Kutafakari kutoka YbS. 3,2-6, 12-14; Wak 3, 12-21; Lk 2:
41-52
Tunasherehekea Jumapili ya Familia Takatifu Yesu,
Maria na Yosefu. Sikukuu hii inatukumbusha kwanza kuhusu mkutano wa wachungaji
na Maria Yusufu, na Mtoto mchanga amelala horini. Hakika kutembelea huku kulisababisha
kutafakari kubwa mioyoni mwa Maria. Sikukuu hii inataja pia ushiriki wa familia
takatifu katika hekalu ya Yerusalemu. Tukio hili liliwasaidia wazazi wa mtoto
Yesu kujua kidogo zaidi kuhusu hazina kubwa ambayo aliwakabidhi Mungu. Hasa kwa
upande wa Mama Maria hii ilikuwa nafasi maalum ya kutafakari kuhusu mpango wa
Mungu. Hii ni nafasi pia ya kutafakari kusuhu maana ya familia za binadamu na
mahitaji ya kuishi thamani nyingi za Familia takatifu ambazo zinampendeza Mungu
na kuisaidia jamii.
Ushiriki wa Familia takatifu (Yesu, Maria na Yosefu)
katika jumuiya yake ni kielelezo/hamasa kwa Ushiriki wetu katika jumuiya/kanisa.
Kulingana na andiko hili la Luka ushiriki wa familia
hii ulikuwa desturi. Miongoni mwa Wayahudi kila Myahudi anapaswa kwenda
Yerusalemu angalau mara moja kwa mwaka kwa sababu ya sherehe ya pasaka pamoja
na wengine. Yesu alikuwa kijana wa umri wa miaka kumi na miwili, na ilionekana alipotea
hekaluni, lakini kwa kweli yeye alijikuta mwenyewe kwa sababu inampendeza kuhusishwa
na kushughulika kuhusu hali ya Baba yake. Hali hii ilikuwa ngumu sana kwa Maria
na Yosufu wafahamu. Hasa Mariamu, ingawa hakufahamu hali hii, alikuwa na tabia
nzuri ya kuweka moyoni mwake matukio muhimu, akitafakari na kutafsiri ili atende
mapenzi ya Mungu. Maria alikuwa makini sana kwa matendo ya Mungu katika
historia ya watu wake. Moyo wake ulikuwa makao ya Mungu, mahali pa kwanza,
ambapo Yesu alizaliwa. Kwa hivyo haikuwa ngumu sana kwa yeye kuishi ushirika wa
ndani na moyo wa mwana wake Yesu.
Sehemu
ya mwisho ya injili hii inasema kwamba Yesu alirudi Nazareti pamoja na wazazi
wake na alikuwa akiwatii. Hii ilikuwa njia yake ya kuishi ambayo inampendeza
Mungu na ni mfano kwa wanadamu wote. Kuhusu hayo somo la kwanza pia linathibitisha
umuhimu wa uhusiano wa ndani kati ya wana wa familia, kufikiria watoto kama
baraka kwa wazazi. kuwatii na kuwaheshimu wazazi kunayahusu mapenzi ya Mungu na
kunazivutia baraka nyingi kwa familia. Kulingana na Mt Paulo mifano ya Kristo
ya utii na upendo lazima kuwa kipimo cha uhusiano kati ya wanandoa kwa sababu
thamani hizi zinampendeza Mungu na zinawahamasisha watoto katika safari yao.
Familia inampedeza Mungu ambaye, tangu mwanzo, alimpanga binadamu kwa mfano
wake, akisema: “Si vizuri huyu mwanamume kuwa peke yake. Nitamfanyia msaidizi
wa kumfaa”. Basi Uumbaji wa wanadamu ulikuwa mwaliko kwa kuishi katika familia.
Ni mapenzi ya Mungu waweze kuwa pamoja, kupendana na kusaidiana. Kwa nini
familia ni muhimu sana? Kwa sababu familia ni msingi wa uzoefu wa binadamu; Kwa
sababu pasipo familia uimara wa jamii hauwezekani. Kwa sababu bila familia
mawasiliano ya thamani ya jamii kizazi kwa kizazi hayawezekani. Kwa maana
uhusiano kati ya wazazi na watoto unawafanya kuwajibika na kukomaa zaidi. Kwa
sababu bora kuliko chochote, familia inayaridhisha mahitaji ya hisia na
fizikia/mwili, kuwapa watoto utoto salama na imara.
Yesu
anapenda sana kushiriki katika maisha ya familia. Yeye alizaliwa katika familia
moja na kutokana na makao ya Nazareti alibariki familia zote za ulimwengu.
Uwepo wake ni ufanisi ili familia zetu
zifikie lengo lao kulingana na utambulisho asili. Kumheshimu Maria, mama yake,
kunatusaidia kutambua uwepo na matendo ya Mwanawe katika familia ili ishinde
hofu, changamoto taabu na majaribio mengi, hasa majaribio ya uzinzi na talaka. Jukumu
la Yosefu pia ni chanzo cha msukumo kwa akina baba wote ili wawe ishara za
ulinzi na utunzaji wa Mungu, kuzaa hali ya usalama na utulivu katika familia. Uwepo
wa Yesu, Maria na Yusufu unaiweka wakfu familia ukiifanya takatifu. Familia ni
mahali pa kumcha Mungu; basi, ni mahali patakatifu. Baba Mt Yohane Paulo II
alisema kwamba ni lazima kuiokoa familia. Nasi tunaweza kufanya hivyo hasa kwa
kuziheshimu na kuzisaidia thamani ambazo zinaishiwa katika familia na
zinatufanya binadamu wa kweli.
Fr Ndega
Mapitio: Sara