Kutafakari kutoka Kum 4:1-2.6-8; Mk 7:1-8.14-15.21-23
Mungu
aliwapa watu wake Amri zake na akawafundisha njia ya kuzishika. Haziwezi
kubadilishwa kulingana na mapenzi ya kibinadamu. Kama maonyesho makuu ya upendo
na utunzaji wa Mungu, Yesu anatukumbusha muhimu zaidi ya sheria na anatufundisha
kuishi na uhusiano wa kiroho na Mungu. Uhusiano huu uko juu ya sheria zote.
Kulingana
na somo la kwanza, kupitia utumishi wa Musa, Mungu anawaalika watu wa Israeli
washike amri zake kama miongozo kwa uzima. Baada ya kuwaweka uhuru kutoka Misri,
Mungu alianzisha agano na watu hawa huko Sinai na Amri zilikuwa miongozo
kama maonyesho ya matarajio yake kuhusu maisha ya watu wake. Kuishi kulingana
na Amri kumekuwa umuhimu katika safari ya Watu wa Israeli ambao Sheria ni Neno
la Mungu na Neno la Mungu ni Sheria. Wakati wao husema “Sheria ya Mungu ni
kamilifu, faraja kwa roho”, wanamaanisha Neno la Mungu. Kuna uhusiano wa ndani
kati ya Sheria na Neno, kwa sababu amri za Sheria zinaonyesha utunzaji na upendo
wa Mungu anayeongea kuonyesha njia za ukombozi. Na tena zinadhihirisha
utambulisho na hekima ya Watu ambao wanamtii Mungu wao. Utii kwa amri ni chanzo
cha baraka kinachoelekeza kwa uhai, wakati uasi kwa hizo unaelekeza kwa mauti.
Katika Sheria kuu, Wayahudi waliweka maagizo mengi ya
kibinadamu na kidogo kidogo walibadilisha mwelekeo kutoka zile zilizokuwa
muhimu zaidi. Hata kwa wao wenyewe ni ngumu kuishi maagizo yote yaliyoongezwa.
Hii ni maana ya mapambano kati ya Yesu na Waandishi na Mafarisayo ambao
walikuwa wakuu kwa mabadiliko ya maana ya Sheria. Kabla ya Yesu manabii wengi walikwisha pinga
kuhusu tabia hii. Miongoni mwao wapo Isaya, Hosea na Amosi. Hasa kulingana na
nabii Isaya, tunakuta tangazo muhimu kutoka kwa Mungu: “Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao ni mbali
nami; nao waniabudu bure. Wanayafundisha maagizo ya kibinadamu tu.”
Yesu anawakosoa walimu wa sheria na
mafarisayo kwa sababu walitafsiri sheria kulingana na mawazo yao na walikuwa
vielelezo vibaya kwa watu wote hasa kwa wanafunzi wake. Mara nyingi Yesu alipokutana
nao hafikii mafanikio kuhusu mapendekezo yake ya maisha mapya kwa sababu wao ni
wanafiki na wanapendelea kumjaribu Yesu kuliko kujiruhusu kubadilishwa
kulingana na matarajio yake. Kwa hivyo mkutano wa Yesu nao ni maana ya
mapambano daima. Wao ni wenye upayukaji kwa sababu hawatendi yale wanayosema. Waliyaondoa
maana ya unabii wa sheria na wanafundisha maagizo ya kibinadamu tu. Wanajifikiria
watu wema na wanajijulisha vizuri nje mbele ya wengine, lakini ndani yao ni
tofauti, ni hali mbaya. Wanatumia dini kwa uradhi wa binafsi yao na wanawazuia
wengine kuishi kwa uhuru na furaha. Kutokuwa na uhalisi na ukweli kuifanya imani yao ishara ya kutafuta heshima na sifa kwa wao wenyewe, mbali sana na Mungu.
Upinzani wa
Yesu dhidi ya tabia ya vikundi hivi viwili ni mwaliko kwa mabadiliko ya mawazo
yetu kuhusu dini, kuhusu uhusiano wetu na Mungu. Utambulisho wetu wa dini hauwezi
kuwa ishara ya nje tu, yaani, kwenda kanisani na ushiriki katika sakramenti,
kutii amri za kanisa. Yesu alithamini zaidi maisha ya watu kuliko sheria. Yesu
anajali zaidi uhusiano wa kiroho na Mungu, anatualika zaidi kubadilika kiroho.
kushiriki kanisani kunatupasa kuwa watu wapya na tofauti nyumbani kwa wema wa
familia. Maneno au matendo mabaya ni ishara ya kutokuwa na uzoefu wa ndani na
Mungu. Utambulisho wetu kama wafuasi wa Yesu unatuongoza kuheshimu uhuru wa
watu na kupendelea mazungumzo kuliko kulazimisha. Kama watoto wa Mungu sheria
yetu ni udugu, kuwafikiria wengine kuwa muhimu zaidi kutuliko sisi wenyewe. Yesu
anatarajia tuwe na uhusiano wa kiroho na Mungu.
Fr Ndega
Mapitio: Sara