Kutafakari kuhusu Lk
9, 11b-17
Tunaadhimisha sikukuu ya Mwili na Damu takatifu
ya Bwana wetu Yesu Kristo. Sikukuu hii ni ukumbusho wa karamu ya mwisho
tunayosherehekea katika Alhamisi kuu. Lakini, katika siku ile hatuwezi
kusherehekea kwa shangwe kubwa kwa sababu ya kukumbuka mateso ya Bwana. Siku hii
ya leo tunaalikwa kusherehekea kwa shangwe na shukrani pamoja na kanisa zima,
hasa kwa maandamano, kwa sababu ya zawadi hii kubwa ambayo tunakumbuka kufa na
kufufuka kwa Yesu na kujitolea kwake kama chakula chetu cha kiroho. Hiki ni
chakula kinachodumu milele nacho kilishuka mbinguni kuutoa uhai kwa ulimwengu.
Neno Ekaristi linatokana na neno la kigiriki na
kumaanisha shukrani. Huu pia ni mwaliko wa kumshukuru Mungu kwa zawadi nyingi
ambazo tumepokea kutoka kwake na hasa kwa zawadi hii kubwa ya Ekaristi
takatifu. Maandamano ni sehemu ya maonyesho ya shukrani hii. Tunaposhukuru tunaonyesha
kwamba tunathamini zawadi tuliyopewa. Ili tuweze kushukuru tunahitaji kukumbuka.
Kukumbuka katika Ekaristi ni kuishi na kushiriki, kwa sababu Yesu aliwaambia
wanafunzi wake maneno haya, yaani, “Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.” Kwa
maneno mengine, tunapokumbuka Yesu tunashiriki katika tukio ambalo
tunaadhimisha. Basi kusherehekea Ekaristi takatifu ni kuishi pamoja na Yesu,
uzoefu wa kujisalimisha kwake kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu. Ndiye anatushirikisha
katika sadaka yake yenye uzima na utakatifu.
Injili inaongea kuhusu kuzidishwa kwa mikate na
samaki. Kupitia uzoefu huu Yesu aliwalisha chakula umati wa watu na kutangaza
wakati mpya. Andiko hili linakuja baada ya mitume watumwe na Yesu kwa nguvu ya
kuponya wagonjwa na kuondoa pepo wabaya. Waliporudi wakampasha Yesu habari
kuhusu mafanikio ya kazi yao naye Yesu aliwaalika waende pamoja naye kwenye
mahali pa faragha. Mwaliko huu wa Yesu haukumaanisha kujifunga ama kutofautiana
kuhusu hali ya watu. Kisha, watu waliwatafuta; nao ingawa waliivuruga nia ya
Yesu na wanafunzi wake, walikaribishwa vizuri na Yesu ambaye aliwahubiria
habari ya ufalme. Hapo tuko na mwanzo wa uzoefu wa muujiza, kwa maana Yesu
alitambua kuwa watu waliomfuata walikuwa na njaa mbili, yaani, njaa ya chakula
cha kimwili na pia njaa ya kusikiliza neno la Mungu. Kama waliyatafuta maisha
mapya, Yesu akawazungumzia juu ya ufalme na kuwaponya wagonjwa.
Wanafunzi wa Yesu walikuwa wametumwa kuwatumikia
watu, lakini uamuzi wa kumwomba Yesu aufukuze umati unadhihirisha kwamba uzoefu
ule haukutosha kwa kubadilisha mawazo yao. Kwa kutaka kuwaaga watu bila kufikiria
hali yao ya njaa na ya mateso ni kutofautiana, yaani, hili ni kosa la ahadi. Yesu
alishiriki na wanafunzi wake mamlaka yake na pia unyeti wake kuhusu hali ya
watu. Kushiriki hata kile kidogo walichonacho kwa ajili ya watu wenye njaa ni
sehemu ya utambulisho wao kama wafuasi wa Yesu. Kile ambacho walikidhania kuwa
kitu kidogo sana kiweze kuwalisha watu, kwa upande wa Yesu kina thamani kubwa.
Yesu angeweza kufanya muujiza peke yake lakini alipendelea kuwashirikisha
Mitume, akiwasaidia kufahamu kwamba uzoefu wa kumfuata unadai mawazo mapya na
tabia mpya. Shauri ya Kristo alibadilisha tabia ya wanafunzi na kuziweka
kupatikana zawadi za Mungu kwa wote. Kama matokeo ya uzoefu huu, watu
walishiba, wakishinda ukusanyaji na kuepuka ubadhirifu wa chakula.
Kupitia Ekaristi takatifu iliyowekwa na Yesu,
Mungu anatulisha kama alivyofanya na Waisraeli kupitia chakula cha mana. Katika
kila Ekaristi tunayoadhimisha tunaishi tena matendo na maneno ya Yesu akiwahakikishia
wote chakula na kutualika kushinda mwelekeo wa kijamii wa ukusanyaji na ubadhirifu wa chakula ambao unauzuia uzoefu
wa ndugu wa kweli ulio matokeo ya adhimisho la Ekaristi. Ikiwa uzoefu wetu wa
Ekaristi ni wa kweli, tunapaswa kujifunza kushiriki kile tulichonacho na
kufanya kwa ukarimu kile tunachoweza, tukiamini kuwa Yesu yupo nasi na kutunganisha
naye ili matendo yetu yawe ushiriki katika kujitolea kwake kwa uhai wa
ulimwengu.
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah