quinta-feira, 29 de outubro de 2015

MTAKATIFU YOHANA CALABRIA NA WAGONJWA

Kutafakari kuhusu Is 49: 14-15; Mt 6: 24-34

        Liturujia inatujulisha mifano miwili yenye nguvu kuhusu Mungu. Katika Somo la kwanza Mungu analinganishwa kwa mama na katika injili Mungu analinganishwa kwa baba. Mungu anawapenda watu wote na hamsahau yeyote wa wana wake. Yeye anakijali kila kitu ambacho wana wake wanahitaji. Mtakatifu Yohana Calabria aliishi kwa uzoefu huu kwa mkazo na aliweza kuushuhudia kwa wengine. 

   Watu wa Israeli walikuwa watumwa katika Babeli na wakajihisi walioachwa na kusahauliwa. Nabii Isaya aliwasaidia kutambua kwamba Mungu alikuwapo miongoni mwao na hakuwasahau. Yeye ni Mungu mpole ambaye anawapenda na kuwalinda watu wake zaidi kuliko mama ampendaye mtoto wake anyonyaye. Basi, uwepo wake ni dhamana ya utunzaji na ulinzi. Katika injili Yesu anawafundisha wanafunzi wake kuhusu umuhimu zaidi wa maisha. Anaongea kuhusu hatari ya utajiri na miliki yote ambayo inaweza kumshika mtu hivi hata asiweze kifikiria mambo yanayomhusu Mungu. Nia kuu ya Yesu ni kuongea kuhusu Mungu kama Baba aliye na wasiwasi kwa utunzaji wa upendo kwa kila kitu. Baba huyu anatarajia jibu la ukarimu kutoka kwa wanadamu ambao wana thamani zaidi kuliko viumbe vingine vyote. Kuwa mwanafunzi wa kweli wa Yesu ni kutafuta kwanza Ufalme wa Mungu Baba na haki yake kama rejea ya maisha. Kwa maneno mengine, anatualika kujisalimisha mikononi mwa Mungu ambaye anayajua mahitaji yetu na yuko tayari daima kutusaidia.

       Injili hii inafikiriwa msingi wa kiroho ya Mt. Yohane Calabria kwa sababu kupitia injili hii aliufanya ugunduzi mkubwa. Aligundua jinsi ya kuishi kwa njia halisi ubaba wa Mungu na kuwa ishara ya riziki yake kwa watu. Kutokana na andiko hili alichukua mistari 33 kama ahadi kwake: “Mtafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake; na hayo yote mtapewa kwa ziada.” Kulingana naye “Injili anatuongelea kwamba Mungu ni Baba, anatujali zaidi kuliko ndege wa angani na maua ya mashamba hata atatujalia kile ambacho tunahitaji kwa chakula na kwa mavazi, lakini tunapaswa kuutafuta kwanza Ufalme wake na haki yake”. Mt Calabria alifahamu kwamba ililazimu kuifufua imani duniani kwa Mungu Baba wa wanadamu wote, kupitia kujisalimisha kabisa kwa Riziki yake. Kwake imani kweli na asili inafikiria Mungu si kama Muumba na Bwana tu, bali kwanza kama Baba”. Mungu ni Baba, hutujali na wote ambao tunawapenda; macho yake ni makini sana kwa kila kitu na kila kitu kinapangwa na kuongozwa na hekima, nguvu na wema wake pasipo mwisho.

      Mt. Yohana Calabria alikuwa mtu mwenye unyeti mno kuuhusu ugumu na mateso ya wengine.  Aliweza kuweka matendoni maneno yake kuhusu wema na utunzaji wa Mungu katika Riziki yake, akisema, “Riziki ni Mama mpole ambaye hupatia kila kitu kwa wema wetu, hata kwa wema wetu mkubwa. Tunapaswa kuhisi tumebebwa kwa mikono yake ya mama”. Yohana Calabria aliamini katika ukweli huo na hata aliyapanga maisha na kazi zake zote kulingana na hali hii. Kama ishara ya utunzaji wa Mungu alikuwa na unyeti mkubwa kwa uhusiano na wagonjwa. Alimwona Kristo mwenyewe katika walio wagonjwa. Alifikiria mateso ya wagonjwa kama thamani na msaada mkubwa kwa mtume wa kanisa. Aliwahamasisha na kuwaonya wagonjwa kuukaribisha ugonjwa na mateso kwa utulivu na sala. magonjwa kwao yana maana kwa wokovu wao na wokovu ulimwenguni. Kristu mwenyewe aliwapenda wagonjwa na wakati wa maisha yake alikwenda mara nyingi kuwatembelea na kuwaponya. Kwa njia Mtakatifu Yohana Calabria, tumwombe Mungu kwa ajili ya wagonjwa wote, hasa kwa hawa ndugu zetu wapo katika misa hii ili neema ya Mungu iimarishe imani na nguvu zao. Maisha yenu yawe ushuhuda wa wema wa Mungu kwa sisi sote.

Fr Ndega
Mapitio: Sara

IMANI YA KWELI NA HALISI

Kutafakari kutoka Mk 10, 46-52

     Yeriko ni mmoja miongoni mwa miji ya zamani ulimwenguni. Hii nieneo ya baadhi ya matukio makuu ya biblia; hata katika muda wa Musa ilikuwa tayari kuongelewa kuhusu mji huu. Tukumbuke “kuzingirwa na kuchukuliwa kwa Yeriko” na Waisraeli katika wakati wa Yoshua (Yoshua 6, 1-27). Tukumbuke pia Zakayo; mabadiliko ya maisha yake yalitokea katika Yeriko. Mji huu ni karibu na mto Yordano na Yesu alipita mahali huko mara nyingi. Andiko siku ya leo linaongea kuhusu mkutano wa Yesu na kipofu Bartimayo, aliyeketi kando ya barabara ya mji. Hakika alikuisha amesikia kuhusu Yesu na alitaka sana nafasi ili kukutana naye. Lakini hakujua kwamba Yesu pia alitaka kukutana naye ili kumwongozea njia mpya ya kuishi. Kisha, nafasi imefika! Shauku ya kipofu ilikuwa kubwa sana kwamba hakuna kitu au mtu kumfanya  anyamaze.

    Kilio cha kipofu ni kilio cha kila binadamu mwenye dhamiri kuhusu udhaifu wake na mahitaji ya huruma ya Mungu. Kipofu ni ishara ya kivuo dhahiri cha ndugu zetu wengi. Ni nafasi ya kutambua kwamba watu wengi wanaanguka au wameachwa barabarani. Wanapaza sauti kwa huruma na kwa nafasi kwa sababu wanaamini kwamba wale ambao wanajiita wafuasi wa Yesu wanaweza kusikiliza sauti yao na kuwatendea mema. Yesu alisikia si kilio cha kipofu tu, bali pia kilio cha wale ambao walimwambia kipofu “anyamaze”! jibu la Yesu linaonyesha mchanganyiko wa huruma na hasira, kwa sababu alikuwa kushughulika kwa upofu wa aina mbili tofauti, yaani, upofu wa Bartimayo na upofu wa umati wa watu ambao walikuwa wakimfuata Yesu bila ushirika na hisia zake. Je, ni nani ana upofu zaidi, yule aliye kipofu asili au wale ambao hawapati kuona walio na mahitaji kandokando yao? Hata hivyo kuna tumaini, kwa sababu miongoni mwa wale ambao walimwambia kipofu “unyamaze!” walikuwapo wengine ambao walimwambia “jipe moyo, anakuita! Yeye hajamsahau na hawaachi wale ambao wanamwamini”. Sauti hizi ni za watu ambao wanachukua ujumbe wa unabi na wanapata kuwahamasisha wenye kukata tamaa. Ni ishara pia ya walio upatanishi wa Mungu katika maisha ya yeyote anayegundua wito wake ili aweze kumjibu Mungu kulingana na matarajio yake.


     Yesu ambaye tunamfuata ni mwenyeunyeti sana. Ana macho na masikio makini sana kwa hali halisi ya watu. Anatualika kuwa na unyeti sawa. Kwa kawaida sisi ni kama kipofu huyo, tunahitaji mkutano wa mabadiliko ya maisha ili kuona bora nini inatokea kandokando yetu na kumfuata yesu ambaye anatuleta maana mpya kwa maisha yetu. Sisi ni pia kama wengine karibu na Yesu, lakini mbali sana na ndugu zetu, waliofungwa kabisa kwa hali halisi kandokando yetu na hata tunafikiri kwamba tuna mamlaka ya kuwaambia wengine: “mnyamaze”. Sisi  tuko na kosa kubwa. Sisi lazima kuwamakini sana kuhusu baadhi ya uzoefu ambao unatufungua kwa Mungu lakini unatufunga kwa wengine. Ikiwa imani yetu haituongozi kukutana na wengine na haitufanyi wenye huruma, imani hii ni udanganyifu. Kupitia Ekaristi hii, tumwombe Mungu neema ya imani ya kweli na halisi.

Fr Ndega
Mapitio: Nikoletee

quarta-feira, 7 de outubro de 2015

MUNGU BABA YETU KATIKA BIBLIA NA KATIKA MAWAZO WA Mt. YOHANE CALABRIA

katika siku hii ya maadhimisho ya sikukuu ya Mtakatifu Yohana Calabria nataka kupendekeza kutafakari kuhusu UBABA WA MUNGU. Tunamshukuru Mungu Baba ambaye ametupa Yohane kama nyota mbinguni na nuru karibu nasi. 
YOHANA WA MASKINI (M: Jorge Trevisol – Translation to Kiswahili: Fr Ndega)
- Imba viumbe vyote! Hii ni siku kwa wote/ Mungu alitupa Yohana, nyota mbinguni, nuru karibu nasi/ imba viumbe na watu!/ imbeni kwa furaha kubwa!/ uhai unapendeza Mungu/ ana upendo wa Baba kwa maskini wake/ Ref: /: Imba Yohana wa maskini, kwamba dunia itakusikiliza/ Mungu aliyefanya mvua, jua, bahari na ni Baba yetu pia.:/ 2. Ninahisi upo karibu/ naimba na unaimba nami/ unasema kwa nyuso za wengi kwa uhai dhaifu ndani yangu unakutafuta/ ufukuze hofu yetu/ kila wakati una nguvu/ Kuishi sasa kwa muda ni kuhisi kwamba wewe ni yote milele/ 3. kwa sababu uliishi hayo/ kwa sababu ulituambia/ vivyo hivyo tutaishi/ pamoja na wewe/ kamwe bila na wewe/
MPANGO WANGU WA KUTAFAKARI
Utangulizi
1 Ubaba wa Mungu katika Biblia
            1.1 neno Baba kwa uhusiano na Mungu katika Agano la Kale
            1.2 neno Baba katika Injili
            1.3 maneno Mungu Baba ni yenyewe ya Waraka wa Mitume
            1.4 Yesu anamdhihirisha Mungu kama Baba
            1.5 “Sala Baba yetu ni awali ya Injili” (Mt. Yohane Calabria)  
2 Uzoefu wa Ubaba wa Mungu kwa Mtakatifu Yohana Calabria na Familia yake ya Kiroho
Hitimisho

Utangulizi
Msomo wa kutafakari kwetu ni kuhusu Mungu Baba au ubaba wa Mungu. Bila shaka kwamba baada ya tutafute maana ya maneno haya katika Biblia, rejeo kwa kutafakari kwetu itakuwa maandiko, mawazo na mtazamo wa Mtakatifu Yohana Calabria. Msomo huu kuhusu ubaba wa Mungu ni jambo la msingi la kiroho ya Calabria. Ni vizuri sana kujua kwamba Yohana Calabria aliwekwa mtakatifu katika mwaka wa Mungu Baba ambao ulikuwa sehemu ya mwisho katika maandalizi kwa sherehe ya yubilei ya Miaka elfu mbili ya kuzaliwa kwake Bwana Yesu Kristu.
Mwanaume huyo mkuu anayeitwa Yohana Calabria alizaliwa terehe nane mwezi wa kumi mwaka wa elfu moja mia nane sabini na tatu. Alikuwa maskini sana kwa mtazamo wa kibinadamu na tajiri sana kwa upande wa Mungu. Kulingana na uzoefu wake tunajifunza kwamba hatuweze kuongea kuhusu Mungu ikiwa hatupitii hayo. Na huu ulikuwa uzoefu wake, yani, Mungu ni Baba na Mtoaji. Ingawa hali mbili inatokea pamoja katika Mungu, tutatafakari kuhusu ubaba peke yake.

1 Ubaba wa Mungu katika Biblia

1.1 neno Baba kwa uhusiano na Mungu katika Agano la Kale
Maneno Baba yetu si maneno ya Yesu tu, kwa sababu kabla yeye yalitumika katika maandiko ya manabii ya Agano la Kale. Bila shaka Yesu hakuyatumia maneno haya tu, bali alianzisha uhusiano mpya na Mungu, akileta maana mpya kabisa kwa maneno Baba yetu. Neno Baba kwa uhusiano na Mungu, tunaweza kukuta katika: Isaya 9:6 (Baba milele); Is 63:16 (wewe ni Baba yetu - mara mbili); Is 64:8 (wewe ni Baba yetu); Yeremia 3:4.19 (Baba yangu – mara mbili); Malaki 2:10 (Tuna Baba mmoja)

1.2 neno Baba katika Injili
Kuhusu injili hali ni tofauti sana kwa sababu neno hili lilikuwapo midomoni mwa Yesu daima, yaani, Baba, Baba yangu, Baba yenu, Baba yake, Baba Yako, Baba yao, Baba yetu,etc. Katika Mathayo - mara 42; Marko – mara 5; Luka - mara 16; Yohane – mara 114. Tunaweza kusema kwamba Yohane ni “Injili ya Baba” kwa sababu inaongea sana kuhusu uhusiano wa Yesu na Baba yake. Tena tunatambua kwamba katika toleo hili peke yake tunaweza kufanya maneno kama Baba mtakatifu, Baba mwenye haki, Baba yangu na yenu pamoja, etc. Katika matoleo ya Mathayo, Marko na Luka tunakuta uzoefu wa ubaba kwa uhusiano na huruma na kujua, kwa nfano, Baba atawasamehe, Baba yenu anajua,etc.  Lakini sala ya Bwana inayojulikana kama Baba yetu, tunaweza kukuta katika Mathayo na Luka peke yao.

1.3 maneno Mungu Baba ni yenyewe ya Waraka wa Mitume
Maneno mawili pamoja, yaani, Mungu Baba, tunakuta katika Agano Jipya peke yake na hasa katika Waraka: Wagalatia 1,1; Waefeso 6,23; Wafilipi 2,11; Wakolosai 3,17; 1Wathesalonike 1,1; 2Wathesalonike 1,2; 1Timotheo 1,4; 2Timotheo 1,4; Tito 1,4; 1Petro 1,2; 2Petro 1,17; 2Yohane 1,3; Yuda 1,1. Mara nyingi maneno haya Mungu Baba yanatumika kuonyesha shukrani au utambulisho kuhusu zawadi za Mungu katika jumuyia. Yanaonyesha pia matakwa ya mtume mwandishi kuhusu safari ya imani ya jumuiya fulani.

1.4 Yesu anamdhihirisha Mungu kama Baba
Yesu anapoongea na Mungu na kuhusu Mungu, anatumia neno Baba. Hali hii inatafisiri uzoefu wa ndani, ushirika wa upendo na uhai kati ya Mwana na Baba yake. Maisha yake na uzoefu wake na Baba ni mwaliko kwa wasikilizaji washiriki katika ushirika sawa, wakiishi kwa uzoefu wa ndani na Mungu. Yesu anatuletea ufunuo wa uso kweli wa Mungu: wa kwanza - Mungu aliye na wasiwasi kwa utunzaji wa upendo kwa kila kitu, “hata nywele moja ya kichwa chetu” (Lk 21,18); wa pili - Mungu Baba, ambaye ana watoto tofauti na anashiriki zawadi zake na wote kwa njia sawa. Anawapenda wote na anataka kwamba watu wote wajihisi kuishi katika familia, washiriki furaha yake kama Baba. Katika familia hii anautoa utunzaji na ulinzi ambao ni maonyesho ya upendo wake wa Baba. Tuko katika ushirika wa ndani naye ikiwa tunashiriki hisia zake kuhusu wengine. Kwa hivyo Yesu alitufundisha kusali, akishiriki nasi njia yake yenyewe ya kusali. Alitujulisha kujua huyo ambaye ni Baba yake na Baba yetu pia.

1.5 “Sala Baba yetu ni awali ya Injili” (Mt. Yohane Calabria)

Mantra: Baba sikia wanao, sikia sauti zao, sikia dunia nzima...
Yesu anapowafundisha wanafunzi wake kusali, aliwakumbusha kuhusu mahitaji ya tabia ya mwana anayemwomba Baba kwa imani. Kama yeye alivyoishi, tabia kamili ya wanafunzi lazima kuwa kujisalimisha mikononi mwa Huyo anayejua mahitaji ya wana kabla ya wamwulize kitu. Sala ya kweli ni kitendo cha kujisalimisha. Sehemu ya kwanza ya sala ambayo Yesu anawafundisha wanafunzi wake ni utambulisho wa ubaba wa Mungu, ambaye ni mwema na mtoaji. Katika sala hii, kila kitu ambacho kinaja baada ya Baba kinategemea kwa neno hili/mwelekeo/hali. Ni lazima kufanya mapenzi ya Mungu ili Ufalme wake utokee duniani kama mbinguni. Mapenzi ya Baba huyu lazima kuwa chakula cha watoto wake kama kilichotokea na uzoefu wa Yesu miongoni mwa wanadamu.  
Kwa Baba huyu sisi lazima kuhutubia kwa imani, wenye uhakika kwamba tumepokea sana. Tunaomba kwa mkate, msamaha na upatanisho. Kulingana na Maandiko matakatifu, “kutokana na wema wake tumepokea neema juu ya neema”. Sala hii inathibitisha utunzaji wa upendo wa Mungu anayeshiriki zawadi zake na wana wake, akitarajia kwamba tufanye vivyo hivyo na wengine ili udugu uwe maonyesho ya kweli ya ubaba wake na chombo cha huruma yake. Maombi Baba yetu yanatufundisha kufikiri kuhusu mahitaji ya wengine na si kwa mahitaji ya kibinafsi tu. Kupitia sala hii tunaomba muhimu zaidi, yaani, “mkate wa kila siku” kwa sababu sisi lazima kupinga dhidi ya aina yote ya ukusanyaji na ubadhirifu ambao unaharibu udugu, kufanya maskini na wenye njaa wateseke. Kuhusu mambo haya Baba Mtakatifu Francisco asema: “Ulaji umetuongoza kutumia chepesi pamoja na ubadhirifu wa chakula cha kila siku... sisi lazima kukumbuka kwamba chakula ambacho sisi hutupa takatakani ni kama ikiwa tulikuwa tumeiba kutoka meza ya walio maskini na wenye njaa.”
Kwa Mt. Yohana Calabria, “sala Baba Yetu ni awali ya Injili. Matatizo lazima kufikiriwa na kusomwa kwa uhusiano na maelewano kwa ubaba wa Mungu.” Ikiwa tunasema “Baba Yetu” ni kwa sababu tunasadiki kwamba sisi ni ndugu wa wengine wengi. Mungu hawabagui watu na hamsahau yeyote wa wana wake. Hapendezwi na sala ambayo haifikirii ndugu wengine. Mungu si daima anatupa vitu ambavyo tunamwomba, bali anatupa daima vitu tunavyohitaji kwa sababu anajua kila kitu. Ikiwa mara nyingi hatupokei vitu ambavyo tunamwomba ni kwa sababu hatuombi ipasavyo. Labda kutokuwa na tabia na nia kamili iliyodaiwa na Yesu wakati aliwafundisha wafuasi wake kusali. Tunaalikwa kuishi kwa udugu kutokana na ubaba wa Mungu na kuwa na mioyo ya wana, kwa sababu mtu asiyeishi kama mwana hajifunzi kuwa ndugu.

2 Uzoefu wa Ubaba wa Mungu kwa Mt. Yohana Calabria na kwa Familia yake ya Kiroho
Mantra: Baba yetu sisi ni wanawe, Baba yetu sisi ni ndugu...
Mt. Yohane Calabria alikuwa mwenye unyeti daima kwa ishara za utunzaji wa Mungu ulimwenguni. Lakini usiku mmoja wakati yeye hakupata kulala usingizi, alichukua injili na aliufanya ugunduzi mkubwa. Aligundua jinsi ya kuishi kwa uhalisi ubaba wa Mungu. Kifungu ambacho kiliichukua uangalifu wake zaidi kilikuwa Mt 6,24-34. Kutokana na kifungu hiki alichukua ahadi kwake na kwa familia yake ya kiroho, yaani, “Mtafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake; na hayo yote mtapewa kwa ziada.” Kulingana naye kwa kushuhudia duniani kwamba Mungu ni Baba, Mama, Kila Kitu, tunahitaji kwanza kufanya sisi wenyewe uzoefu wa ubaba wa Mungu na kulima hisia ya miliki ya Baba huyu. Kama hivyo alimwambia mama fulani: “Sisi ni wa Mungu, Mungu ni Baba, Mama Kila kitu chetu. Upende Bwana na atakuwa heri (mwenye furaha)” (24-1-1930).
Kwa yeye, “Mungu ni Baba na Baba mwema. Hakuna mama ambaye anawapenda sana watoto wake kama Mungu anawapenda watu wote na kila mmoja wetu”. Calabria anaongea pia kuhusu Mungu kama Riziki, kwa sababu kulingana naye, haiwezekani kutenga Ubaba wa Mungu na Riziki yake. Kwa hivyo, asema, “Riziki ni Mama mpole ambaye hupatia kila kitu kwa wema wetu, hata kwa wema wetu mkubwa. Tunapaswa kuhisi tumebebwa kwa mikono yake ya mama”. Yohana Calabria aliamini katika ukweli huo na aliyapanga maisha na kazi zake zote kulingana na hali hii. Katika mwanzo mwa kazi yake, alipoonekana mtoto wa kwanza, Yohana alifahamu kwamba Mungu akatarajia kutoka kwake imani maalum ambayo huonyeshwa kupitia matendo mema kwa masikini wapendelewa na Mungu. Baada ya mtoto wa kwanza, wengine wengi walikuja nyumbani. Nyumba hiyo iliitwa “Nyumba ya wavulana wema”. Kama hii, ishara ya mapenzi ya Mungu ilikuwa wazi sana kwa Yohana Calabria.
Kupitia uzoefu ambao Mt. Calabria aliishi kuhusu ubaba wa Mungu, akawa mshahidi na mhubiri wa ubaba huu. Kama hivyo asema, “Injili anatuongelea, kwa mfano, Mungu ni Baba, anatujali zaidi kuliko ndege wa angani na maua ya mashamba hata atatujalia kile ambacho tunahitaji kwa chakula na kwa mavazi, lakini tunapaswa kuutafuta kwanza Ufalme wake na haki yake. Basi, je, imani yetu katika ubaba wa Mungu ni nzuri? Je, tena ni nzuri imani yetu katika Riziki yake takatifu na wema?” 
Imani kweli na asili inafikiria Mungu si kama Muumba na Bwana tu, bali kwanza kama Baba”. Mungu ni Baba, hutujali na wote ambao tunawapenda; macho yake ni makini sana kwa kila kitu; hakuwezi tokea chochote kisichotarajiwa kama mshangao (bila maana); kila kitu kinapangwa na kuongozwa na hekima, nguvu na wema wake pasipo mwisho. Juu ya yote tunaweza kusema kwamba ni kwa wema wake.

Hitimisho
Uzoefu wa ubaba wa Mungu ulimhamasisha Yohane Calabria kuanza Kazi kubwa. Katika mwanzo, padre Yohane alisaidiwa na mama yake. Lakini, baada ya wakati mchache, walikuja Mabruda, Mapadre, Masister, makundi mengi ya watu wasio watawa. Pamoja na padre Yohana, sisi ni Familia ya Kiroho ya Calabria inayoitwa “Poor Servants of Divine Providence” na kazi yetu ni kutafuta Ufalme wa Mungu. Hali hii inatokea katika ahadi ya kuifufua imani duniani kwa Mungu Baba wa wanadamu wote, kupitia kujisalimisha kabisa kwa Riziki yake. Kiroho yetu ni Injili. Kulingana na Mtakatifu Yohana Calabria, tunahitaji kurudi kwa Injili daima ili maisha yetu yabadilike na hali kandokando yetu pia.
Maandiko ya Mt. Yohana Calabria yanadhihirisha jinsi alivyokuwa na ubinadamu mno, akifahamu ugumu wa wengine, lakini kwa wakati sawa, alijua kuonyesha njia kamili kwa ufumbuzi wa matatizo yao. Kutokana na uzoefu wa Mt. Calabria tunajifunza kwamba Mungu ni Baba mwema na mtoaji bila mwisho, na sisi sote ni ndugu katika Kristo. Tunaalikwa kuishi kama ndugu kutokana na ubaba wa Mungu na kuwatendea mema wengine vivyo hivyo tungependa wao watutendee. Kulingana naye, “Tunapaswa kuwa na kujihisi watumishi, bali kwa utumishi wa Mwenyeji fulani ambaye ni pia, na kwanza kabisa, Baba. Basi utumishi wetu ni wa wana, utumishi wa huria na upendo... kama alivyotumika Bwana wetu Yesu Kristo, mtumishi wa Baba kwa namna ya ajabu, ambaye wakati wa maisha yake ya kibinadamu alifanya tu kutimiza amri zako: “Ninafanya kama Baba alivyoniamuru kufanya.”

Tumsifu na tumshukuru Mungu Baba kwa kielelezo cha imani ambacho ni Yohane Calabria na mtume wake duniani kupitia Familia yake ya Kiroho. 

Fr Ndega
Mapitio: Sara  

domingo, 4 de outubro de 2015

IN THE BEGINNING GOD CREATED WOMAN AND MAN


Reflection from Mk 10:2-16

    In the beginning of today’s gospel Jesus was teaching the people as he always did. Suddenly some Pharisees came to him, trying to trap him. The matter was about divorce. Jesus perceived their bad intention, but even so welcomed them well, listening to them with patience and valuing their effort in questioning him. In the dialogue with Jesus, their unique problem was the deficient vision about matrimony and family. Jesus corrects this mentality, reminding them about the original plan of God concerning man and woman. He speaks also about adultery as result of the divorce and shows special relationship with the children who merit to be respected and valued so that they can grow in security and joy.

      Some Pharisees use the Law of Moses to trap Jesus. According to their mentality, this Law allows divorce, but Jesus doesn’t agree with them. Why does Jesus have a different position in relating to this matter of the Law? According to the Book of Deuteronomy 24, the man can write a letter of divorce if he finds something in his wife which he doesn’t like. The woman had very few opportunities to present letter of divorce to his husband, for example, if the husband was infected with leprosy. In this context the situation of the woman was very difficult because she was bullied and depended of the good will of the man. But Jesus helps them to think better because the Law was made for the good of the people and not the people for the good of law.

    The position of Jesus is very clear. He came to reveal the original plan of God and according to this plan, both man and woman have been created liked and resembled God and God shared with them his love which makes them to desire one another and at last to leave their parents, to unite themselves and be one body. This reality shows that the man doesn’t have right to do what he wants with his wife, for example, to abandon the wife in any moment he wants. So, their union means that they cannot abandon each other or to be separated. The main objective of Jesus is to recover the dignity of the woman removed by the Law. According to Jesus woman has right of being respected in the matrimonial life and not being mistreated or dominated like possession. The intention of God is that husband and wife continue growing in love and lastly get eternal life. And we can share this plan of God of living unity of life in our families or communities.   

       Human desire to love and to be loved is the reason of the existence of the marriage and the family. The family is the base of human experience and anything which goes against this principio is prohibited in the Bible. For that “don’t commit adultery” is included among the Ten Commandments. Why does adultery threaten the family? Adultery can destroy a family because it can result in pregnancy and the birth of a child. That child will start out life with no family. If adultery doesn’t destroy a family, it almost always causes terrible harm to a marriage, such as sense of betrayal and loss of trust which means that adultery causes a fraudulent life. It is necessary to be careful with some kinds of friendship. When the husband or wife has some friendship with relationship stronger than which he/she has with the spouse it is more difficult to resist to the adultery. When a husband or wife is having sex with someone other than their spouse, the thought cannot release about another person and how to deceive the spouse. Adultery doesn’t protect the family and doesn’t protect the spouses from emotional pain.  


     Protecting the family is the reason for the commandment. Why the family is so important? Because without it the social stability is impossible. Because without it the passing on of society’s values from generation to generation is impossible. Because the relationship between parents and children make them more responsible and mature. Because more than anything else the family satisfies emotional and material needs, giving to the children secure and stable childhood.

Fr Ndega
Review: Sara

MWANZO MUNGU ALIWAUMBA MWANAMKE NA MWANAMUME


Kutafakari kutoka Marko 10:2-16

     Mwanzoni mwa injili ya leo Yesu alikuwa akiwafundisha watu kama ilivyokuwa desturi yake. Ghafla baadhi ya Mafarisayo walimwendea wakimjaribu. Jambo lilikuwa kuhusu talaka. Yesu aliitambua nia yao mbaya, lakini aliwatendea mema, akiwasikiliza kwa utulivu na kuthamini juhudi zao za kumwuliza maswali. Katika mazungumzo na Yesu shida yao ya pekee ilikuwa mtazamo pungufu kuhusu ndoa na familia. Yesu alisahihisha mtazamo huo, akiwakumbusha mpango asili wa Mungu kwa mwanamume na mwanamke. Aliongea pia kuhusu uzinzi kama matokeo ya talaka na kuonyesha uhusiano maalum na watoto wadogo ambao wanastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa ili wakue kwa usalama na furaha.

      Baadhi ya Mafarisayo wanatumia sheria ya Musa kumjaribu Yesu. Kulingana na mawazo yao, Sheria hiyo inaruhusu talaka, lakini Yesu anayakataa hayo. Kwa nini Yesu ana msimamo tofauti kwa uhusiano na jambo hili la Sheria? Kulingana na Kitabu cha Kumbukumbu la Sheria, sura 24, mwanamume aliweza kumpatia mkewe talaka ikiwa hakupendezwa naye kwa sababu ameona kwake kitu kisichofaa. Mwanamke alikuwa na nafasi chache za kutoa talaka kwa mmewe, mfano mwanaume akiugua ukoma. Katika mazingira haya hali ya mwanamke ilikuwa ngumu sana kwa sababu daima alionewa na daima alitegemea huruma tu ya mwanamume. Lakini Yesu aliwasaidia kufikiri vizuri kwa sababu Sheria zimewekwa kwa manufaa ya watu na si watu kwa ajili ya sheria.

      Msimamo wa Yesu ni wazi sana. Yeye alikuja kudhihirisha mpango asili wa Mungu na kulingana na mpango huu, wote mme na mke wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na Mungu ameweka upendo asili unaowafanya watamaniane na hatimaye kuwaacha wazazi wao, kuungana na kuwa mwili mmoja. Jambo hili linaonyesha kuwa mwanaume hana haki ya kuamua atakavyo kwa mkewe, mfano kumwacha mke wake kwa muda wowote anaotaka. Hivyo kuungana kwao kunamaanisha kuwa hawawezi kuachana au kutenganishwa. Lengo kuu la Yesu, ni kukarabati nafasi na utu wa mwanamke ulioharibiwa na sheria. Kulingana na Yesu Mwanamke ana haki ya kuheshimiwa katika maisha ya ndoa na si kutendewa na kumilikiwa kama chombo tu. Nia ya Mungu ni kuwa mume na mke waendelee kukua katika pendo na kupata uzima wa milele. Nasi tunaweza kuushiriki mpango huu wa kuishi maisha ya umoja katika familia na jumuiya zetu.

     Thamani ya kibinadamu ya kupenda na kupendwa ni maana ya uzoefu wa ndoa na familia. Familia ni msingi wa uzoefu wa kibinadamu na yoyote ambayo ni dhidi ya kanuni hii ni marufuku katika biblia. Kwa hiyo “Usizini” ni moja miongoni mwa Amri Kumi. Kwa nini uzinzi hutishia familia? Uzinzi unaweza kuharibu familia kwa sababu unaweza kusababisha ujauzito na kuzaliwa kwa mtoto. Mtoto huyo ataanza safari ya maisha pasipo familia. Ikiwa uzinzi hauharibu familia, mara nyingi unasababisha madhara ya kutisha ndoa, kama hisia ya usaliti na upotevu wa itibari ambayo inamaanisha kwamba uzinzi unasababisha maisha ya ulaghai. Ni lazima kuwa macho kwa baadhi ya aina za urafiki. Wakati mume au mke ana urafiki fulani ambao anaanzisha uhusiano wa nguvu zaidi kuliko ule anaoishi na mke au mume, ni ngumu sana kuuepuka uzinzi. Wakati mume au mke ana ngono na mwingine kuliko mkewe/mumewe, mawazo kuhusu yule mtu ni daima na mawazo kuhusu jinsi ya kumdanganya mume au mke ni daima pia. Uzinzi haulindi familia na tena hauwalindi wanandoa dhidi ya maumivu ya hisia. 

        Maana ya Amri “Usizini” ni ulinzi kwa familia. Kwa nini familia ni muhimu sana? Kwa sababu pasipo familia uimara wa jamii hauwezekani. Kwa sababu bila familia mawasiliano ya thamani ya jamii kizazi kwa kizazi hayawezekani. Kwa maana uhusiano kati ya wazazi na watoto unawafanya kuwajibika na kukomaa zaidi. Kwa sababu bora kuliko chochote, familia inayaridhisha mahitaji ya hisia na fizikia/mwili, kuwapa watoto utoto salama na imara.

Fr Ndega

Mapitio: Sara