katika siku hii ya maadhimisho ya sikukuu ya Mtakatifu Yohana Calabria nataka kupendekeza kutafakari kuhusu UBABA WA MUNGU. Tunamshukuru Mungu
Baba ambaye ametupa Yohane kama nyota mbinguni na nuru karibu nasi.
YOHANA WA MASKINI (M: Jorge Trevisol – Translation to Kiswahili:
Fr Ndega)
- Imba viumbe vyote! Hii ni siku kwa wote/ Mungu alitupa
Yohana, nyota mbinguni, nuru karibu nasi/ imba viumbe na watu!/ imbeni kwa
furaha kubwa!/ uhai unapendeza Mungu/ ana upendo wa Baba kwa maskini wake/ Ref: /: Imba Yohana wa maskini, kwamba
dunia itakusikiliza/ Mungu aliyefanya mvua, jua, bahari na ni Baba yetu pia.:/ 2.
Ninahisi upo karibu/ naimba na unaimba nami/ unasema kwa nyuso za wengi kwa
uhai dhaifu ndani yangu unakutafuta/ ufukuze hofu yetu/ kila wakati una nguvu/
Kuishi sasa kwa muda ni kuhisi kwamba wewe ni yote milele/ 3. kwa sababu
uliishi hayo/ kwa sababu ulituambia/ vivyo hivyo tutaishi/ pamoja na wewe/
kamwe bila na wewe/
MPANGO
WANGU WA KUTAFAKARI
Utangulizi
1 Ubaba wa Mungu katika Biblia
1.1 neno Baba kwa uhusiano na Mungu katika
Agano la Kale
1.2
neno Baba katika Injili
1.3
maneno Mungu Baba ni yenyewe ya Waraka wa Mitume
1.4
Yesu anamdhihirisha Mungu kama Baba
1.5
“Sala Baba yetu ni awali ya Injili” (Mt. Yohane Calabria)
2 Uzoefu wa Ubaba wa Mungu kwa Mtakatifu
Yohana Calabria na Familia yake ya Kiroho
Hitimisho
Utangulizi
Msomo wa kutafakari kwetu ni kuhusu
Mungu Baba au ubaba wa Mungu. Bila shaka kwamba baada ya tutafute maana ya
maneno haya katika Biblia, rejeo kwa kutafakari kwetu itakuwa maandiko, mawazo
na mtazamo wa Mtakatifu Yohana Calabria. Msomo huu kuhusu ubaba wa Mungu ni
jambo la msingi la kiroho ya Calabria. Ni vizuri sana kujua kwamba Yohana
Calabria aliwekwa mtakatifu katika mwaka wa Mungu Baba ambao ulikuwa sehemu ya
mwisho katika maandalizi kwa sherehe ya yubilei ya Miaka elfu mbili ya kuzaliwa
kwake Bwana Yesu Kristu.
Mwanaume huyo mkuu anayeitwa Yohana Calabria alizaliwa
terehe nane mwezi wa kumi mwaka wa elfu moja mia nane sabini na tatu. Alikuwa
maskini sana kwa mtazamo wa kibinadamu na tajiri sana kwa upande wa Mungu. Kulingana
na uzoefu wake tunajifunza kwamba hatuweze kuongea kuhusu Mungu ikiwa hatupitii
hayo. Na huu ulikuwa uzoefu wake, yani, Mungu ni Baba na Mtoaji. Ingawa hali
mbili inatokea pamoja katika Mungu, tutatafakari kuhusu ubaba peke yake.
1 Ubaba wa Mungu
katika Biblia
1.1 neno Baba kwa
uhusiano na Mungu katika Agano la Kale
Maneno Baba yetu si maneno ya Yesu tu, kwa sababu kabla yeye yalitumika
katika maandiko ya manabii ya Agano la Kale. Bila shaka Yesu hakuyatumia maneno
haya tu, bali alianzisha uhusiano mpya na Mungu, akileta maana mpya kabisa kwa
maneno Baba yetu. Neno Baba kwa
uhusiano na Mungu, tunaweza kukuta katika: Isaya 9:6 (Baba milele); Is 63:16 (wewe
ni Baba yetu - mara mbili); Is 64:8 (wewe
ni Baba yetu); Yeremia 3:4.19 (Baba
yangu – mara mbili); Malaki 2:10
(Tuna Baba mmoja)
1.2 neno Baba katika
Injili
Kuhusu injili hali ni tofauti sana kwa
sababu neno hili lilikuwapo midomoni mwa Yesu daima, yaani, Baba, Baba yangu, Baba yenu, Baba yake, Baba
Yako, Baba yao, Baba yetu,etc. Katika Mathayo - mara 42; Marko – mara 5;
Luka - mara 16; Yohane – mara 114. Tunaweza kusema kwamba Yohane ni “Injili ya
Baba” kwa sababu inaongea sana kuhusu uhusiano wa Yesu na Baba yake. Tena tunatambua
kwamba katika toleo hili peke yake tunaweza kufanya maneno kama Baba mtakatifu, Baba mwenye haki, Baba yangu
na yenu pamoja, etc. Katika
matoleo ya Mathayo, Marko na Luka tunakuta uzoefu wa ubaba kwa uhusiano na
huruma na kujua, kwa nfano, Baba
atawasamehe, Baba yenu anajua,etc.
Lakini sala ya Bwana inayojulikana kama Baba yetu, tunaweza kukuta katika
Mathayo na Luka peke yao.
1.3 maneno Mungu Baba
ni yenyewe ya Waraka wa Mitume
Maneno mawili pamoja, yaani, Mungu Baba, tunakuta katika Agano Jipya
peke yake na hasa katika Waraka: Wagalatia 1,1; Waefeso 6,23; Wafilipi 2,11;
Wakolosai 3,17; 1Wathesalonike 1,1; 2Wathesalonike 1,2; 1Timotheo 1,4;
2Timotheo 1,4; Tito 1,4; 1Petro 1,2; 2Petro 1,17; 2Yohane 1,3; Yuda 1,1. Mara nyingi
maneno haya Mungu Baba yanatumika
kuonyesha shukrani au utambulisho kuhusu zawadi za Mungu katika jumuyia.
Yanaonyesha pia matakwa ya mtume mwandishi kuhusu safari ya imani ya jumuiya
fulani.
1.4 Yesu
anamdhihirisha Mungu kama Baba
Yesu anapoongea na Mungu na kuhusu Mungu,
anatumia neno Baba. Hali hii inatafisiri uzoefu wa ndani, ushirika wa upendo na
uhai kati ya Mwana na Baba yake. Maisha yake na uzoefu wake na Baba ni mwaliko
kwa wasikilizaji washiriki katika ushirika sawa, wakiishi kwa uzoefu wa ndani
na Mungu. Yesu anatuletea ufunuo wa uso kweli wa Mungu: wa kwanza - Mungu aliye
na wasiwasi kwa utunzaji wa upendo kwa kila kitu, “hata nywele moja ya kichwa
chetu” (Lk 21,18); wa pili - Mungu Baba, ambaye ana watoto tofauti na
anashiriki zawadi zake na wote kwa njia sawa. Anawapenda wote na anataka kwamba
watu wote wajihisi kuishi katika familia, washiriki furaha yake kama Baba.
Katika familia hii anautoa utunzaji na ulinzi ambao ni maonyesho ya upendo wake
wa Baba. Tuko katika ushirika wa ndani naye ikiwa tunashiriki hisia zake kuhusu
wengine. Kwa hivyo Yesu alitufundisha kusali, akishiriki nasi njia yake yenyewe
ya kusali. Alitujulisha kujua huyo ambaye ni Baba yake na Baba yetu pia.
1.5 “Sala Baba yetu
ni awali ya Injili” (Mt. Yohane Calabria)
Mantra: Baba sikia wanao, sikia sauti zao, sikia dunia
nzima...
Yesu anapowafundisha
wanafunzi wake kusali, aliwakumbusha kuhusu mahitaji ya tabia ya mwana
anayemwomba Baba kwa imani. Kama yeye alivyoishi, tabia kamili ya wanafunzi
lazima kuwa kujisalimisha mikononi mwa Huyo anayejua mahitaji ya wana kabla ya
wamwulize kitu. Sala ya kweli ni kitendo cha kujisalimisha. Sehemu ya kwanza ya
sala ambayo Yesu anawafundisha wanafunzi wake ni utambulisho wa ubaba wa Mungu,
ambaye ni mwema na mtoaji. Katika sala hii, kila kitu ambacho kinaja baada ya Baba
kinategemea kwa neno hili/mwelekeo/hali. Ni lazima kufanya mapenzi ya Mungu ili
Ufalme wake utokee duniani kama mbinguni. Mapenzi ya Baba huyu lazima kuwa
chakula cha watoto wake kama kilichotokea na uzoefu wa Yesu miongoni mwa
wanadamu.
Kwa Baba huyu sisi
lazima kuhutubia kwa imani, wenye uhakika kwamba tumepokea sana. Tunaomba kwa
mkate, msamaha na upatanisho. Kulingana na Maandiko matakatifu, “kutokana na
wema wake tumepokea neema juu ya neema”. Sala hii inathibitisha utunzaji wa
upendo wa Mungu anayeshiriki zawadi zake na wana wake, akitarajia kwamba
tufanye vivyo hivyo na wengine ili udugu uwe maonyesho ya kweli ya ubaba wake
na chombo cha huruma yake. Maombi Baba yetu yanatufundisha kufikiri kuhusu mahitaji
ya wengine na si kwa mahitaji ya kibinafsi tu. Kupitia sala hii tunaomba muhimu
zaidi, yaani, “mkate wa kila siku” kwa sababu sisi lazima kupinga dhidi ya aina
yote ya ukusanyaji na ubadhirifu ambao unaharibu udugu, kufanya maskini na
wenye njaa wateseke. Kuhusu mambo haya Baba Mtakatifu Francisco asema: “Ulaji
umetuongoza kutumia chepesi pamoja na ubadhirifu wa chakula cha kila siku...
sisi lazima kukumbuka kwamba chakula ambacho sisi hutupa takatakani ni kama
ikiwa tulikuwa tumeiba kutoka meza ya walio maskini na wenye njaa.”
Kwa
Mt. Yohana Calabria, “sala Baba Yetu ni awali ya Injili. Matatizo lazima
kufikiriwa na kusomwa kwa uhusiano na maelewano kwa ubaba wa Mungu.” Ikiwa
tunasema “Baba Yetu” ni kwa sababu tunasadiki kwamba sisi ni ndugu wa wengine
wengi. Mungu hawabagui watu na hamsahau yeyote wa wana wake. Hapendezwi na sala
ambayo haifikirii ndugu wengine. Mungu si daima anatupa vitu ambavyo
tunamwomba, bali anatupa daima vitu tunavyohitaji kwa sababu anajua kila kitu.
Ikiwa mara nyingi hatupokei vitu ambavyo tunamwomba ni kwa sababu hatuombi
ipasavyo. Labda kutokuwa na tabia na nia kamili iliyodaiwa na Yesu wakati
aliwafundisha wafuasi wake kusali. Tunaalikwa kuishi kwa udugu kutokana na
ubaba wa Mungu na kuwa na mioyo ya wana, kwa sababu mtu asiyeishi kama mwana
hajifunzi kuwa ndugu.
2 Uzoefu wa Ubaba wa
Mungu kwa Mt. Yohana Calabria na kwa Familia yake ya Kiroho
Mantra: Baba yetu sisi ni wanawe, Baba yetu sisi ni
ndugu...
Mt. Yohane Calabria alikuwa mwenye
unyeti daima kwa ishara za utunzaji wa Mungu ulimwenguni. Lakini usiku mmoja
wakati yeye hakupata kulala usingizi, alichukua injili na aliufanya ugunduzi
mkubwa. Aligundua jinsi ya kuishi kwa uhalisi ubaba wa Mungu. Kifungu ambacho
kiliichukua uangalifu wake zaidi kilikuwa Mt 6,24-34. Kutokana na kifungu hiki
alichukua ahadi kwake na kwa familia yake ya kiroho, yaani, “Mtafuteni kwanza
Ufalme wa Mungu na haki yake; na hayo yote mtapewa kwa ziada.” Kulingana naye
kwa kushuhudia duniani kwamba Mungu ni Baba, Mama, Kila Kitu, tunahitaji kwanza
kufanya sisi wenyewe uzoefu wa ubaba wa Mungu na kulima hisia ya miliki ya Baba
huyu. Kama hivyo alimwambia mama fulani: “Sisi ni wa Mungu, Mungu ni Baba, Mama
Kila kitu chetu. Upende Bwana na atakuwa heri (mwenye furaha)” (24-1-1930).
Kwa yeye, “Mungu ni Baba na Baba mwema. Hakuna mama ambaye
anawapenda sana watoto wake kama Mungu anawapenda watu wote na kila mmoja
wetu”. Calabria anaongea pia kuhusu Mungu kama Riziki, kwa sababu kulingana
naye, haiwezekani kutenga Ubaba wa Mungu na Riziki yake. Kwa hivyo, asema,
“Riziki ni Mama mpole ambaye hupatia kila kitu kwa wema wetu, hata kwa wema
wetu mkubwa. Tunapaswa kuhisi tumebebwa kwa mikono yake ya mama”. Yohana Calabria
aliamini katika ukweli huo na aliyapanga maisha na kazi zake zote kulingana na
hali hii. Katika mwanzo mwa kazi yake, alipoonekana mtoto wa kwanza, Yohana
alifahamu kwamba Mungu akatarajia kutoka kwake imani maalum ambayo huonyeshwa
kupitia matendo mema kwa masikini wapendelewa na Mungu. Baada ya mtoto wa
kwanza, wengine wengi walikuja nyumbani. Nyumba hiyo iliitwa “Nyumba ya
wavulana wema”. Kama hii, ishara ya mapenzi ya Mungu ilikuwa wazi sana kwa
Yohana Calabria.
Kupitia uzoefu ambao Mt. Calabria
aliishi kuhusu ubaba wa Mungu, akawa mshahidi na mhubiri wa ubaba huu. Kama
hivyo asema, “Injili anatuongelea, kwa mfano, Mungu ni Baba, anatujali zaidi
kuliko ndege wa angani na maua ya mashamba hata atatujalia kile ambacho
tunahitaji kwa chakula na kwa mavazi, lakini tunapaswa kuutafuta kwanza Ufalme
wake na haki yake. Basi, je, imani yetu katika ubaba wa Mungu ni nzuri? Je,
tena ni nzuri imani yetu katika Riziki yake takatifu na wema?”
Imani kweli na asili inafikiria Mungu si kama
Muumba na Bwana tu, bali kwanza kama Baba”. Mungu ni Baba, hutujali na wote
ambao tunawapenda; macho yake ni makini sana kwa kila kitu; hakuwezi tokea
chochote kisichotarajiwa kama mshangao (bila maana); kila kitu kinapangwa na
kuongozwa na hekima, nguvu na wema wake pasipo mwisho. Juu ya yote tunaweza
kusema kwamba ni kwa wema wake.
Hitimisho
Uzoefu wa ubaba wa Mungu ulimhamasisha
Yohane Calabria kuanza Kazi kubwa. Katika mwanzo, padre Yohane alisaidiwa na
mama yake. Lakini, baada ya wakati mchache, walikuja Mabruda, Mapadre, Masister,
makundi mengi ya watu wasio watawa. Pamoja na padre Yohana, sisi ni Familia ya Kiroho
ya Calabria inayoitwa “Poor Servants of Divine Providence” na kazi yetu ni
kutafuta Ufalme wa Mungu. Hali hii inatokea katika ahadi ya kuifufua imani
duniani kwa Mungu Baba wa wanadamu wote, kupitia kujisalimisha kabisa kwa
Riziki yake. Kiroho yetu ni Injili. Kulingana na Mtakatifu Yohana Calabria,
tunahitaji kurudi kwa Injili daima ili maisha yetu yabadilike na hali
kandokando yetu pia.
Maandiko ya Mt.
Yohana Calabria yanadhihirisha jinsi alivyokuwa na ubinadamu mno, akifahamu
ugumu wa wengine, lakini kwa wakati sawa, alijua kuonyesha njia kamili kwa
ufumbuzi wa matatizo yao. Kutokana na uzoefu wa Mt. Calabria tunajifunza kwamba
Mungu ni Baba mwema na mtoaji bila mwisho, na sisi sote ni ndugu katika Kristo.
Tunaalikwa kuishi kama ndugu kutokana na ubaba wa Mungu na
kuwatendea mema wengine vivyo hivyo tungependa wao watutendee. Kulingana
naye, “Tunapaswa kuwa na kujihisi watumishi, bali kwa utumishi wa Mwenyeji
fulani ambaye ni pia, na kwanza kabisa, Baba. Basi utumishi wetu ni wa wana,
utumishi wa huria na upendo... kama alivyotumika Bwana wetu Yesu Kristo,
mtumishi wa Baba kwa namna ya ajabu, ambaye wakati wa maisha yake ya kibinadamu
alifanya tu kutimiza amri zako: “Ninafanya kama Baba alivyoniamuru kufanya.”
Tumsifu na tumshukuru Mungu Baba kwa kielelezo
cha imani ambacho ni Yohane Calabria na mtume wake duniani kupitia Familia yake
ya Kiroho.
Fr Ndega
Mapitio: Sara