Kutafakari kuhusu Mk 16, 15-18
Hii ni nafasi maalum ya kuonyesha upendo wetu
kwa kazi ya Mungu kama alivyo Mt. Paulo. Mtu huyo alikuwa mcha Mungu na kushughulika
sana kwa ajili ya dini yake. Kupitia njia yake ya
kuishi sheria kwa uaminifu, aliamini kwamba akawa anampendeza Mungu. Kwa jina
la Mungu aliwatesesha watu wengi. Kwa sababu ya matendo ya Sauli, aliye na
ushabiki, watu wengi walikufa. Moyo wa ibada na nguvu zake zote zilitumika kwa
kutangaza Mungu wa mauti na uwepo wake ulisababisha hofu na mateso kwa watu.
Hakika hakuwa akitumikia Mungu wa kweli. Basi ufunuo wa Yesu wakati wa safari
ya Sauli ulikuwa maonyesho ya kwamba kujitoa kwake hakumpendeza Mungu. Sauli alipaswa kugundua tena maana
ya maisha na kazi yake. Alikuwa aliyetesesha na sasa ndiye aliyeteseka. Kulingana
na maneno yake mwenyewe, tunaweza kusema kwamba Sauli alizaliwa tena akiwa
mjumbe mkuu wa Yesu kwa mataifa yote. Alipata kufanya kazi zaidi kuliko mitume
wengine wote kwa ajili ya Yesu. Huu ni mwendo wa toba ambao sisi sote
tunaalikwa kuchukua.
Uwezo wa
Paulo wa kuongea na kufundisha unatoka kwa Yesu ambaye ana maneno ya neema na
nguvu. Ingawa yeye ni yule peke yake kwa mamlaka ya kutangaza wokovu wa Mungu,
alishiriki mamlaka hii na Paulo na wanafunzi wengine wake ili watumikie watu,
wakidhamini maisha mengi kwa wote. Kulingana na injili ya siku ya leo, kipimo kwa
kuishi maisha mengi haya ni imani, ambayo huja kwetu kupitia hali ya ubatizo. Wanafunzi walitumwa kama wajumbe wa habari njema
kwa viumbe vyote kwa sababu injili haina mpaka. Maisha mapya ambayo Yesu
alileta kupitia ufufuko wake yanafikia uumbaji mzima. Yesu alikuwa amewaahidia
kuandamana na safari yao mpaka upeo. Ingawa uwepo wa mwili wa Yesu usionekana
tena, Roho wake yupo daima katika safari ya mitume na maisha ya wote
waliomwamini umeyafanya maneno yao ufanisi kupitia ishara nyingi na matendo mengi
mazuri.
Utumishi
kwa watu ambao ni wa Mungu ni utumishi kwa Mungu. Kwa hivyo ni lazima kuwa
macho kuepuka kuyatumia mamlaka kwa njia mbaya. Mbele yao Yesu alitenda kwa
mamlaka kinyume na nguvu za maovu ambayo yaliwapooza watu, yakiwazuia kushiriki
kikamilifu katika jamii. Aliwadai njia ya unyenyekevu wa maisha kupitia
kujinyima na kujitolea hasa kwa ajili ya wagonjwa, kutangaza ukaribu wa ufalme
wa Mungu. Ni jukumu lao kutangaza ufalme wa Mungu, lakini ikiwa watu
hawalikubali pendekezo lao si jukumu lao tena. Wanafunzi wa Yesu wanapaswa
kutenda kama mwalimu wao alivyo, yaani kuheshimu uhuru wa wengine. Ufalme wa
Yesu ni ufalme wa uhuru na amani, wa haki na msamaha. Habari ya ufalme huu
inatokana na ukarimu wa Mungu. Nayo ni njema maana ni matokeo ya bure,
kuusaidia uhuru.
kama
wanafunzi wapya wa Yesu sisi pia tunahitaji mkutano wa kuongoka/toba kama
ilivyotokea na mt. Paulo. Kwanza kabisa, tunapaswa kuwa macho kwa msukumo wa
Mungu na kuzifuata nyayo za Yesu kuchukua njia yake ya maisha, yaani njia ya
unyenyekevu. Hatuwezi kufikiri kwa hakika kwamba tunampendeza Mungu wala kwamba
hatuhitaji mwendo wa toba. Mwendo huu ni wa muda mrefu sana. Ingawa Paulo
alikuwa mtume mkuu aliruhusu kusaidiwa na marafiki wengi, yaani Luka, Marko,
Barnabas, Timotheo, Tito na viongozi wengine wa jumuiya ambazo alitengeneza. Kulingana
na uzoefu wake mafanikio ya utume wetu yanawezekana ikiwa uzoefu wa kutenda
pamoja unapata kushinda uzoefu wa kutenda mtu akiwa peke yake, kusaidiana
katika jumuiya na kwa manufaa wa jumuiya. Tunaweza kutangaza halisi ukaribu wa
ufalme kupitia utumishi wetu wa ukarimu na bure, kuheshimu wale waliotenda
tofauti nasi. Baadhi ya ugumu katika safari yetu tunapaswa kukabili kupitia
roho ya sala na toba daima. Ukarimu na utayari wetu uwe vyombo ambavyo Mungu aweze
kutumia kuwajalia wote maisha mengi.
Fr Ndega
Mapitio: Sara