Kutafakari kuhusu Ex 3, 1-8a. 13-15; 1Kor
10,1-6.10-12; Lk 13,1-9
Somo la kwanza linaongea kwamba huko mlimani Horebu Mungu
anatokea kwa Musa na kuudhihirisha utambulisho wake kama Mungu aliye yupo katika
historia ya ubinadamu daima. Yeye ana unyeti mbele ya hali ya mateso ya watu
wake na kuamua kuwaokoa kutokana na utumwa wa Misri, kuwaongoza kwa nchi njema,
yaani nafasi ya kuishi maisha mapya. Katika mwendo huu Mungu anatumia Musa kama
chombo cha huruma yake na Musa anakubali kuiacha mipango yake ya maisha na
kuchukua mpango wa Mungu ili ukombozi wa Mungu ufikie Watu wake kubadilisha
hali ya mauti kuwa hali ya uzima. Katika somo la pili, Mt Paulo anawakumbusha
Wakristo wa Korinto kwamba miongoni mwa wale waliopitia huruma na ukarimu wa
Mungu wengi waliangamizwa jangwani kwa sababu maisha yao hayakumpendeza Mungu. Hili
ni onyo kwa sisi sote ya kuishi kulingana na zawadi za kiroho tumepokea kwa
sababu yule ambaye anatoa zawadi hizi antarajia mabadiliko ya maisha yetu kama
matokeo ya tendo lake la ukarimu.
Katika injili, baadhi ya watu alimwendea Yesu na
kumpasha habari kuhusu ukatili wa Pilato kwa ajili ya Wagalilaya. Kama
ilivyotokea mara zingine, hii ni nafasi zaidi aliyotumia Yesu awafundishe na
kuwaalika kwa toba. Kwanza kabisa alipaswa kusahihisha mawazo fulani yapo
miongoni mwao kwamba watu ambao wanateseka ni kwa sababu ya dhambi walizotenda.
Kulingana na mawazo haya, mateso yote yalionekana kama matokeo ya dhambi. Kama
hii ilikuwa hali ya wagonjwa wote katika mazingira ya Yesu. Kwa hivyo, kabla ya
kufanya muujiza wowote alimwambia mgonjwa, “Nakuondolea dhambi zako”. Alisema
hivyo kama ushuhuda kwa jamii nzima ambayo pia ilipaswa kupona na hali ya
ubaguzi kuhusu wagonjwa. Kulingana na Yesu njia hii ya kufikiri ni hatari kwa
sababu inaweza kuwa kikwazo kwa watu kukataa kuwasaidia wale walio katika
mateso. Kutokuwa na ahadi kwa ajili yao na kutofautiana kunayaongeza zaidi
mateso yao.
Kwake Yesu, mateso hayatokani na Mungu, bali yanaweza
kuwa ni nafasi kwa mtu kumrudia Mungu kwa moyo wote na kumtukuza. Inawezekana
pia kuwa ni nafasi ya jumuiya nzima kujifunza juu ya huruma waipokeayo kutoka
kwa Mungu ambayo inapaswa kuwaongoza waonyeshe upendo na huruma hasa kwa wale
wanaoteseka. Sisi ni kama wagonjwa kwa sababu ya uzoefu wa dhambi. Wakati Yesu
aliposimulia mfano kuhusu mti bila rutuba, alitaka kuongea kuhusu uvumilivu na
huruma ya Mungu kwa ajili ya wanadamu wote. Kama ilivyotokea na mti ule, Mungu
anataka kutupa nafasi moja zaidi ili tuweze kuzaa matunda anayotarajia. Mungu
hutupa muda ya kukomaa na kuishi maisha bora. Subira ya Mungu ni nafasi kwetu
ya kupata wokovu kwa njia ya toba.
Kwaresima ni nafasi tupewayo na Mungu ya kuacha dhambi
na kumrudia Mungu kwa uthabiti zaidi. Tunaweza kufanya hivyo kwa kuacha
kuwatenga watu katika makundi tofauti ya walio wema na walio dhambi na kuwaona
wote kama walio dhambi wanaohitaji msamaha wa Mungu. Kulingana na Yesu, Mungu
anatarajia maisha yetu yaweze kumpendeza kupitia matunda mazuri. Tumepokea
nafasi nyingi ili tufikie lengo hili. Katika uzoefu wa watu wa biblia yeye
anajifunua kama mkombozi na mwenye uvumilivu mbele ya hali ya udhaifu wa watu. Kwa
upande wa Mungu uvumilivu na huruma; kwa upande wetu ushujaa na toba. Kama
ilivyotokea na Musa, Mungu anatualika kwa uzoefu tofauti ambao unalenga
kutubadilisha kuwa katika vyombo vya huruma yake.
Fr Ndega
Mapitio: Sara