar a Dios?

Fr Josuel Ndega
Traducion: Nomade de Dios

MNASEMA KUWA MIMI NI NANI?


Tafakari kutoka Zek 12,10-11:13,1; Wag 3,26-29; Lk 9,18-24


       Katika somo la kwanza Bwana aliahidi kuwafanya watu wake wenye unyeti kwa kuwapa roho ya huruma na dua. Bila aina hii ya roho hakuna mtu anayeweza kukiri udhaifu wake, kumwomba Bwana huruma yake na kupata maisha mapya iliyo matokeo ya tendo la Mungu maishani mwake. Kulingana na somo la pili utambulisho wetu ni kuwa wana, yaani wana wa Mungu na kwa hivyo, kuwa ndugu wa watu wengi kwa sababu ya utume wa Kristo ambaye alitufanya kuwa wamoja, ingawa sisi tu tofauti. Ubatizo wetu ni ishara halisi ya hali hii ambayo tunaunganishwa na Kristo na katika Kristo ili tuweze kuishi kwa ushirika kuhisi uchungu na furaha za wana wengine wa Mungu kwa sababu sisi tu watu wa Kristo.

           Katika injili, kabla ya kufunua jambo muhimu kwa wanafunzi wake na kuwauliza swali la msingi, Yesu alikuwa akisali. Mara nyingi injili zote zinamjulisha Yesu akisali kama alama ya ushirika wake na Baba na pia kama maonyesho ya umuhimu wa tukio lifuatalo. Ushuhuda wa sala kutoka kwa Yesu ni msukumo/msaada ili wanafunzi waweze kuelewa kwamba hakuna njia nyingine kwa uaminifu katika safari ya wito ila kupitia sala. “Lililo kweli kwa Yesu nila kweli pia kwa kila mtu. Ni katika mazungumzo ya moyoni na Mungu, ninapokubali kuhojiwa naye na hata wengine, na kisha kujikubali nilivyo mwenyewe... Ni pale tu tunapokuwa na mawasiliano na Mungu kwa njia ya sala ndipo tunapoanza kujielewa tulivyo.”

        Ingawa Yesu anajua mtazamo wa watu kumhusu yeye, alitaka kuwauliza wanafunzi wake maswali kama nafasi nzuri ya kuwafundisha vizuri kuhusu utambulisho wake wa Masiha wa Mungu. Jibu la kwanza la wanafunzi linadhihirisha kwamba watu hawakuwa na wazo kamili/wazi kuhusu Yesu na wakaridhika kwa kumlinganisha na manabii wa zamani. Kwa maneno mengine walikuwako mbali na matarajio ya Yesu. “Kumwita Yesu nabii ni nusu tu ya ukweli wote. Manabii huandaa njia kwa ajili ya mtu mwingine. Lakini Yesu pekee ndiye ambaye njia yake iliandaliwa na manabii wengine wote.” Kupitia jibu la pili, Petro pamoja na wengine walitambua umasiha katika Yesu, lakini hawakuwa na wazo kamili kuhusu umasiha wa Yesu. Maana ya kufikiri hivi ni kwa sababu ya mawazo yao ya kiyahudi. Kulingana na mawazo hayo Masiha wa Mungu anapaswa kuwa shujaa na mwenye nguvu ili aweze kuwakomboa watu wa Israeli kutoka utawala wa Roma. Kwa maneno mengine walikuwa na mawazo ya upungufu kuhusu utambulisho wa Yesu kama Masiha wa Mungu. Yesu aliwataka kama wanafunzi wake lakini haiwezekani kuwa wanafunzi wa Yesu kwa njia yoyote. Maana tofauti ya umasiha na ile ya mwalimu ni hatari Ili wafikie mafanikio katika safari yao.


          Kisha, Yesu aliamua kuwaeleza maana ya umasiha wake kwa kusahihisha mtazamo wao. Umasiha aliochagua Yesu ni umasiha wa mtumishi wa Bwana ambaye alijiona kupakwa mafuta ili atangaze wokovu wa wa Mungu kupitia kukataliwa, mateso, kufa na kufufuka kwake. Njia ya utukufu wa masiha huyu inatokea kupitia njia ya utupu na unyenyekevu. Yesu anapendekeza njia hii kwa wote ambao wanataka kumfuata kwa uaminifu. Kwa maneno mengine Kristo anaujulisha msalaba kama njia ya utukufu. Utambulisho wa wanafunzi na mwalimu Yesu kunatokea kupitia hali ya msalaba wa kila siku. 

          Kristo ambaye tunamfuata anajua vizuri hali yetu naye alichukua changamoto nyingi za kila siku hadi msalaba kama kilele. Kwa upande wa Kristo msalaba ulikuwa sehemu muhimu katika mwendo wa kufanya mapenzi ya Mungu na kudhihirisha mpango wa upendo wake. Kwa upande wetu kama wanafunzi msalaba wa kila siku ni ishara ya utayari wetu kwa kuruhusu kuongozwa na Mungu na kukaribisha mapenzi yake kwa maisha yetu. Kwa kufikia lengo hili tunapaswa kujikataa na kujisahau wenyewe ili wengine waweze kukumbukika. Tunapaswa kujikataa wenyewe ili Mungu aweze kujifunua kwa nguvu yote ya upendo wake. Kujiondoka kutoka katikati/mahali muhimu ili wengine waweze kuwa na nafasi zaidi. Kwa maneno mengine, tunapaswa kuwafikiria wengine kuwa wamuhimu zaidi kuliko sisi wenyewe. Kama haiwezekani kumfuata Kristo bila msalaba, mfano wake wa uaminifu kwa mpango wa Mungu utuimarishe ili tuchukue msalaba wetu wa kila siku, kumfuata kwa uaminifu na kufanya mapenzi ya Mungu. 

Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah

MUNGU ANATUPATIA YALE TUNAYOHITAJI


Kutafakari kuhusu Mt 6, 24-34

Kifungu hiki cha injili ni andiko la msingi wa kiroho ya Mt. Yohane Calabria. Huyu ni mwanzilishi wa Shirika letu, yaani, Poor Servants of Divine Providence. Alianza kuwajali watoto maskini na yatima kwa sababu alitambua kwamba tendo hili lilikuwa mapenzi ya Mungu. Nambari ya watoto iliongezeka daima na vyakula havikutosha kwa wote. Lakini Mungu aliyekuwa makini sana kwa hali hii, akapatia daima yale ambayo Yohane Calabria na watoto waliyahitaji kwa kuishi. Hali hili ilidhihirisha maneno ya injili ambayo tunatafakari.
Kwa upande wa Mungu, yeye anajua kwamba tunahitaji mambo hayo yote. Kwa upande wa binadamu ni lazima kuwa na imani na kujisalimisha mikononi mwa Mungu ambaye ni Baba na Mtoaji. Mtakatifu Yohane Calabria alikuwa na uhakika kuhusu hali hii kwa sababu “aliishi injili na kwa injili”. Kupitia Injili aliugundua ubaba wa Mungu kwa njia halisi sana. Ugunduzi huu mkubwa ulisimuliwa na Askofu aliyeitwa Chiot kutoka Jimbo la Verona - Uitalia ambaye alitembelewa na Mt Calabria kwa kumjulisha kuhusu tukio muhimu. Huu ni msukumo katika safari yetu kama watoto wa Mungu.
“Usiku mmoja, padre Calabria aliandika na kuituma barua kwa baba askofu Chiot akisema, “ningojee kesho saa nne asubuhi maana nahitaji kuongea nawe. Wakati padre Calabria alipofika nyumbani mwa Askofu Chiot, baba huyo alimwuliza swali: Je, bahati mbaya gani ilitokea? Barua yako ilinisumbusha. Padre Calabria akamwambia, “hapana bahati mbaya; hili ni jambo la ajabu.” - “La ajabu!”, aliuliza baba Chiot. Naye padre Calabria aliendelea kwa kusema, “Alisoma injili nzima!” Baba askofu alisema, “Hili si jambo la ajabu!” Je, inawezekana kuwepo padre ambaye hajasoma injili nzima?” Padre Calabria alisema, “Tafadhali, niruhusu kueleza. Mimi pia nimekwisha soma na kuihubiri injili, lakini juzi baada ya kuishi kwa ugumu mchana kutwa na bila kupata utulivu kwa kulala usingizi, nilichukua inijili na kuisoma nzima pamoja na kitabu cha Matendo ya Mitume. Nilipata kusoma kila kitu kwa usiku mmoja peke yake. Jambo hili lilisababisha uzoefu wa ajabu maishani mwangu. Kweli injili ni jambo kubwa! Nimestaajabia. Hebu, sikiliza! “Msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini, au kuhusu miili yenu, mtavaa nini. Waangalieni ndege wa angani, wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Fikirini maua ya shambani yameavyo. Hayafanyi kazi wala hayafumi. Lakini nawaambia, hata mfalme Solomoni katika fahari yake yote hakuvikwa kama mojawapo ya hayo maua.”
Padre Calabria ailikuwa amesisitiza yaliyomhakikishia maana ya kweli ya kuishi na kutangaza, yaani Mungu ni Baba nasi tu watoto wake. Alichukua kama ahadi na mpango wa maisha kwake na kwa shirika lake zima maneno ya mstari wa 23, yaani, “Mtafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake na hayo yote mtapewa kwa ziada.”
Je, Maneno haya yana maana gani katika safari yetu siku ya leo? Kulingana na Yesu hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili, yaani Mungu na mali. Mali inaweza kuvuruga uangalifu wetu kwenye njia ya Mungu ya kutenda na kuwajali watoto wake. Yesu hakanushi kwamba sisi tunahitaji mambo mengi. Lakini anajua kwamba kosa la utambuzi linatuongoza kuishi kwa wasiwasi na kusumbukika kuweka uangalifu katika yale yasiyo muhimu sana.
Kulingana na mafundisho tumepokea kutoka kwa Yesu Mungu ni Baba kabla ya kuwa Muumba. Yeye si kama baba yeyote bali yu Baba Mwema ambaye anashughulika sana na hali ya wana wake. Yeye analinda na kutunza bila kulala. Yeye anajua mahitaji ya wana kabla ya wamwombe kitu. Kwa utunzaji wa upendo Mungu anashiriki zawadi zake na wana wake, kutarajia kwamba tufanye vivyo hivyo kwa ajili ya wengine ili undugu kati yetu uwe maonyesho ya ubaba wake. Matatizo yote yapaswa kufikiriwa na kusomeka kwa maelewano na ubaba wa Mungu.” Mungu hamsahau hata mmoja wa wana wake.

Tunaalikwa kumwelekea kwa imani na kuwa na uhakika kwamba tumepokea sana. Mungu hatupatii daima yale tunayomwomba, bali anatupatia daima tunayohitaji. Ikiwa hatupokei yale tunayomwomba yeye ni kwa sababu hatuombi ipasavyo. Tufanye upya imani yetu katika riziki yake kuwa na tabia kamili katika ushusiano wetu naye.  

Fr Josuel Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah

ALISAMEHEWA KWA SABABU ALIPENDA SANA

Kutafakari kuhusu Lk 7:36-8,3



     Tukio hili la mwanamke mwenye dhambi lilitokea humo nyumbani kwake Simoni Mfarisayo, aliyemwalika Yesu kula chakula. Yesu Alipokuwa mezani akila pamoja na wageni wengine mwanamke huyo anayefahamika kama mwenye dhambi akatokea na kuanza kumkaribia Yesu akimwonyesha ishara za upendo na shukrani kwa sababu aliuona msamaha na upendo wa Mungu katika hali yake ya dhambi. Ingawa Simoni alichukwa ahadi ya mwaliko, ni Yesu mwenyewe aliyetaka kukutana na Simoni na kumwongozea njia mpya ya kuishi. Kwa kweli Simoni alihitaji njia mpya, mtazamo mpya na kadhalika. Alimwalika Yesu lakini hakujua jinsi ya kumkaribisha vizuri. Yeye alisahau ishara za msingi kama zilivyokuwa desturi miongoni mwa Wayahudi, yaani, hakumpa Yesu maji kwa miguu yake; hakumbusu Yesu akionyesha kwamba alipendezwa na kutembelea kwake; hakumpaka kichwa chake Yesu mafuta.

      Katika injili ya Luka, Yesu anapenda kushiriki pamoja na watu katika chakula. Kwa kushiriki milo na watu wa aina na ngazi zote katika jamii, Yesu alionyesha kuwa yeye alikuwa wa watu wote, matajiri na maskini pamoja. Tukumbuke wakati alipokula chakula nyumbani kwake Mathayo pamoja na wenye dhambi wengi; tukumbuke pia wakati alipojikaribisha mwenyewe kwa karamu nyumbani mwa tajiri Zakayo. Kutembelea kwake Yesu kunasababisha mabadiliko maishani mwa watu kuwaongoza kufikiri na kutenda tofauti. Katika injili ya leo, ingawa alikuwa Simoni ambaye alimwalika Yesu nyumbani kwake, ni mwanamke fulani ambaye alimkaribisha vizuri. Mwanamke huyo ingawa hana jina, yaani heshima, hata hivyo ana ishara ambazo Yesu alitarajia kukuta kutoka kwa Simoni aliyejiona amejaa heshima. Mtazamo wa upungufu wa Simoni uliona kwanza udhaifu na makosa ya mwanamke. Lakini Yesu alimwalika Simoni kuona vizuri, akisema, “unamwona mwanamke huyo?” Huu ni mwaliko wa kuanza tena na kuona tofauti, kama Yesu mwenyewe alivyo. Yesu anajua dhambi nyingi za mwanamke huyo, hata hivyo anatambua kwanza ishara nyingi za upendo ambazo zinashinda udhaifu wake. Kwa upande wa Yesu upendo unashinda dhambi naye mtu anathamini zaidi kuliko makosa yake.  

         Katika mazingira yale, Simoni ni mmoja miongoni mwa waliojiona kuwa wenye haki na kwa hivyo, walijiona pia kwa mamlaka ya kuwachagua baadhi ya watu na kuwakataa wengine. Yesu anaukubali mwaliko wa Simoni, lakini haukubali mwelekeo wake wa kumhukumu mwanamke aliye miguuni mwake. Yesu anataka kwamba Simoni atambue kuwa mgawanyiko kati ya watu wazuri na wabaya haukubaliki mbele ya Mungu. Katika njia ya Mungu ya kutenda ubaguzi hauko. Pendo na huruma yake yapatikana kwa wote. Kwa hivyo Yesu alimsamehe mwanamke huyo na kupendekeza toba kwa wengine. Hili ni sharti ili huruma ya Mungu iwe ufanisi maishani mwao. Kama hivi Yesu alitangaza ufalme wa Mungu na wale ambao walimfuata waliruhusu kuguswa na huruma ya Mungu. Ni jambo la ajabu kwamba injili hii inaanza kwa mwanamke bila jina na kuhitimisha kwa majina kadhaa ya wanawake, yaani, Mariamu, Yohana, Susana na wengine wengi waliopokea tena heshima yao kwa sababu ya mkutano na Yesu na huruma ya Mungu.


      Kama ilivyotokea kwa mwanamke huyo, sisi pia tunaalikwa kujiona kukaribishwa na kubadilishwa kwa sababu ya mkutano na huruma ya Mungu hasa kupitia uzoefu wa sakramenti ya kitubio na upatanisho. Uzoefu huu tena unatusaidia kuushinda mwelekeo wetu wa kibinadamu wa kuwahukumu wengine na kuuona makosa yao kuliko tabia zao nzuri. Wakati tunapowahukumu tunajiona wenye haki, yaani tunajiona bora kuliko wengine. Je, ni nani aliye mwenye haki mbele ya Mungu? Tunaalikwa kuweka juhudi zaidi ili tuweze kuwaona wengine kwa mtazamo wa Yesu. Kama ilivyotokea katika tukio la mwanamke, Yesu anaona upendo wetu kwa kanisa, kwa jumuiya, kwa familia juu ya yote. Nao upendo wetu unaonyeshwa kupitia uzoefu wetu wa kusamehe, wa kuwakaribisha wengine vizuri na kuwatendea mema. Kusamehe ni asili ya Mungu (Kut 34:6). Hatuununui msamaha wa Mungu kwa mapendo yetu bali tunaupokea kwa hiari. Ekaristi hii takatifu itusaidie kupenda na kusamehe kama Mungu alivyo. 

Fr Josuel Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah

sábado, 4 de junho de 2016

MUNGU AMEWAANGALIA WATU WAKE


Kutafakari kuhusu 1Waf 17, 17-24; Wag 1, 11-19; Lk 7, 11-17

Liturujia ya jumapili hii inatualika kuona huruma ya Mungu kwa kwa ajili ya wote wanaoteseka. Mungu anaguswa na hali yetu na kutenda kwa huruma kwa sababu hii ndiyo tabia yake mwenyewe na kwa sababu tena anataka tujifunze kutoka kwake mfano mzuri wa kutenda. Turuhusu kusaidiwa na neno lake ambalo linaimarisha imani yetu na kuutoa mwelekeo kamili kwa maisha yetu. Neno hili ni kweli kinywani mwa Eliya alipompa mama mjane mtoto wake aliyefufuka. Hili tena ni kweli kupitia mahubiri ya Mtakatifu Paulo alipoutangaza ufunuo wa Yesu Kristo kama habari iliyojaa maana. Neno hili linaendelea kusababisha hali mpya kabisa maishani mwa wote ambao wanamtumainia Mungu.
Katika sehemu ya mwisho injili inaongea kwamba “habari hii ikaenea katika Uyahudi wote. Na katika nchi zote za kando kando. Hii ni habari kuhusu kutembelea kwake Mungu kuwakomboa watu wake kupitia Yesu aliye Nabii mkuu. katika Yesu Mungu anajifunua kama aliye karibu sana na mwenye unyeti sana. Kwa hivyo ni halali kusema kwamba Mungu wetu anao “moyo”. Tulisherehekea hali hii katika Ijumaa iliyopita kupitia Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu. Yesu mwenyewe alisema kwamba Yeye yu mpole na mnyenyekevu wa moyo. Katika moyo wake zinakaa hazina za hekima na elimu. Kutokana na moyo wake tumeona tendo la huruma ya Mungu. Mfano wake wa unyeti ni mwaliko wa kuboresha tabia za wema na upole kama alama ya utunzaji wa Mungu. Habari ya njia maalum ya Mungu ya kuwajali watu wake inapaswa kutangazika. Habari hii inaiimarisha imani na kuyafufua matumaini kama ilivyotokea maishani mwa mama yule mjane ambaye alikuwa amempoteza mwanawe wa pekee, lakini akampokea tena kwa sababu ya hisia za moyo wa Yesu.
“Wakati Yesu alipomwona mama yule... akamwonea huruma.” Injili zote zinamjulisha Yesu kama yule aliyeguswa na mahangaiko na mateso ya watu. Huruma ni tabia yenyewe ya moyo wake. Huruma hii inamsukuma kutenda vitendo, ili kuwapunguzia wanaoteseka uzito wa mateso na mahangaiko yao. Mbele ya mahangaiko ya wanadamu Mungu amejibu daima kwa jibu kamili ambalo linaonyesha njia maalum yake ya kupenda. Upendo wake si kitu cha kinadharia bali “kwa mwonekano wake unaonyesha kitu cha kushikika: nia, mitazamo na tabia zinazoonyeshwa katika maisha ya kila siku.” Njia maalum ya Mungu ya kujibu mbele ya maumivu ya kibinadamu inamaanisha mahangaiko ya upendo wake kwetu. Watu walitambua huruma na ukombozi wa Mungu kupitia tendo la Yesu. Hivyo, walifikia lengo la utume wa Yesu, yaani, kudhihirisha huruma ya Mungu. “Kila kitu ndani yake kinaongelea huruma. Hakuna chochote kwake kinachopungukiwa na huruma. Tendo lake kwa ajili ya maisha ya watu linafunua kwamba Mungu anatamani wawe wenye afya njema; anataka kuwaona wenye furaha, wenye kujaa furaha na amani."

            Kanisa linatufundisha kutangaza kwamba “moyo wa Yesu ni chemchemi ya huruma” na Neno la Mungu lenyewe linashuhudia kwamba “Kwa upande wake tumepokea neema juu ya neema”.  Tunaalikuwa kuamini kwamba Yesu ni mwenye unyeti sana mbele ya hali yetu hasa nyakati za maumivu na huzuni, ambazo zinaonekana kwamba sisi tumeachwa peke yetu. Katika Kristo Mungu ni mwenye unyeti hasa kwa kutufundisha njia kamili ya kuwa binadamu wa kweli, yaani, njia ya kusaidiana na kumpa Mungu nafasi ya kutenda maishani mwetu kwa nguvu ya upendo wake. Yeye tunayemwamini ni Mungu wa uhai naye amependezwa kutushirikisha katika uzima wake wa milele, kwa sababu sisi tu wanawe wapendwa. Tujihakikishie kwamba Mungu hawezi kutuacha wala kunyamaza mbele ya kinachotokea kwetu. Ikiwa katika Yesu, yeye anajifunua kama ufufuko na uzima, tunapaswa kutangaza kwamba Mungu hataki kifo. Hali hii inatupa matarajio kuhusu kufufuka kwetu na maisha kamili kwani yeye si Mungu wa wafu bali wa wanaoishi. Kulingana na mapenzi yake maisha yetu yanafaa kupata ukamilifu. Neema ya Mungu iimarishe imani yetu katika riziki yake kwa sababu yeye yupo karibu nasi daima na hawaachi kamwe wale wanaomwamini.

Fr Josuel Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah

MOYO SAFI KABISA WA BIKIRA MARIA


Kutafakari kutoka Is 61: 9-11; Lk 2: 41-51

Tunaadhimisha kumbukumbu ya moyo safi kabisa ya Bikira Maria. Kumbukumbu hii ni uenezi wa sikukuu ya Moyo Mtakatifu wa Bwana ambayo tulisherehekea jana. Tunaalikwa kutafakari kuhusu uwezo wa Mama Maria wa kuweka moyoni mwake Neno la Mungu na kuzaa tunda zuri kwa ajili ya dunia kulingana na mpango wa Mungu. Tunaalikwa kutafakari pia mshikamano wa Mariamu mbele ya mateso ya mwana wake kama ushirika wa mioyo miwili.

          Somo la kwanza, kutoka kitabu cha Isaya, linaongea kuhusu uhusiano wa kina kati ya Mungu na watu wake. Yeye anaitumia nguvu yake ili atende matendo ya ajabu kwa ajili ya wokovu wa watu wa Israeli. Mungu ni mwaminifu kwa watu hawa na kuahidi kuanzisha agano jipya la milele, kuuthibitisha ukaribu wake nao na kuwaalika kuishi uhusiano naye kwa hisia ya miliki. Uhusiano huu na Mungu unawahakikishia baraka nyingi na kuwabadilisha kuwa mfano kwa mataifa yote. Hali hii inafanana na ndoa, yaani, Mungu ni kama mume na watu kama mke. Watu wanaalikwa kwa shukrani na furaha kwa sababu Bwana mume wao ametenda makuu kwa ajili yao, akiwavalisha kwa wokovu na ushindi. Jumuiya ya kikristu hutafsiri hali ya mke huyo kama mfano wa Bikira Maria ambaye alikuwa mtumishi mwaminifu akikubali kumzaa Yesu kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu mzima.

       Injili inaongea kuhusu ushiriki wa Familia takatifu (Yesu, Maria na Yosefu) katika jumuiya yake. Ushiriki wa Familia hii katika jumuiya ulikuwa desturi. Miongoni mwa Wayahudi kila Myahudi anapaswa kwenda Yerusalemu angalau mara moja kwa mwaka kwa sababu ya sherehe ya pasaka pamoja na wengine. Hivyo, Yesu alikuwa kijana wa umri wa miaka kumi na miwili, na ilionekana alipotea hekaluni, lakini kwa kweli yeye alijikuta mwenyewe kwa sababu kwa kuhusishwa na kushughulika kuhusu hali ya Baba yake kunampendeza. Hali hii ilikuwa ngumu sana kwa wazazi wake wafahamu. Lakini walikuwako tayari kuyakaribisha na kuyatenda mapenzi ya Mungu. Hasa kwa upande wa Bikira Maria, ingawa hakufahamu vizuri hali hiyo, alikuwa na tabia nzuri ya kuweka moyoni mwake mambo hayo yote, akitafakari na kutafsiri ili atende mapenzi ya Mungu. Kama hitimisho, mtoto Yesu alirudi Nazareti pamoja na wazazi wake na alikuwa anawatii. Hata utiifu kwa Mungu ulikuwa utambulisho wa wana wa familia hii. 

      Kulingana na kumbukumbu ya leo, tunaalikwa kuulenga uangalifu wetu kwenye moyo wa mama Bikira Maria, aliye mfano maalum wa mtumishi, wa mke na wa mwanafunzi kwa wote. Maria aliishi uhusiano wa ndani na Mungu kwa sababu moyo wake ulikuwa mali ya Mungu na ulikuwako kwa Mungu. Maria alikuwa makini sana kwa matendo ya Mungu katika historia ya watu wake. Moyo wa Bikira Maria ulikuwa makao ya Mungu, mahali pa kwanza ambapo Yesu alizaliwa. Kulingana na Wazee wa Kanisa, “Kabla ya kumzaa Yesu tumboni mwake, Maria alimzaa moyoni mwake.” Kwa hivyo haikuwa ngumu sana kwake Mariamu kuishi ushirika wa kina na moyo wa mwana wake Yesu. Mbele ya mateso ya Mwana, tunaitafakari huruma ya Mama, anayejua jinsi ya kupenda na jinsi ya kuteseka kwa ajili ya yule anayependa. Maria alichukua katika moyo wake uchungu wote wa mwanawe. Hivyo utabiri wa Simeoni hekaluni ulitimizika, yaani, alipochukua mtoto Yesu mikononi mwake, alimwambia mamaye, “Upanga utachoma moyo wako mwenyewe”.       


      Kati ya tabia kadhaa za Bikira Maria tukaribisheni ushuhuda wake wa ukimya kama mwanafunzi wa kwanza na mwaminifu wa Mwanawe. Yeye alichukua jukumu lake hadi matokeo ya mwisho. Wakati wanafunzi wengine walienda zao, Maria akabaki amesimama kando ya msalaba. Hebu mfano huu wa Maria utuimarishe ili tuweze kuishi kwa uaminifu utambulisho wetu kama wanafunzi wa Mwana wake Yesu na tujifunze jinsi ya kujitolea kabisa kwa wema wa engine.   

Fr Josuel Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah

ECUMENISMO: RECONOCIENDO LA DIFERENCIA COMO UNA GRAN RIQUEZA


Estamos por celebrar cincuenta y cinco años del inicio del Concilia Vaticano II, verdadero Pentecostés para la vida de la Iglesia. Una de las grandes contribuciones que este Concilio trajo fue una nueva comprensión en el campo ecuménico. El documento específico en esta materia se llama Unitatis Redintegratio y es del que tenemos la siguiente afirmación: “(…) Es menester que los católicos reconozcan, con alegría, y estimen los bienes verdaderamente cristianos, oriundos de un patrimonio común, que se encuentran entre los hermanos separados. Es justo y necesario reconocer las riquezas de Cristo y las obras de virtud en la vida de los que testimonian en favor de Cristo, a veces hasta la efusión de sangre: Dios es siempre admirable y digno de admiración en sus obras” (UR 4/772).

Las diversas iniciativas, en el campo ecuménico emprendidas por las iglesias cristianas has sido fruto de un deseo intenso de comunión. Es impresionante el esfuerzo incansable de aproximación, comprensión y diálogo, existentes en las diversas organizaciones de los que confiesan la misma fe, en todo el mundo (claro que me estoy refiriendo a las Iglesias envueltas en el movimiento ecuménico). Como vimos arriba, es en el reconocimiento mutuo de lo que Dios realiza en cada una de las partes que sucede la comunión. Todo eso nos hace descubrir la dinámica del Espíritu Santo, para el cual no existen fronteras que no puedan ser superadas. En medio de tantas diversidades, viene suscitando la unidad. Este Espíritu de Comunión ha hecho maravillas a lo largo de la historia, principalmente en lo que se refiere a la propia concepción ecuménica, en que cada una de las partes envueltas se armaba con muchos argumentos para defender su verdad sobre Jesús, criticando los otros, considerándose dueños de la verdad, fijándose más en sus diferencias, en aquello que causaba todavía más división. Hubo una apertura mayor para la acción del Espíritu de manera que pasaran a percibir que el camino no era aquel, se cambió la postura y el dialogo pasó a nortear las discusiones. Se descubrió que la diferencia de cada uno puede ser riqueza para el otro; es necesario caminar y juntos buscar lo que es factor de comunión.

El discurso sobre la búsqueda de la unidad, infelizmente fue mal comprendido tanto por parte de algunos líderes como por parte de otros fieles. Lejos de  ser uniformidad o anulación de las diferencias individuales, se trata de acoger lo diferente, respetándolo en su manera de ser y reflexionar, descubriendo siempre más lo que causa aproximación. Esta búsqueda no impide que se piense diferente, al contrario, a través de la diversidad, ambas partes son conducidas a la verdad que nos une. Cuando Jesús dice que él es la verdad y quien es de la verdad escucha su voz, se refiere a los ritos, formulas y maneras de hacer las “cosas”, características accidentales. Él llama la atención para lo que es esencial: la verdad que Él es. Una cristología que parte de Jesus como parámetro de la verdad es una cristología que conduce a la unidad. Esta es una referencia común a todos. Y como la verdad es Jesús, la búsqueda de conocerla siempre más sólo puede llevarnos a envolvernos con el diálogo ecuménico. Rechazarlo conscientemente sería un acto de irresponsabilidad, pecado o ir contra aquello que reconocemos ser correcto.

El camino de aproximación se inició, el paso caracterizado por la fraterna superación de las divisiones entre las diferentes Iglesias cristianas, ya ha sido dado. Lo que resta ahora es que todos contribuyan para vencer las dificultades que impiden el avance ecuménico. El Espíritu actuó, hizo que disminuyéramos las tensionas; ahora tenemos la gran responsabilidad de ser fieles a la verdad y a la justicia mientras buscamos superar las diferencias y trabajar en conjunto. Sabemos también que el camino ecuménico debe ser trillado con caridad, humildad, prudencia, buena formación y amor al cristianismo. El papa y santo Juan Pablo II, en su carta sobre la unidad de los cristianos, dice que “la división contradice abiertamente la voluntad de Cristo, y es escandalo para el mundo, como también perjudica la santísima causa de la predicación del evangelio a toda criatura” (UUS 6). De hecho, la gran victima ha sido la evangelización, pues es difícil creer cuando los que predican el evangelio se comportan como enemigos. Es claro que no da para generalizar, pero si todavía hay impasse en el entendimiento, es porque algunos líderes de las diferentes partes se cierran, acompañando el proceso con un cierto indiferentismo en relación a la riqueza que esta novedad puede traer. Mucho están con el recelo de quedarse menos católicos, menos protestantes, etc. La verdad es que dejamos de pensar como Jesús, que se preocupaba con los que necesitaban creer a partir del testimonio de unión de las comunidades cristianas. Olvidamos de lo que necesitamos, como cristianos, estar unidos para que el mundo crea.

No es conveniente continuar atemorizando a las personas con un Jesús dividido, un Jesús que sólo sirve para un grupo y no sirve para otro. Está en la hora de ser evangelios vivos, ponernos en el centro de nuestras búsquedas y aspiraciones, la persona y la propuesta de Jesucristo. La actitud de Jesús delante de lo diferente era de escucha y de acogida; necesitamos reaprender de él. Si de hecho somos cristianos y creemos en la posibilidad de unidad rezada por Cristo, realizaremos lo que dice San Agustín: “en las cosas esenciales, la unidad; en las cosas dudosas, la libertad; en todo, la caridad”. Esta expresión es retomada por el Concilio Vaticano II que la propone como compromiso de los católicos y cristianos de todo el mundo: “Resguardando la unidad en las cosas necesarias, todo en la Iglesia, según el munus dado a cada uno, conserven la debida libertad, tanto en las varias formas de vida espiritual y de disciplina, en cuanto en la diversidad de los ritos litúrgicos, y hasta aún en la elaboración teológica de la verdad revelada. Pero en todo cultiven la caridad. Actuando así, manifestarán, siempre más plenamente, la verdadera catolicidad y apostolicidad” (UR 4/771).

Fr Ndega

Traducion: Nomade de Dios