Kutafakari kuhusu Lk 21, 25-28, 34-36
Tumeanza wakati mpya katika liturujia ya kanisa uitwao Majilio. Wakati huu unayahamasisha matumaini yetu
katika matarajio ya Kuja kwake Bwana
mara ya pili katika mwisho wa nyakati na unakumbuka pia Kuja kwake kwa kwanza,
kutuandaa tusherehekee sikukuu ya
kuzaliwa kwake katika Krismasi.
Basi, Liturujia ya msimu huu ni mwaliko kwa kukesha ili
tutambue na kuzikaribisha ishara
za uwepo wa Bwana katika hali
yetu ya kila siku. Ni mwaliko
pia kwa shukrani
kwa sababu Bwana anakuja
daima kukutana na sisi, kutupa wokovu
wake. Matukio yote makuu
yanahitaji maandalizi mazuri ili yaweze kusherehekewa
vizuri. Kama hii ni Majilio kwa uhusiano na tukio kubwa la Krismasi.
Mwanzoni mwa sura ya kumi
na tatu ya injili ya Luka Yesu anaongea kuhusu uharibifu wa Yerusalemu. Ufunuo
huu uliwahamasisha baadhi ya wanafunzi wake wamwulize swali kuhusu ishara gani,
siku na saa gani ya uharibifu huu. Yesu anatumia nafasi hii kutabiri kuhusu
mambo mengi akiiandaa mioyo ya wafuasi wake kwa wakati ujao. Aliwaambia kuhusu
ishara nyingi mbinguni, taabu, mateso, dhiki kuu na kuja kwake, kulingana na
unabii wa Danieli, yaani, juu ya mawingu ya angani mwenye nguvu na utukufu
mwingi. Kanisa katoliki hutafsiri tukio hili kama kuja kwake Yesu mara ya Pili
ili kuwahukumu wazima na wafu. Hiyo ndiyo imani yetu ambayo sisi hutangaza kila
jumapili. Kuhusu siku na saa hii hakuna mtu ajuaye. Hii ni
sehemu ya mpango wa hekima na wema
wa Baba. Kwa hivyo huu ni pia mwaliko kwa
kukesha.
Ingawa uharibifu wa mji
wa Yerusalemu ulitokea katika mwaka wa 70 B.K., nia ya Yesu haikuwa kuwajulisha
kuhusu tukio hili, bali kuhusu matokeo ya tukio hili katika maisha ya wafuasi
wake. Alitabiri kwamba “nguvu za mbingu zitatikiswa” akifikiria imani na
ushuhuda wa wanafunzi wake kama nguvu za mbingu zipo ulimwenguni. Wanafunzi wa
Yesu wataishi kipindi cha machafuko na watajaribiwa kuiacha imani katika Kristo
na kukata tamaa kuhusu utambulisho wao wa wanafunzi kwa sababu ya matusi,
majaribio, matatizo na mateso mengi. Ilionekana kwamba walikuwa peke yao mbele
ya machafuko hayo yote. Lakini Yesu mwenyewe alikuwa amewaahidi uwepo wake daima
kupitia maneno haya, “mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamiliifu wa
dahari.” Maneno haya ni mwaliko kwa ushuhuda na kusali kama njia ya kukesha. Hao
wana jukumu la kuendelea utume wa Mwalimu, wakiwa makini kwa ishara za kuja
kwake ili akutane nao na kuwatuza kwa maana ya uaminifu wao.
Andiko hili linatuambia kwamba Kristo ni mshindi na ujio wake unaanzisha wakati
mpya anaoshiriki na wanafunzi wote wanaobaki wamesimama na kuinua vichwa vyao
kupitia imani na ushuhuda kwa uaminifu. Tunapaswa kuishi imani yetu ya kikristo
kwa uhusiano na kila kitu ambacho kinatokea kandokando yetu. Jamii inatarajia
imani yenye maana na iwe jibu kwa hali iliyopo na binadamu anayoiishi. Je, imani yetu ni gani? “Je, tena wakristo
wanapaswa kuwa na tabia gani wakati wa mazingira magumu? Kama aliwaambia wafuasi wake wa zamani, Yesu
anatuhakikishia kuwa mazingira magumu ni sehemu ya safari ya wale ambao
wanamfuata katika nyakati zote, lakini Yeye anatukumbusha pia kwamba ni katika
machafuko haya ya dunia hii tunapojiandaa kukutana naye mwishoni mwa maisha
yetu binafsi hapa duniani. Kwa hivyo kila hatua ya safari yetu ni maandalizi
kwa mkutano wa mwisho na Bwana wetu.
Liturjia linataka
kuimarisha imani yetu na kufufua tumaini letu kwa tendo la wokovu wa Mungu
ndiye mkuu katika nyakati zote, zilizopita na zijazo. Hali hii inatualika
kuishi wito wetu wa wafuasi kwa uaminifu katika nyakati zote pia, hata wakati
wa mateso makali. Baada ya machafuko yote tutakuwa washindi pamoja na Bwana
wetu mshindi. Kulingana na mithali fulani, “hakuna usiku hata wa muda mrefu
pasipo mapambazuko”. Basi, kwa wale wanaomfuata Kristo, mazingira magumu si
ishara za mwisho wa nyakati bali ni wakati mpya, wakati wa kuishi wito wetu kwa
shauku zaidi, furaha na tumaini, kuushuhudia kwa uaminifu uwepo wa Bwana
miongoni mwetu. Anakuja kwa upendo na kutuokoa. Tukaribishe ishara za nyakati
kama msaada tutambue uwepo wa Bwana na kuishi mafundisho yake kwa njia mpya.
Fr Ndega
Mapitio: Sara