Kutafakari kutoka Hes 11:25-29; Mk 9:38-43, 45, 47-48
Mungu hawabagui watu kwa maana anapenda na katika
upendo hakuna ubaguzi. Maatarajio yake ni kwamba watu wake wote wangekuwa
manabii, wanasikiliza neno lake na kuongea katika jina lake. Kupitia Roho wake
Mtakatifu, anawahamasisha watu ili watende mema kulingana na mapenzi yake, akidhibitisha
kwamba tendo lake halina mpaka. Mbele ya Mungu hakuna mtu wa heshima zaidi
kuliko mwingine. Yeye hakubali umaarufu au ubaguzi, bali anatarajia ahadi kwa
njia yake ya kufikiri na kutenda. Maana kwa njia hii ni upendo wake wa bure kwa wote.
Wanafunzi wa kwanza walijaribu kumkataza mtu fulani
kufanya mwujiza kwa jina la Yesu kwa sababu hakuwa mmoja wao. Wlifanya hivyo
kwa mamlaka gani? Yesu hakubaliani na tabia hii na akawaambia kwamba mtu ambaye
anatenda mema kwa jina lake (Yesu) hawezi kumnenea mabaya. Kisha akiendelea kwa
mafundisho yake, alisema kwamba watu wanaosaidia wafuasi wake watapokea tuzo
kwa sababu ya utambulisho wake na wale waliotumiwa katika jina lake. Yesu
anawakumbusha pia kwamba juhudi yote ya wale wanaomfuata lazima kuwa hamasa kwa
wale ambao wanaanza kumwamini Kristo au wana ugumu kumwamini. Kashfa ni jambo mahututi sana na ni lazima
kuepukwa kwa sababu huivuruga imani.
Tumetafakari kuhusu ugumu wa wanafunzi wa Yesu
kuelewa na kuyapokea mafundisho yake. Wanaelewa nusunusu, hasa ile sehemu
rahisi, wanaipokea na kuacha yaliyo magumu. Ni hatari mno kuelewa nusu ya
ukweli kwa sababu kama hii tunaweza kuleta uzushi. Kujaribu kumkataza mtu
fulani ambaye alifanya mema kwa jina la Yesu ni ishara ya ugumu ya kumfahamu
Yesu na mapendekezo yake. Maana ya kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu si maneno tu,
bali ni matendo mema hata kama mtu huyu hayumo kwenye kundi. Badala ya kuwakataa
wengine ambao wanatenda mema kwa jina la Yesu, wanafunzi wake wanapaswa
kujikataa wenyewe. Kuwa mwanafunzi wa Yesu inamaanisha imani iliyoonyeshwa kwa
matendo. Kwani wao wanaokiri na kutenda kama kadiri ya neno” ndiyo mama na
ndugu zake na wanafunzi wake. Ikiwa huyo mtu alitenda mema kwa jina la Yesu,
tayari alikuwa mwanafunzi wake. Mtazamo wa wanafunzi una upungufu na ubaguzi,
lakini mtazamo wa Yesu ni mpana na ni kwa wote wenye mapenzi mema.
Kitu muhimu katika dini au imani ni matendo na
siyo maneno. Matendo husema zaidi ya maneno. Mifano halisi ni wakristo wa
kwanza, waliweza kuwavuta wengine si kwa maneno, bali njia yao ya maisha. Kuhusu
wao watu walisema: “Mwone kama wanavyopendana”! hali hii iliwezekana kwa sababu
ya upendo wao ulionyeshwa kupitia ridhaa wao kwa wao, kushiriki pamoja,
uvumilivu katika maombi pamoja na unyenyekevu wa moyo. Kuhusu hayo Sinodi ya
Afrika imesema: “Sharti muhimu la kuhubiri ni ushuhuda wa maisha”. Mwanafunzi
wa kweli wa Yesu hawezi kuwa na ubaguzi na kuamini kuwa watu wa kundi lake
pekee, au chama chake cha utume, au kanisa lake ndiyo wanafunzi pekee wa Yesu
na wameokolewa. Hatuwezi kufikiri kwamba Yesu ni mali yetu. Ikiwa tunahisi karibu na Yesu, hatuwezi kuishi mbali sana na ndugu zetu, kufungwa
kabisa kwa hali kandokando yetu na hata kufikiri kwamba tunakuwa na mamlaka ya
kuwazuia wengine watende kwa jina la Yesu. Tuko mbele ya kosa kubwa. Sisi
lazima kuwa makini sana kuhusu baadhi ya uzoefu ambao unatufungua kwa Mungu
lakini unatufunga kwa wengine. Ikiwa imani yetu haituongozi kukutana na wengine
na kutambua mema ambayo wanaweza kufanya imani yetu ni utenganisha. Basi, ili Mungu
atufundishe kutambua mwendelezo wa kazi zake mbele ya matendo mema ya wakristo
na kusaidiana kwa wema wa wote.
Fr Ndega
Mapitio: Sara