terça-feira, 29 de março de 2016

PUEBLOS AFRICANOS VENIDOS A BRASIL Y SUS CARACTERÍSTICAS



A través de los datos históricos de estos autores que estamos trabajando, vamos descubriendo que fueron innumerables las culturas y pueblos retirados a la fuerza de sus tierras para ser sometidos a la situación de esclavitud aquí en Brasil. En el artículo anterior mencioné la estimativa en números. En este artículo, quiero trabajar brevemente los tipos de culturas africanas con sus principales características. El autor R. Cintra, acostumbra a dividirlos en tres grandes grupos, que corresponden a los diversos ciclos del tráfico esclavista. Vea íntegramente[1]:
1) Culturas sudanesas, representadas principalmente por los pueblos Iorubás de Nigeria (Nagô, Ijêcha, Egbá, Ketu, Ibadon, Ijebú) y de Daomé (grupo Gêge o Ewe, Fon o Egon) por el grupo Mina de la Costa de Malagueta, de la Costa de Marfil (Krumano, Agni, Zema, Teminí, Gós, Tehis, etc.)
2) Culturas guineano-sudaneses islamizados, representados en primer lugar por los Peuhl (Fulah, Fula) después por los Mandinga (Solmke, Bombara), por los Haussá del norte de Nigeria y por grupos menores, como los Tapa, Bornu, Gurunsi, Komusis y otros.
3) Culturas bantos, constituidas por numerosas tribus del Congo, de Angola y de la Contra Costa (Cabindas, Benguelas, Macuas, Angicos, Caçanges, Rebolos, Muxincongos).
los bantos del Congo y de Angola parecen ser los más primitivos. Vivían en las florestas o en las planicies cerca de la costa, en pequeñas aglomeraciones o tribus. Las habitaciones eran chozas o cabañas de techo cónico. El vestuario era elemental. No conocían los tejidos, andaban semi-desnudos o usaban tangas de fibras de palmeras o cascaras de árboles. Había una gran variedad de razas y lenguas, según los grupos localizados al Norte, al Sur o al Centro. Se dedicaban al pastoreo o a la agricultura básica como azadas de madera (Artur Ramos). Los más civilizados eran los sudaneses, iorubás, nigerianos o daomeanos. Eran altos, corpulentos y activos. Vivían en ciudades, poseían puestos con embarcaciones. Sus jefes eran tratados por los portugueses como reyes. Conocían el tejido y negociaban con los extranjeros “paños de la costa”. Tenían herreros y artistas en cobre, oro y madera. Criaban animales de porte grande y mediano: caballos, ganado, cabras, carneros. Tenían habitaciones de adobe y construían fortalezas. Los sudaneses islamizados haussás, malês conocían los progresos de la cultura árabe. Poseían armas más perfeccionadas. Los fanti y Ashanti, como los habitantes de la Costa de Oro y del Golfo de Guiné, participaban del adelantamiento de la cultura. Negociaban el oro con los portugueses y sabían trabajar metales. Los más poderosos, particularmente los régulos de Daomé y de Lagos, (…) practicaban el trueque con los portugueses o bahianos, cambiando esclavos por rollo de humo (12 rollos de humo a cambio de un esclavo). Agua ardiente, azúcar, harina de mandioca, productos agrícola en bruto, objetos orientales, pólvoras y armas eran también mercaderías usadas en el trueque”.[2]
A esta altura, es importante percibir, que sin saber, los portugueses estaban introduciendo, en esta tierra, personas de tradiciones muy diferentes unas de otras, de religiosidad totalmente diversas; algunos con una capacidad enorme de organización, otros, no tanto; algunos venidos de reinos, otro apenas de una organización tribal. En fin, trajeron personas que al encontrarse – por la rivalidad existente entre ellos – podrían haberse destruido mutuamente[3]. Pero eso no sucedió, pues ahora, delante de toda la distracción causada en sus tierras, restaba sumar fuerzas contra un enemigo común, buscando una manera mejor de reorganizarse para mantener vivas las raíces de la Madre África, rescatando valores y tradiciones. En verdad, el proyecto portugués tuvo efecto contrario, pues, así como el tráfico no cesaba, tampoco cesaba la continua renovación de las fuentes de vida, “estableciendo un contacto permanente entre los antiguos esclavos o sus hijos y los recién llegados en cuyas hileras venían, con frecuencia, sacerdotes, adivinos, médicos- hechiceros, lo que hizo que durante el período esclavista existiese un rejuvenecimiento de los valores religiosas”[4].
En cuanto a la práctica religiosa, ya sucedía algo significativo en las senzalas, aunque sin una organización estructural como casas de culto, terrenos, etc. Sucedían verdaderas celebraciones, sin que sus señores lo notasen. Tratándose de Candomblés, Xangôs y Batuques, como tenemos hoy, se tratan de organizaciones muy recientes, que datan su inicio al final del siglo XVIII y al inicio del siglo XIX[5]. Nuestro estudio, por lo tanto, va a intentar profundizar las prácticas religiosas, buscando su verdadero significado ayer y hoy en África y en Brasil, sin la pretensión de agotar el tema, sino de profundizar los elementos comunes de dialogo y de encuentro cultural, con el fin de que, en nuestra síntesis teológica, descubramos la acción del Dios de la vida, presente en las diversas manifestaciones del Pueblo Negro.

Fr Ndega
traducion: Nomade de Dios



[1]CINTRA, R. Candomble e Umbanda. p. 32; Veja dados correspondentes e complementares em BASTIDE, R, Religioes Africanas no Brasil, p. 67.  Quanto ao destino de toda esta gente, é significativa a colocação que CINTRA faz: "(...) Os sudaneses, particularmente os Iorubás ficaram mais na Bahia e no Nordeste, os daomeanos, particularmente os Gêges, foram para o Maranhão. Há também representantes na Bahia e em Pernambuco. Os Haussas, malês e mandingas, espalhados pelo Nordeste, foram os principais responsáveis pelos Quilombos; os bantos espalhados um pouco pelo Brasil inteiro, são mais numerosos no Rio De Janeiro, em Minas Gerais e nos Estados do Sul".
[2]Idem, Ibidem, p. 32
[3]Cf. BASTIDE, R. Op. cit.,p. 68.
[4]Id. Ibid., p. 69.
[5]Cf. Id. Ibid., p. 69; nos parece interessanteapresentaralgumas datas de fundação. O nosso autor, fundamentando-se nas pesquisas feitas por P. VERGER, mostra que a casa da Minas de São Luís do Maranhão tenha sido provavelmente fundada em 1796 por membros perseguidos da família real do Daomé; e Nunes Pereira soube por MãeAndréia que sua “casa” havia sido fundada por “contrabandos”, isto é, por negros trazidos clandestinamente depois de 1815 e que tinham sido libertados quando de suachegada ao Brasil. Sabemos, de outro lado, que o Candomblé de EngenhoVelho em Salvador foi fundado por duas sacerdotisas da família de Xangô, trazidas como escravas para esta cidade no começo do séculoXlX.

domingo, 27 de março de 2016

MASHAHIDI WA BWANA MFUFUKA


Kutafakari kuhusu Matendo 10: 34a. 37-43; Yoh 20,1-9

Tufurahi sote, kwa sababu hii ni siku Mungu aliyotufanyia! Tangazo la ufufuko wa Yesu ni mwaliko wa furaha, yaani furaha ya maisha ambayo yanayashinda mauti, furaha ya upendo ambao unaushinda uchungu na kutenda kama rafiki katika safari ya watu wapya wa Mungu, kuyaimarisha matumaini yao. Wanafunzi wa kwanza walipotangaza tukio hilo, walianza kutokana na maisha ya binadamu ya Yesu, aliyetiwa na Mungu kwa kazi ya wokovu wa binadamu. Kwao Wanafunzi wa kwanza uzoefu pamoja na Yesu ulikuwa umejaa maana. Kutokana na uzoefu huu wanaweza kutenda kama mashahidi. Kama alama ya wema wa Mungu, maana ya maisha ya Yesu ilikuwa kuwatendea watu mema. Nalo tendo lake liliwezekana kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye. Alitaka kuupendekeza uzoefu wa maana kabisa kwa wale ambao watakuwa mashahidi wake.
Kama Kristu hakuwa amefufuka, je, mahubiri ya wanafunzi wake yangekuwa na maana gani? Hakika yangekuwa tupu, yaani, pasipo maana. Mbele ya kifo kisicho na haki cha mwalimu wao walikufa moyo sana, lakini ushindi wa uhai unawapa maana mpya ya kuishi. Basi, ujumbe wa wanafunzi unatafsiri pia ushindi dhidi ya hali ya hofu ambayo waliishi baada ya kifo cha Mwalimu, yaani kikundi chao kilivunjika. Kwa wanafunzi ilikuwa vigumu sana kuendelea kwa safari baada ya kukatishwa tamaa kwao kuhusu  mwalimu Yesu ambaye walitarajia mengi, hasa awe mfalme mwenye nguvu. Lakini maisha yao yalibadilishwa kabisa baada ya kuona ushahidi wazi wa ufufuko wa Mwalimu, yaani kaburi tupu, vitambaa alivyolalia, na baadaye Yeye mwenyewe akajionyesha kwao; kisha waliacha hofu, wakiitoa nafasi kwa imani na kuchukua maisha ya mashahidi. Ni njia kamili ambayo tunapaswa kuishi ili tuwe wanafunzi wa Yesu wa kweli.     
Lakini tunapaswa kutambua kwamba safari hii ya imani ya wanamume ilisababishwa na mwanamke, yaani Maria Magdalena ambaye alikuwa na upendeleo wa kuwa ni wa kwanza kuenda kaburini, kukutana na Yesu na kupewa habari kwa ajili ya Mitume. Walipaswa kuiacha picha ya Yesu kama alivyokuwa alipoteseka, amekufa na kuzika ili wakaribishe njia mpya ya Yesu aliye mzima na anayeishi kati yao kwa njia mpya na tofauti kabisa. “Magdalena ni yule ambaye Yesu aliponya kwa kufukuza mashetani saba ndani yake. Katika Biblia namba saba inamaanisha ukamilifu. Basi, Maria Magdalena alikuwa ameponywa na Yesu kikamilifu.” Katika Kristo Maria alikuta upendo wa kweli ambao alikuwa ameutafuta sana kwa muda mrefu. Mwanamke huyo alijifunza jinsi ya kuwa mwanafunzi wa kweli, akimfuata Yesu wakati wa mahubiri, tangu Galilaya hadi msalabani. Kwa hivyo anastahili cheo cha “Mtume wa Mitume wa Yesu.” 

Baada ya kupokea habari kuhusu udidimizi wa mwili wa Kristo, wanafunzi wawili wakaenda mbio kuelekea kwenye kaburi, yaani Petro na mwanafunzi aliyependwa na Yesu (Yohane). Walikimbia pamoja, lakini huyo mwanafunzi alifika kwanza. Kama hivi ni upendo ambao unapaswa kufika kwanza katika kila kitu. Yule anayependa anapata kuwa wa kwanza katika maonyesho ya upendo na imani. Anaweza kutambua mabadiliko kandokando yake, kwa sababu yeye mwenyewe ana moyo ambao umebadilishwa na uzoefu wa kujiona kupendwa. Uzoefu wa ufufuko ni uzoefu wa upendo wa Mungu anayetuchagua tumtumikie na kutubadilisha kabisa ili tuwe mashahidi wa upendo unaozaa uzima, unatufanya kushinda vikwazo, hofu na mashaka na kutufanya kuishi kwa hamu uzoefu wa ndugu. Kuhusu Petro, ndiye alama ya mapigano daima ya mtu ili aweze kushinda kuchoka kwa kazi; ni alama pia ya mtu ambaye anajaribiwa kufa moyo, lakini anashinda kwa sababu ya uzoefu mkubwa wa kujitolea ulio muhimu kwa kuwaongoza na kuwashauri wengine. Ushuhuda wetu kama mashahidi wa Bwana Mfufuka uwe kama ilivyotokea na wao. Tumsifu Bwana Mfufuka!  

Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah

sábado, 26 de março de 2016

TUFURAHI KWA SABABU BWANA WETU AMEFUFUKA


Kutafakari Kuhusu Lk 24, 1-12

Ndugu na dada zangu, tufurahi kwa sababu Bwana Yesu amefufuka! Amefufuka ili akae pamoja nasi na kutufanya watu wapya. Kufufuka kwake Yesu ni tendo la ajabu la Mungu na maana ya kweli ya maisha yetu. Kupitia Kristo Mfufuka uumbaji wote unafanyika upya. Mwanga wake unayaangaza magiza ya maisha yetu na kuufungua upeo wa macho wa uzima wa milele. Sikukuu hii ya ufufuko wa Bwana wetu inatualika kuishi furaha kubwa, yaani, furaha ya maisha ambayo yanayashinda mauti, furaha ya upendo ambao unaushinda uchungu. Yesu ni uwepo hai miongoni mwa wanadamu, kufufua matumaini yao. Ni nafasi nzuri ya kufanya upya ahadi yetu ya wanafunzi na kushinda hofu ambayo inatuzuia kuwa mashahidi wa kweli.
Masomo ya Agano la Kale yanatuonyesha mambo makuu ya Mungu ulimwenguni na hasa katika safari ya watu wake. Kupitia matendo ya Uumbaji, Agano, Ukombozi na Maisha mapya yeye anajifunua kuwa Mungu wa uhai na kutaka daima furaha kubwa kwa kila mmoja wa viumbe vyake. Furaha hii inatokana na uhai wa Utatu Mtakatifu, aliye ushirika wa upendo. Tangu uumbaji ametushirikisha katika uhai wake mwenyewe. Basi, uumbaji ulikuwa mwaliko wa tushiriki katika ushirika wa uhai na upendo wa Mungu. Matendo yake katika Agano la Kale hayakuwa kitu kingine ila kuwandaa watu wake kwa kuzaliwa upya kupitia ufufuko wa Mwanawe pekee. Hali hii ni wazi sana kupitia ubatizo ulio uzoefu wa ufufuko kwa njia maalum, kutufanya kuumba tena na kuchukuliwa na Mungu kama watoto wake tulio warithi pamoja na Mwanawe. Kwa maneno mengine, tunakufa na Yesu, kuzika hali zee ya wenye dhambi na kufufuka tena naye kama watu wamefanyika wapya kabisa.  
Katika injili, wanawake, yaani Mariamu Magdalene, na Yoana, na Mariamu mamaye Yakobo na wanawake wengine walikuwa na upendeleo wa kuwa mashahidi wa kwanza wa ufufuko wa Bwana. Waliamuka mapema asubuhi, kwa sababu waliimarishwa na upendo wa kweli kwa Yesu; upendo huu unawaongoza kumtafuta. Kwa muda, uzoefu wa ufufuko kwao ulikuwa kaburi tupu na tangazo la malaika, lakini ishara mbili zilitosha ili waweze kuishi tena furaha ya uwepo wa Bwana wao. Yesu hakuwako kaburini kwa sababu huko ni mahali pa wafu; naye ndiye alifufuka na kuishi milele. Habari njema hii ya furaha kubwa inapaswa kutangazwa. Baada ya tukio lililoonekana kuwa ushinde, yaani, kifo chake, Yesu aliruhusu uwezo wa kuziona ishara za ushindi wake kwanza kwa wale ambao walikuwa waathirika wa ubaguzi katika jamii na, kwa hivyo, walijiona waliotenganishwa. Kwa kweli kupitia chaguo hilo Yesu alithibitisha pendekezo lake la muda mpya, mawazo mapya na uhusiano mpya kati ya watu. kwa kufanya kazi muhimu ya tangazo la ufufuko, wanawake walipaswa kushinda hofu na mawazo kutoka jamii kuhusu wao wenyewe. Walikuwa na uhakika kwamba Mtu aliyechagua aliwaandamana nao daima.  

Kama wanawake na wanafunzi wa kwanza wengine, tunaalikwa kufanya uzoefu wa Bwana Mfufuka. Uzoefu huu siku hizi unaidai imani zaidi kuliko kugusa. Neno lake na ushuhuda wa wale waliotutangulia unatusaidia kushinda hofu na kuchukua ahadi ya kuwa mashahidi pia. Kupitia msaada wa wengine na msukumo wa Mungu tunaweza kushinda hofu zetu zote na kukubali kwa shauku utume wa kutangaza habari njema ya ufufuko wa Yesu. Yeye yupo miongoni mwetu na ndani yetu ili atufanye vyombo vya huruma yake. Uzoefu wa wanawake unatusaidia kumtafuta Bwana Mfufuka kwa mioyo yetu yote na kuruhusu kuongozwa na mwanga wake ili uwepo wetu uwe ufanisi katika mahali popote tuendapo. Uzoefu wa kumtafuta Bwana unatuwezesha kushinda vikwazo njiani, kutufanya mashahidi wa upendo ambao unauzaa uhai. Bwana Mfufuka anaishi miongoni mwetu! Tunapaswa kuwa macho ili tumtambue katika hali nyingi zinazoyahusisha maisha yetu. Yeye atupatie ujasiri ili tuwe mashahidi wake wa kweli.

Fr Ndega
mapitio na marekebisho: Sara

quinta-feira, 24 de março de 2016

MATESO YA KRISTU NI ALAMA KUU YA MSHIKAMANO WAKE KWA AJILI YA WANAOTESEKA


Kutafakari kutoka Yoh 18-19

Kanisa zima linakumbuka siku ya leo mateso na kifo cha Kristu, mume wake na mkombozi wa ulimwengu. Kuadhimisha mateso na kifo cha Yesu ni kuadhimisha upendo wake mkuu hadi matokeo upeo. Yesu ni zawadi kuu ya Mungu na alama ya upendo wake kwa dunia nzima, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee... Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye (Yo 3,16-17).” Mwana wa Mungu aliuleta wokovu ulimwenguni akafa msalabani na akiyashinda mauti kupitia ufufuko wake mtukufu. Kwa hivyo kupitia msalaba mtakatifu tunakumbuka si mateso na kifo cha Kristu tu, lakini pia ushindi wake na wokovu wetu. 

Somo la kwanza linatujulisha historia ya mateso makali ya mtumishi wa Bwana, ambaye ni mwaminifu kwa kazi aliyomkabidhi Bwana wake, akichukua dhambi za watu wote. Mtumishi huyu aliuleta ukombozi, akibeba huzuni ya wote, akijiruhusu kujeruhiwa na makosa na maovu yao. Ingawa yeye alidhulumiwa na kuteswa, akaweza kuyasalimisha maisha yake mikononi mwa Mungu, akiuhakikisha msamaha kwa wenye dhambi wote. Mafanikio ya kazi yake hayakutokana na uwezo wa binadamu, lakini yalitokana na nguvu ya Mungu aliye kimbilio lake na ulinzi wake. Wakristo hutafsiri kazi ya mtumishi huyo kama mfano na utabiri wa maisha na kazi ya  Kristu ambaye alichagua kuwa mtumishi, akikubali fedheha na mateso ili afanye mapenzi ya Mungu.

Simulizi ya mateso, kulingana na mwinjilisti Yohana, inatusaidia kutafakari kwa njia ya ndani kuhusu maana ya mateso na kifo chake Yesu. Tunaalikwa kutambua katika kusulubiwa alama kuu ya upendo wa Mwana wa Mungu, aliyeutoa uhai wake kwa ajili ya wanadamu wenye dhambi. Mateso yake ni mwanzo wa ushindi wake juu ya mauti, kufufua matumaini ya watu. Kwake hakuna upendo mkuu isipokuwa kuyatoa maisha kwa wema wa marafiki. Tabia hii inatusaidia kutafakari kuhusu hali ngumu ya mateso ya binadamu na kuamini kwamba Mungu hawaachi wale wanaoteseka. Kama binadamu, Yesu hakutaka kuteseka, lakini alikubali hiyo kwa sababu alitaka kuwapea wanaoteseka nafasi ya kuishi maisha mapya. Mateso ya Kristu yanatufundisha jinsi ya kukaribisha mateso kwa utulivu na kuwa uwepo ufanisi maishani mwa watu wanaoteseka.

Mateso na kifo cha Kristu hakiwezi kufahamiwa kama kilichotakwa na Mungu, lakini kilikuwa matokeo ya ahadi yake ya kinabii na ufunuo wa upendo na huruma ya Mungu kwa namna ya ajabu. Kristo “alikufa kwa sababu ya uaminifu wake kwa mpango wa Mungu mpaka upeo”. Yesu hakufa kama asiye na matumaini na huzuni zake hazikumaanisha kutelekezwa na Mungu. Ushuhuda kuhusu hili ni kujisalimisha kwake mikononi mwa Baba yake, kulingana na toleo la Luka, yaani, “Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu (Lk 23,46)”. Ishara yake kuu ya upendo ilikubaliwa na Baba, aliyejibu kwa ufufuko mtukufu, akiyapa maisha ya binadamu maana kabisa. Katika kifo chake vifo vyote vinashindwa na katika ufufuko wake matumaini yote yanafufuka. Nasi tunashiriki katika mwendo huu. Kwa hivyo Mt. Paulo asema, “Kila wakati tumekuwa tukichukuwa mwilini mwetu kifo cha Kristo, ili uhai wake Yesu udhihirike katika miili yetu (2Cor 4,10).”  

Pamoja na mateso ya Mwana tunatafakari pia huruma ya Mama yake ambaye anajua jinsi ya kupenda na pia jinsi ya kuteseka kwa ajili ya mtu anayependa. Maria alichukua katika moyo wake huzuni zote za mwanawe. Kama hii ilitimizwa unabii wa Simeoni katika Hekalu: "Upanga utachoma roho yako mwenyewe". Kama mwanafunzi wa Kwanza na Mwaminifu wa Mwanawe, Maria alichukua jukumu lake hadi matokeo upeo, akibaki kusimama mbele ya msalaba. Pamoja naye, wanawake wengine watatu na mwanafunzi aliyependwa na Yesu wanabaki pia. Upendo tu unaweza kueleza maana ya nguvu na uvumilivu wa wanawake katika mazingira haya magumu. Kweli, walijifunza kumfuata Yesu kwa njia ya ukarimu na kujisalimisha kabisa. Ishara ya upendo ya Kristo na safari ya kumfuata kutoka kwa wanawake ni mwaliko wa kujitolea kwetu, kuibeba misalaba yetu na kumfuata Yesu kulingana na matarajio yake kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu mzima.  

Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sara

quarta-feira, 23 de março de 2016

EKARISTI NA UTUMISHI WA NDUGU


Kutafakari kutoka Yoh 13, 1-15

Liturujia ya Kikristu ina asili katika ibada ya Wayahudi, ambayo ina kama umuhimu Jahveh, Mungu aliyeamua kufanya historia na watu wake, akianzisha agano la upendo nao. Tukio hili lilitanguliwa na tendo la nguvu, likiweka huru mababu wa Wayahudi kutoka utumwa wa Misri. Watu hao walipokea kutoka kwa Mungu uongozi ili kusherehekea nafasi maalum ya uhuru wao kwa kula mwana-kondoo wa mwaka mmoja. Hatimaye, walizipokea Amri jangwani Sinai kama alama ya agano aliloanzisha Mungu nao. Hao walikuwa Watu wa Mungu. Tangu kipindi hiki na kuendelea Wayahudi wameadhimisha uhuru wao kila mwaka kwa kula hasa kile mababu wao walikuwa wamekula katika usiku maarufu wa uhuru. Mkutano huu unaitwa Mlo wa Pasaka.
Kutumia Ibada sawa, Yesu alianzisha Ibada mpya, ni kwamba, Mlo wa Ekaristi, akitangaza kwa Wafuasi wake ukombozi kamili ambao ulikuwa ukija na kwamba alitamani kwa shauku kushiriki na rafiki zake. Katika karamu hii kwa hali ya familia na matarajio makuu, Yesu alijitoa kama chakula, akitangulia kwa njia ya ibada kile kitatokea naye msalabani. Kupitia ishara na mifano alionyesha maana ya kujisalimisha huria na kwamba pia lazima kuwa tabia ya maisha ya wafuasi wake. Kwa hiyo, aliwaosha wafuasi miguu, akiwapa mfano wa unyenyekevu na utupu (Kenosis), akiunganisha milele adhimisho la Mwili na Damu yake na utumishi wa udugu. Wale ambao wataendeleza kazi ya Mwalimu ulimwenguni, wanapaswa kuchukua tabia sawa ya utumishi, mawazo mapya na uhusiano mpya.
Yesu ni Mwalimu ambaye anatumikia na anapenda hadi matokeo upeo. Akijua kwamba upendo unahitaji uwepo, yeye aliendeleza uwepo wake ulimwenguni kupitia Ekaristi. Ekaristi ni maonyesho ya kujisalimisha kwake Kristu huria na alama ya upendo inayokuwa utumishi. Hali hii una uhusiano na utumishi wa ukuhani, ishara ya Kristu Mchungaji ambaye anaendelea kuongoza kundi lake. Kupitia ubatizo tuna ukuhani pamoja na waminifu wengine kushiriki katika mwili mmoja wa Kristu, kuchukua jukumu la kuendeleza kujenga mwili huo kwa upendo. Ekaristi ina maana tu ikiwa ni maonyesho ya upendo wa udugu na wale tu ambao wanapenda wanaweza kutumikia. Wale tu ambao wanapenda kweli  wanaweza kuendelea hadi matokeo upeo. Upendo tu unazaa ushirikiano na “vitu tu vinavyofanywa na upendo vina uimara”.
Hili ni fumbo la imani yetu:  ukweli wa ndani na utajiri tunaoalikuwa kukaribisha kwa upendo na unyenyekevu na kumjua Mungu kama yeye ndiye. Ukweli huu unaitwa Fumbo la Paska, ambalo linajumuisha mateso, kifo na ufufuko wa Yesu. Yesu alianzisha Ekaristi katika Alhamisi Kuu, kutoa mwili na damu yake  kwa kula na kunywa wakati wa Karamu ya Mwisho. Ijumaa Kuu tena akatupa mwili wake na damu yake, lakini wakati huu kwa kufa msalabani. Hii ni sadaka ya kweli kwa njia mbili tofauti. Siku hizi mbili, Alhamisi Kuu na Ijumaa Kuu zinahusiana kwa karibu.  Katika Jumapili ya Pasaka ushindi wake juu ya mauti unakamilika na maisha mapya yanapatikana kwa wote.
Basi, Ekaristi ni adhimisho ya mateso, kifo na ufufuko wa Yesu. Uwepo wake ni hai, una nguvu, nao ndio ufanisi, yaani, una uwezo wa kutoa matokeo. Katika Ekaristi Yesu hutenda kazi na kusababisha mabadiliko katika maisha yetu. Kama hii, kwa Ekaristi tunabadilishwa kamili katika fumbo tunaloadhimisha, kukubali ukweli wa Fumbo la pasaka kama “Pasaka ya Kristu katika Pasaka yetu na Pasaka yetu katika Pasaka ya Kristo”. Hivyo Baada ya kila adhimisho ya Ekaristi tuna changamoto ya kurudi shughuli zetu za kila siku kama mashahidi wa Kristo anayetoa maisha yake kwa upendo ili watu wote wawe na uzima wa milele.

Ee Yesu, tunakushukuru kwa utajiri wa Ekaristi. Tunakushukuru pia kwa uzoefu wa udugu ambao tunaishi katika kila misa takatifu ambayo sisi huadhimisha. Tunasadiki kwamba uwepo wako ni wa kweli na ufanisi kati yetu na tunataka kufanya upya ahadi ya kuishi urafiki mwafaka na wenye nguvu nawe, kutumikia wengine kwa ukarimu. Mfano wako wa unyenyekevu na utupu utufanye kugundua ukuu wa utumishi wa ndugu. Amina.

Fr Ndega

terça-feira, 22 de março de 2016

AFRICANOS Y EUROPEOS, UN ENCUENTRO DRAMÁTICO


En mi articulo anterior, había afirmado que la campaña del colonizador por la esclavitud de indígenas fue algo que no dio mucho resultado. Los factores para eso están en dicho artículo. En continueidad, vamos a ver que el colonizador va a apelar a la esclavitud de los africanos. La propia experiencia en Portugal confirma la eficacia en el trabajo deseado, por haber invadido Africa desde 1400[1]. El autor D. Freitas hace una pequeña comparación entre estos dos tipos de esclavos: el indígena y el africano:
“Los indios se mostraban incorregiblemente inadaptables al trabajo esclavo. Cuando no escapaban para vivir de nuevo en la mata bajo la ley de sus instintos naturales, morían en masa, segados por el mortífero contagio con las enfermedades europeas. Ya el africano, como era físicamente robusto, poseía una tradición de vida sedentaria (…) configurando por esto la solución práctica y necesaria del problema de la fuerza de trabajo para la empresa colonizadora”[2].
Alrededor de los siglos XIV y XV, encontramos una Africa dividida en tribus – algunos libros utilizan el termino reinos – que competían entre sí, en busca de mayores espacios territoriales. Algunas tribus eran de cultura primitiva, otras de cultura más avanzada; de estas, algunas estaban formadas culturalmente sobre la influencia del islamismo. Una de las ventajas indiscutibles que los negros del siglo XV tenían sobre los europeos era la superioridad técnica en el uso de los metales. Los africanos poseían sociedades basadas en la posesión de la tierra y practicaban con intensidad el trabajo colectivo[3].
“Los pueblos del oeste africano tenían indudablemente, sistemas agrícolas bien desenvueltos. Los Daomés tenían hasta un sistema de plantación. Todos esos pueblos – Daomés, Ashante, Yoruba, para mencionar algunos del comercio cuidadosamente reglamentado; existía gran número de ligas artesanales, y comenzaba a surgir una estructura de clase”[4].
Según J. Chiavenato, ese pueblo, en particular, los del oeste africano, tenían una agricultura más avanzada en sus técnicas que Portugal. El autor continúa todavía destacando la capacidad cultural de los yoruba y su religión musulmana, recordando, por lo tanto, que estos pueblos se desenvolverían independientemente del contacto con los musulmanes[5] .
La llegada de las poderosas naciones europeas, bien armadas y ávidas de lucro, contribuyó para aumentar algunas rivalidades, alimentó las guerras tribales, sobre todo, abaló fuertemente esos conjuntos sociales y culturales e hizo desaparecer ciertas tradiciones. Hasta la familia ampliada, que era compuesta de la esposa o de las esposas, el padre, los hijos, los primos y que resistió hasta los primeros tiempos de la colonización, por ahora, tuvo que romperse[6]. En vista a la dilatación de la fe y del imperio, no importaba lo que se hacía. En este sentido, la ejecución del programa fue bien maquiavélica. Delante de los abusos y crueldades, algunos papas incluso intentaron protestar. Entre ellos encontramos al Papa Pio II, en 1462 y Pablo III, en la Bula Sublimis Deum, de 1537[7]. En tanto, en Brasil, la realidad era otra, pues de tan estructural que estaba la esclavitud por aquí, el Padre Manuel de la Nóbrega llega a “escribir al rey pidiendo entra otras cosas necesarias (vacas, instrumentos de hierro y una dotación), también… algunos esclavos de Guiné… para hacer mantenimientos…”[8]
Un gran cuestionamiento al  que no se tiene respuesta exacta es: ¿cuánto negros fueron traídos a Brasil? La dificultad en afirmar, con certeza, es debido a la quema de documentos oficiales sobre el trafico negrero[9], a fin de borrar de la historia esta página que, para Brasil representa una vergüenza, y que simplemente es necesario olvidar, pues somos el último país que suprimió la esclavitud. Aún así, existe la estimativa de más de cuatro millones de negros, lo que corresponde al 40% del total de América[10]. Calmon va a hablar de 6 millones, mientras que Taunay reduce a 3.600.000[11]. Ya Pandira Calógeras, citado por R. Cintra, evalúa en más de quince millones, basándose en cálculos sobre la capacidad de las embarcaciones y de los viajes marítimos. No se sabe, en verdad, cuantos fueron; lo que si se sabe es que no todos llegaban vivos[12]. Continuaremos este asunto en el próximo articulo.
Modjumbá  axé!
Fr Ndega
Traducion: Nomade de Dios



[1] Cf.  CINTRA, R. Candomblé e Umbanda. São Paulo: Paulinas, 1985, p. 27.
[2] FREITAS, D. O escravismo brasileiro. Porto Alegre: Mercado Aberto, 2. ed. 1982, p. 23.
[3] Cf. Id. Ibid., p. 49.
[4] Id. Ibid. , p. 49.
[5] Id. Ibid. p. 20.
[6] Cf.  MATTOSO, K. Q. Ser escravo no Brasil. São Paulo: Brasiliense, 3ª ed., 1990, p. 27.
[7] Cf. em CINTRA R.. Op. cit., p. 23);  R. BASTIDE, vai dizer que a Igreja lutou contra a escravidão do índio, mas aceitou a do negro.  (Cf. BASTIDE, R. As religiões africanas no Brasil. 3 ed., São Paulo: Biblioteca Pioneira de Ciências Sociais, 1989,  p. 77).
[8]BEOZZO, J. O. A escravidão que fez e explica o Brasil. Revista Vida Pastoral, São Paulo: Paulinos, ano XXIX - n. 138, janeiro-fevereiro de 1988, p.18.
[9] Cf.  CINTRA, R. Op. cit.,  p. 23); Cf. também  BASTIDE, R., Op. cit., p. 50.
10 Cf. TOLEDO, R. P de.  Á sombra da escravidão. Veja, São Paulo: Ed. Abril, ed 1444, Ano 29 – n20, 15 de maio de 1996 p. 53.
11 Cf. BASTIDE, R. Religiões africanas no Brasil., p. 50-52.
12 Cf. CINTRA. R. Candomblé e Umbanda., p. 24;



domingo, 20 de março de 2016

SHANGWE KWA BWANA MSHINDI NI TANGAZO LA USHINDI WAKE


Isa 50, 4-7; Phil 2, 6-11; Lk 22, 14-23,56

    Kupitia liturjia hii tumeanza wiki kuu ya mwaka iliyo wiki kuu ya imani yetu. Kama inavyotokea katika sherehe hii, hivyo wiki hii takatifu inatualika kushiriki katika matukio ya mwisho ya utume wa Yesu wa binafsi. “Mwana wa Adamu atateseka na kufa, lakini atafufuka”. Mateso ya Mwana kwa upendo ni nafasi ya kumtukuza Baba yake na kuwaokoa ndugu zake. Tunaposhiriki katika mateso yake tena tutashiriki katika utukufu wake, kwa sababu mapenzi yake ni kwamba wale wanaomfuata washiriki katika furaha yake ya milele. Jumapili ya matawi inatufanya kusherehekea, kwa utangulizi, uhakika wa utukufu huu kwa sababu tunamshagilia Bwana mshindi anayeenda Yerusalemu bila hofu, hata akiijua nia mbaya ya adui zake. Mji huu ni maarufu kwa sababu ya upinzani kinyume na Mungu kupitia mauaji ya manabii wengi. Hata Yesu alipoongea kuhusu kazi yake ya nabii alitaja kuwa sio vizuri kwamba nabii akufe nje ya Yerusalemu. Kama wayahudi ambao walisherehekea ushindi kwa kushika matawi ya mtende, tunatumia matawi haya kama ishara ya utayari wetu wa kumfuata Yesu kwa uamuzi sawa naye mpaka upeo.

     Yesu anaanza safari yake ya kujisalimisha kama aliyebarikiwa kwa jina la Bwana. Matukio yaliyotangulia mateso na kifo chake yanadhihirisha yale yaliyokuwa sehemu ya uchaguzi wake wakati wote wa kazi yake, yaani, uamuzi wa kwenda Yerusalemu, wa kupanda mwana-punda, wa kuruhusu watu wamshangilie na wa kutaja neno mawe kama uenezi wa sifa kwa Mungu anayefanya upya uumbaji wote kupitia kujisalimisha kwake Mwanae. Somo la nabii Isaya linaitaongelea kazi ambayo Yesu alichukua kama mtumishi wa Bwana anayejua sana utambulisho wake kama mwenye ulimi wa wafundishwao. Yeye ana masikio makini kwa neno la Bwana na anaweza kusema daima maneno ya faraja kwa wale ambao wana mahitaji mengi; anajua pia kwamba kila kitu alichopokea kwa Baba kinalenga kutangaza ukaribu na wokovu wake Mungu. Tena anajua kwamba hatembei peke yake kwa sababu Bwana wake yu mwaminifu wala hawaachi wale ambao wanamtumainia.

       Njia iliyochaguliwa na Yesu awaokoe wanadamu ni njia isiyotarajiwa na mawazo ya kawaida. Hali hii inatajwa katika waraka wa wafilipi unaojulikana kama “injili ya tano”. Andiko hili linaonyesha njia ya utukufu wa Kristo kulingana na mapenzi ya Mungu. Hii ilikuwa njia ya utupu. Kwa kweli ingawa akawa sawa na Mungu, hakuona hali hii kuwa ni kitu cha kushikamana, lakini alipendelea kuacha utukufu na kuchukua hali ya binadamu na kama mtumishi alitii mpaka mauti, yaani, mauti msalabani. Yeye alijifanya maskini ili atufanye tajiri kupitia utajiri wake. Alikataa heshima kama hii ipasavyo kwa Mungu illi apate heshima kwa maskini na wasio na nguvu katika jamii.


        Mwendo wa utupu wa Kristo ni mwendo ambao tunahitaji kupita ili maisha yetu yaweze kumpendeza Mungu ambaye ana mazoea ya kuwashusha wakuu na kuwapandisha wadogo. Hii ni njia ya uanafunzi wa kweli kama alivyosema Yesu mwenyewe kwa wafuasi wake, yaani, “yeyote anayetaka kuwa wa kwanza akawe wa mwisho; na mtu anayetaka kuwa mkuu akawe mtumishi wa wote. Hakuna njia nyinigine ili tuweze kufikia matarajio ya Mungu kama wanafunzi wa Mwanae ambaye alikuja sio kutumikiwa bali kutumikia na kuutoa uhai wake kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu. Nao utumishi wake umejaa maana kwa sababu ulifanyika kwa upendo. tujifunze kujisalimisha kutokana na kielelezo cha Yesu ambaye hata katika wakati wa huzuni na mateso, aliilenga imani yake katika tendo la riziki ya Mungu: “Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu”. Hili lazima kuwa kilio cha roho zetu ili tujihakikishie kwamba Mungu hawezi kutuacha wala kunyamaza mbele ya kinachotokea nasi. Mbele ya kufa kwake Yesu, jibu la Mungu ni ufufuko wa Mwanawe. Mfano wake ni mwaliko wa tujitolee kwa ajili ya wengine, kufananisha maisha yetu na njia yake ya kuishi na kutumikia.   

Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sara

segunda-feira, 14 de março de 2016

ESCLAVITUD INDIGENA EN BRASIL COLONIAL, PRELUDIO DE LA ESCLAVITUD DE LOS PUEBLOS NEGROS.



Quiero presentar en este blog, diversos artículos a partir de mi investigación NEGRITUD Y EXPERIENCIA DE DIOS. Deseo iniciar trayendo la cuestión indígena que, ad experimentum, no tuvo el resultado esperado, dejando a los negros y negras, la responsabilidad involuntaria del mantenimiento del estado de “preguicite” del colonizador deshumano.

Es sabido, en un sentido general, que la experiencia de Dios en la vida de diferentes personas y pueblos es determinante para un crecimiento más humano, en que la otredad no es una posibilidad, sino una realidad. Tratándose de comunidades afro, esta experiencia posee una evidencia notable por asumir características culturales, sin las cuales no tendría sentido su existencia. Sobre esta relación, ya se ha escrito y discutido mucho, pero todavía hay muchas preguntas sin respuestas. El objetivo aquí es descubrir y profundizar algunas manifestaciones afro, buscando relacionar el caminar de las diferentes comunidades que encuentran en la experiencia de los Sagrado, una manera de mantener vivas las raíces. Mi referencia son las culturas más influyentes: bantú e nagô (yoruba).

Habiendo sido invadida América, a fines del siglo XV (1492) y, en particular, Brasil, a inicios del siglo XVI (1500), la sed de riquezas, la ganancia económica y la falta de respeto cultural llevaran a los colonizadores a explorar el vasto interior brasileño, organizando expediciones, asentamientos, en busca de metales preciosos. Lo que en un primer momento, estas tierras les podían ofrecer eran unas pocas mercaderías, algunas plantas medicinales, o pau-brasil, papagayos multicolores y monitos divertidos; nativos sin ropa había a millares, pero nada de eso despertó, enseguida, gran interés de exploración. Algunos lo definían como tierra extraña, inhóspita, cubierta de vastas florestas y poblada por indios antropófagos. Con el avance de otras naciones europeas y temiendo perder todo eso, Portugal inicia, a partir de 1530, una devastación, que tienes sus restos hasta el día de hoy[1] .

Era necesario, más allá de lo que la tierra ofrecía, introducir nuevas culturas como la del azúcar, cuyo consumo comenzaba a crecer en Europa, y la agricultura comercial. Para desenvolver esta actividad, era necesario mano de obra y población local. Debido a las guerras, pestes y epidemias anteriores que causaron muchas pérdidas de personal, Portugal no disponía de gente, “casi sin cultura”, que viniese para trabajar en esta tierra, sin saber lo que le podría suceder en este nuevo Mundo. Apela entonces, para la esclavitud del nativo (indígena). Ya era hábito en Portugal, pues así sucedió con los descendientes de árabes conquistados y los prisioneros de guerra de África del Norte. Se estima que en 1550, 10% de la población de Lisboa eran esclavos negros. En cuanto a la población, era necesario que la corona portuguesa ofreciese considerables privilegios para atraer colonos blancos. Por eso la costa de Brasil fue dividida en doce sectores, por líneas paralelas, y toda la extensión del país, a partir del litoral y hasta el misterio de su interior, fue dada, a titulo de hereditario, a capitanes, que a cambio de dispensa de transporte e instalación recibían derecho de soberanía[2] sobre el territorio otorgado.

Necesitando de mano de obra para sus proyectos grandiosos, y viendo tanta “gente de la tierra” a disposición, parecía mucho más fácil al colonizador portugués implementar la esclavitud en Brasil. Al principio traía buenos resultados[3], pero no los esperados, pues, ávidos de lucro como eran, querían siempre más. Entonces comenzaron a  surgir algunas dificultades: “La primera y la más importante de ellas fue el estado de civilización aborigen, habituado al nomadismo y una cultura itinerante que no se podía someter al trabajo sedentario del mismo modo que a la disciplina, al método y al rigor de una vida organizada. La segunda fue la reacción de la Iglesia Católica contra la esclavitud del indio que impedía su cristianización”.[4]

Aún así, el resultado de todo esto ya es de nuestro conocimiento. Datos revelan que, de millones de indígenas, tenemos poco más de ciento cincuenta mil. Estos que restan están acorralados, esperando que hagan algo por ellos. Proyectos como este siempre fueron parte de la historia de nuestra Nación Brasil, en que algunos tienen que pagar, de la forma más maquiavélica posible, por las mayordomías y ganancias de los otros. Los cuadros se repiten principalmente en sectores empresariales y gubernamentales de nuestra sociedad. ¿Hasta cuándo?

Modjumbá axé!
Pe. Degaaxé
Traducion: Nomade de Dios




[1] Cf. BASTIDE, R. Religiones Africanas en el Brasil, ps. 47-50
[2] Cf. Id. Ibid. p. 48;
[3] Cf. Id. Ibid., p. 49
[4] Id. Ibid., ps. 49s.

domingo, 13 de março de 2016

MTU ANATHAMINI ZAIDI KULIKO MAKOSA YAKE


Kutafakari kutoka Yoh 8, 1-11

       Andiko hili linatuletea tukio la mwanamke ambaye alifumaniwa katika uzinzi na kutusaidia kutafakari kuhusu jambo muhimu katika sheria ya wayahudi na maisha ya binadamu, yaani, hali ya umoja kati ya mume na mke kupitia ndoa. Umoja huu ulichukuliwa kama mtakatifu na kubarikiwa na Mungu tangu mwanzo. Katika mpango wake wanapaswa “kuwa mwili mmoja”. Lengo la umoja huu ni kwa kuzaa watoto na kupata utimilifu kwa wanandoa. Mungu alijua kwamba umoja huu ulihitaji kulindwa na, kwa hivyo, alianzisha kama amri “Usizini na Usitamani mwanamke asiye na wako”. Alisema hivyo kwa sababu yeye ni wa kwanza anayejua kwamba bila umoja binadamu haishi vyema na bila uaminifu umoja hauwezekani.
    Wale ambao walimleta mwanamke huyo mbele ya Yesu walitenda dhambi ya udhalimu mara mbili. Ya kwanza ni kwa sababu uzinzi unawezekana tu kati ya watu wawili. Ikiwa washitaki hao walimleta mwanamke peke yake kumshitaki na kumwachia huru mwanamme, walitenda dhidi ya sheria wenyewe. Kulingana na kitabu cha Walawi (Wal 20, 10), “kama mwanamume akizini na mke wa jirani yake, ni lazima wote wawili wauawe.” Ya pili ni kwa sababu hao washitaki walijua kwamba wao wenyewe hawakuwa wasafi. Walikuwa wasio na haki na hata walitaka kwamba Yesu atende kulingana na matendo yao. Ishara zilizofanywa na Yesu zilikuwa nafasi ya watafakari kwamba maisha ya mtu ni bora kuliko sheria; ya kutafakari pia kuhusu umuhimu wa mwanamke katika jamii; tena kuhusu haja ya uhusiano wa kweli na Mungu pia na wengine, na kumpea mtu nafasi moja zaidi kama vile Mungu anavyofanya kwa ajili ya wenye dhambi, kwa sababu hataki kifu cha mwenye dhambi bali atubu na kupata uzima. Katika mwendo huu, Yesu aliamsha dhamiri zao kuhusu udhalimu wa ubaguzi akiwafanya kufikiri na kutenda tofauti. Kupitia njia ya Yesu ya kutenda, moyoni mwao waliweza kukiri kwamba wao pia walikuwa wadhambi na hivyo walihitaji msamaha wa Mungu. Kama matokeo, wote walisamehewa na Yesu, yaani, washitaki na mshitakiwa kwa sababu Yesu anataka kujenga jamii mpya kupitia uhusiano mpya kati ya watu.
       Kuhusu mwanamke huyo, alibaki katika mahali kamili, yaani, katikati; lakini sio kama rejeo ya hukumu bali kama rejeo ya huruma. Yeyote anayekutana na Kristo anakutana na huruma ya Mungu na kupata nafasi ya kuishi maisha mapya. Mwanamke yule alikuwa amekufa na amefufuka, alikuwa amepotea na ameonekana. “Enenda zako; wala usitende dhambi tena”. Yesu hakuja kuadhibu bali kuokoa; kwa hivyo maneno na ishara zake zinamsaidia mwanamke achukue ahadi ya kuishi tofauti, kulingana na mapenzi ya Mungu. Maneno haya yanaonyesha kwamba Yesu hakubali udhalimu wala hapitishi kosa lolote. Anatarajia mabadiliko ya maisha. Kwake mtu anathamini zaidi kuliko makosa yake. Kuhusu hili, yako maneno ya Mt. Yohana Calabria yanayosema, “tunapaswa kuyachukia makosa ya mtu, lakini tunapaswa kumpenda mtu huyu kwa sababu ndiye ndugu yetu”. Upendo unatufanya kusadiki kwamba inawezekana kubadilisha hali mbaya kuwa hali nzuri. Tunapompenda mtu tunausadiki uwezo wake wa kushinda udhaifu na mwelekeo mbaya wa maisha yake. Kwa upande wa mtu aliyependwa hii ni nafasi ya kuonyesha kwamba anaweza kujibadilisha.

    Maneno ya Yesu yalikuwa faraja na kusababisha kitendo tofauti. Ishara zake zilikuwa makaribisho na kusababisha mabadiliko ya maisha. Ikiwa maneno na ishara zetu zinatokana na msukumo wa Mungu zinapaswa kusababisha matokeo kama hayo. Mwanamke huyo ni mfano wa watu ambao wanahukumiwa na kuadhibiwa miongoni mwetu. Mawe ni alama ya maneno na ishara ambazo hazijatumika kwa kujenga ndugu, zikitia moyo na kuimarisha imani yao, bali zimewazuia kuamini kwamba wanaweza kubadilisha maisha yao na kufikia matarajio ya Mungu. Sisi pia ni kama mwanamke huyo. Baada ya kila mkutano na Bwana, hasa kupitia sakramenti, tunaalikwa kuiacha dhambi na kuchukua mwelekeo mpya wa kuishi. Neema ya Mungu ituongoze.

Fr Ndega 
Mapitio na marekebisho: Sara

domingo, 6 de março de 2016

THE MERCIFUL FATHER AND OUR SACRAMENTAL FREQUENCE


Reflection from  Lk 15, 1-3. 11-32


            We have accompanied the proclamation of the parable of the merciful father. This parable shows the special way of God dealing with the sinners. This special way was revealed by Jesus, whom is called also “the face of the mercy of God, because everything in him speaks about mercy.” He narrated this parable because in that context, where he lived, some people considered themselves worthy of the salvation of God more than others, because their fidelity to the law. They decided to separate the people in two different groups, such as, the righteous ones and the sinner ones. This authority doesn’t come from God because the criterion used is the discrimination. In this case, it becomes very difficult to create fraternity and to enter in communion with God, who welcomes everybody in order to save all. As incarnation of God’s mercy, Jesus had very clear option: “This man welcomes the sinners and even eats with them” The identity of Jesus was very clear even for the ones who made opposition to him. So, Jesus not only spoke about God’s mercy, but also used gestures of welcome, confirming the finality of his mission and the authenticity of his teaching. In fact, many taxi collectors, prostitutes and others rejected by society felt themselves welcomed by Jesus and transformed by the meeting with God’s mercy. It is in this context that we can understand this parable narrated by Jesus.    
   
            According to Jesus, God is a Father who has different children and shares his gifts in equal way with all. He loves all and wants that all should feel in family, participating of his joy as Father. In this family he offers care and protection so that all should have good reasons to remain always with him. When somebody decides acting against him and to stay very far from him, it is not because he/she doesn’t feel loved by the Father, but it is because he/she feels free. Like this is the experience of the love of the Father: it is expression of his generosity and gratuity, which generates freedom. We feel ourselves very far from him when we act against him, that is, when we commit sin. God feels himself abandoned and betrayed, but doesn’t stop loving. For that we feel remorse and also attracted to recover the experience of communion which we had lost because the sin. The experience of the mercy of God helps us to know him better and to use the right discernment in our decisions. We celebrate this reality through the Sacrament of Reconciliation, that is, reconciliation with God, with others and with ourselves.

In the Sacrament of Reconciliation we celebrate the experience of return to the communion with God, as “the prodigal son” did. This experience allows us to participate in the sacrament of Eucharist, nourishing the communion with God and others with more intensity. God makes us to feel really touched and embraced by his love of Father.  The own God tell us through the prophet Jeremiah: “You are my dearest son/daughter, the child I love best. Whenever I mention your name, I think of you with love (Jr 31, 20).” There is another personality in this parable who neither feel himself son - because according to his own words, he is employee - nor brother, because ignores his brother, the young one. He prevents the full joy of the Father and the fullness of the feast. Being reconciled with God and with others are necessary conditions so that our Eucharistic experience should be true. We are in intense communion with God if we share his feelings in relating to others. The Eucharist will never reach its total finality while others continue being ignored in our midst.         

O Lord, we thank you for your word and the invitation to live in intense communion with you, who is so good. We are ashamed, because we have sinned, turning away from you, but bring us back; we are ready to return to you, Lord our God. Through the Holy Eucharist and Penance we want to intensify our relationship with you and to become instruments of your love and mercy. Increase our faith and revive our hope so that we may be motivated in our mission.  Amen.

Fr Ndega

MUNGU ANAFURAHI TUNAPOMRUDIA YEYE


Kutafakari kuhusu Lk 15, 1-3.11-32

Sura ya kumi na tano ya toleo la Luka ni maarufu miongoni mwa mifano ya Yesu. Hii inaitwa sura ya Mifano ya huruma. Tuna mifano mitatu (Kondoo aliyepotea: 4-7; Sarafu iliyopotea: 8-10; Mwana mpotevu: 11-32). Lakini siku ya leo liturjia inatujulisha moja peke yake, yaani, mfano wa mwana mpotevu. Mfano huu unaonyesha tabia ya huruma ya Mungu kuhusu wenye dhambi na furaha ya kukutana tena na yule ambaye alipotea. Kwa kufahamu nia ya Yesu kwa uhusiano na mifano hii tunahitaji kutafakari kwanza kuhusu mazingira ambayo Yesu aliishi. Katika muktadha huo, baadhi ya watu walijiona wanastahili upendo wa Mungu zaidi kwa ajili ya uaminifu wao kwa Sheria. Walichukua mamlaka ya kuwatenganisha watu, wakiwapanga kama wema au wabaya. Mamlaka haya hayatoki kwa Mungu kwa sababu kipimo ni ubaguzi. Walisahau kwamba mbele ya Mungu watu wote ni sawa. Mungu habagui katika upendo wake. Kwa upande wake watoza ushuru na wenye dhambi ni watoto wake sawa na Mafarisayo na Waandishi wa Sheria. Ikiwa hao wanaweza kuzaa ndugu, tena wanaweza kuishi katika ushirika na Mungu, anayekaribisha kila mtu ili awaokoe wote.
      Ingawa yako matukio mengi katika Agano la Kale, ambayo yanaonyesha njia maalum ya Mungu ya kutenda, ni “katika Yesu Kristo kwamba huruma ya Mungu imepata kuwa hai na yenye kuonekana, na hata ilifikia kilele chake katika Yeye... Yesu ni uso wa huruma ya Baba. Kila kitu ndani yake kinaongelea huruma. Hakuna chochote kwake kinachopungukiwa na huruma (Baba Mt Francisco).”  Kama alama ya huruma ya Mungu, Yesu ana chaguo wazi sana, yaani, “Mwanamume huyu anawakaribisha wenye dhambi naye hata anakula nao”. Maneno haya yalisemwa na wale waliompinga Yesu. Kwa kweli, Yesu aliongea kuhusu huruma ya Mungu si kwa maneno tu, bali “kwa neno lake, matendo yake na kwa nafsi yake yote.” Yeye alitumia ishara nyingi za makaribisho, akithibitisha lengo la ujumbe wake na ukweli wa mafundisho yake. Kwa kweli, watozaushuru wengi, makahaba na wengine waliokataliwa na jamii walijihisi wamekaribishwa na Yesu na, kwa hivyo, kubadilishwa kwa mkutano na huruma ya Mungu.
      Ingawa katika mfano wa mwana mpotevu tunasikia tukio la kijana mdogo na hisia za kijana mkubwa, lakini ni baba wa vijana hawa wawili ndiye aliye mhusika mkuu wakati wote. Uhusiano wake wa mapendo kwa vijana wake, ambao wote ni wapotevu kwa njia tofauti ndio umuhimu wa tukio hili. Kulingana na Yesu, baba huyo ni kama Mungu ambaye ana watoto tofauti na kushiriki nao zawadi zake kwa njia sawa. Yeye anawapenda wote na kutaka kwamba watu wote wajihisi wakiwa katika familia, kushiriki kwa furaha yake kama Baba. Katika familia hii anautoa utunzaji na ulinzi ili wawe na maana nzuri ili kubaki naye daima. Wakati yeyote anaamua kutenda kinyume naye na kubaki mbali sana naye, sio kwa maana mtu huyo hajihisi kupendwa, bali ni kwa sababu anajiona mwenye uhuru. Kama huu ni uzoefu wa upendo wa Baba: huu ni huria na kuuzaa uhuru. Sisi pia tunahisi mbali sana na Mungu wakati sisi hutenda kinyume naye, yaani, tunapomkosea. Yeye anajihisi ameachwa na kusalitiwa, lakini haachi kutupenda. Kama yule baba, Mungu anashughulika sana na maisha yetu. Anakuja kututafuta ili kutupa sisi ulinzi na utunzaji wake. Kwa hivyo tunahisi majuto na kivutio ya kuishi tena uzoefu wa ushirika tumeopoteza. Ingawa mara niyingi tunakataa utambulisho wetu wa wana, kupitia dhambi zetu, Mungu haukatai utambulisho wake wa Baba kamwe.

      Katika mfano huu yuko pia mwana mkubwa ambaye hajihisi mwana kwa sababu anajiona kuwa ni mfanyakazi wala anajihisi ndugu, kwa sababu anatojali ndugu yake mdogo. Tabia ya huyo mwana mkubwa inaizuia furaha kamili ya Baba na ukamilifu wa sikukuu. Kumrudia Mungu ni maana ya furaha kubwa kwake. Lakini furaha yake haiwezekani kuwa kabisa ikiwa hatushiriki katika hisia zake kuhusu wengine. Hataki kwamba tuwe wivu kuhusu njia yake ya kupenda; anataka kwamba tutende kama yeye alivyo. Kwa hivyo Yesu alisema, “Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo.” Upatanisho na wengine ni kipimo ili uhusiano wetu na Mungu uwe kweli. Hii ni njia ya kweli ya toba iliyo mwendo wa muda mrefu na huanza mioyoni mwetu. Kupitia Ekaristi hii, turuhusu kuguswa na huruma ya Mungu ili tuweze kuwa vyombo vya huruma hii kwa wale wanaohitaji msamaha wetu.

Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sara